Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰

MASOMO YA MISA, MACHI 29, 2022: JUMANNE: JUMA LA 4 LA KWARESIMA

β€’
Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image

SOMO 1

Eze. 47:1-9, 12

Malaika alinileta mpaka lango la nyumba; na tazama, maji yalitoka chini ya kizingiti cha nyumba, kwa njia ya mashariki, maana upande wa mbele wa nyumba ulielekea upande wa mashariki; nayo maji yakashuka toka chini ya upande wa kuume wa nyumba, upande wa kusini wa madhabahu. Ndipo akanileta nje kwa njia ya lango upande wa kaskazini, akanizungusha kwa njia ya nje mpaka lango la nje, kwa njia yake iliyoelekea mashariki; na tazama, maji yalitoka upande wa kuume. Na alipotoka mtu yule, mwenye uzi wa kupimia mkononi mwake, kwenda masharikini, akapima dhiraa elfu, akanivusha maji yale; maji yakafika mpka viweko vya miguu. Kisha akapima dhiraa elfu, akanivusha maji yale, maji yakafika mpaka magoti. Kisha akapima dhiraa elfu, akanivusha, maji yakafika mpaka viuno. Kisha akapima dhiraa elfu, yakawa mto nisioweza kuuvuka; maana maji yamezidi, maji ya kuogelea, mto usiovukika. Akaniambia, Mwanadamu, je! Umeona haya? Kisha akanichukua, akanirudisha mpaka ukingo wa mto. Basi nikiisha kurudi, tazama, kando ya ukingo wa mto ilikuwapo miti mingi sana, upande huu na upande huu. Ndipo akaniambia, Maji haya yanatoka kwenda pande za nchi ya mashariki, nayo yanashuka mpaka Araba, na kuingia katika bahari; maji yatokezwayo yataingia baharini, na maji yake yataponyeka. Tena itakuwa, kila kiumbe hai kisonganamacho, kila mahali itakapofika mito hiyo, kitaishi; kutakuwapo wingi mkubwa wa samaki, kwa sababu maji haya yamefika huko; maana maji yale yataponyeka, na kila kitu kitaishi popote utakapofikilia mto huo. Na karibu na mto, juu ya ukingo wake, upande huu na upande huu, utamea kila mti wa chakula, ambao majani yake hayatanyauka, wala matunda yake hayatatindika kamwe; utatoa matunda mapya kila mwezi, kwa sababu maji yake yanatoka mahali patakatifu; na matunda yake yatakuwa ni chakula; na majani yake yatakuwa ni dawa. Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 46:1-2, 4-5, 7-8 (K) 7

(K) Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu. Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. (K) Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye juu. Mungu yu katikati yake hautatetemeshwa; Mungu atausaidia asubuhi na mapema. (K) Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu. Njoni myatazame matendo ya Bwana, Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi. (K)

SHANGILIO

Amo. 5:14

Tafuteni mema, wala si mabaya, mpate kuishi, hivyo Bwana, atakuwa pamoja nanyi.

INJILI

Yn. 5:1-3, 5-16

Baada ya hayo palikuwa na sikukuu ya Wayahudi; naye Yesu akakwea kwenda Yerusalemu. Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Betzatha, nayo ina matao matano. Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza. Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane. Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima? Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu. Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende. Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda. Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo. Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwambia yule aliyeponywa, Leo ni sabato, wala si halali kwako kujitwika godoro. Akawajibu, Yeye aliyenifanya kuwa mzima ndiye aliyeniambia, Jitwike godoro lako, uende. Basi wakamwuliza, Yule aliyekuambia, Jitwike uende, ni nani? Lakini yule mtu aliyeponywa hakumjua ni nani; maan aYesu alikuwa amejitenga, kwa sababu palikuwa na watu wengi mahali pale. Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi. Yule akaenda zake, akawapasha habari Wayahudi ya kwamba ni Yesu aliyemfanya kuwa mzima. Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwudhi Yesu, kwa kuwa alitenda hayo siku ya sabato. Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
AckySHINE Solutions
✨ Join AckySHINE for more features! ✨

Comments 50

Please log in or register to comment or reply.
πŸ‘₯ Samson Tibaijuka Guest Jun 16, 2024
Tumaini ni nanga ya roho
πŸ‘₯ Josephine Nduta Guest Jun 16, 2024
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
πŸ‘₯ John Malisa Guest Apr 23, 2024
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
πŸ‘₯ Jacob Kiplangat Guest Mar 6, 2024
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
πŸ‘₯ John Kamande Guest Jan 30, 2024
Mungu ni mwema, wakati wote!
πŸ‘₯ Lydia Wanyama Guest Aug 6, 2023
Tembea kwa imani, si kwa kuona
πŸ‘₯ Josephine Nduta Guest Jul 21, 2023
Wakati wa Mungu ni kamilifu
πŸ‘₯ Henry Mollel Guest Apr 10, 2023
Sifa kwa Bwana!
πŸ‘₯ Agnes Lowassa Guest Dec 1, 2022
Endelea kuwa na imani!
πŸ‘₯ Rose Mwinuka Guest Jun 24, 2022
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
πŸ‘₯ George Tenga Guest Jun 17, 2022
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
πŸ‘₯ Mariam Hassan Guest May 9, 2022
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
πŸ‘₯ Samuel Were Guest Apr 16, 2022
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
πŸ‘₯ Hellen Nduta Guest Mar 17, 2022
Mungu akubariki!
πŸ‘₯ Charles Mchome Guest Dec 31, 2021
Kwa Mungu, yote yanawezekana
πŸ‘₯ Lucy Mahiga Guest Dec 20, 2021
Rehema zake hudumu milele
πŸ‘₯ Alex Nakitare Guest Sep 9, 2021
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
πŸ‘₯ Elizabeth Mrope Guest Jul 12, 2021
Imani inaweza kusogeza milima
πŸ‘₯ George Mallya Guest Jun 26, 2021
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
πŸ‘₯ Margaret Anyango Guest Jun 8, 2021
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
πŸ‘₯ Betty Kimaro Guest Jan 13, 2021
Nakuombea πŸ™
πŸ‘₯ Henry Sokoine Guest Nov 15, 2020
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
πŸ‘₯ Irene Makena Guest Oct 11, 2020
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
πŸ‘₯ Elizabeth Mtei Guest Jul 14, 2020
Neema ya Mungu inatosha kwako
πŸ‘₯ Grace Njuguna Guest Apr 13, 2020
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
πŸ‘₯ Josephine Nekesa Guest Apr 6, 2020
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
πŸ‘₯ Agnes Sumaye Guest Oct 31, 2019
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
πŸ‘₯ Samson Tibaijuka Guest Jul 25, 2019
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
πŸ‘₯ Linda Karimi Guest Dec 24, 2018
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
πŸ‘₯ David Nyerere Guest Dec 19, 2018
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
πŸ‘₯ Monica Nyalandu Guest Dec 15, 2018
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
πŸ‘₯ Victor Kamau Guest Oct 6, 2018
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
πŸ‘₯ Lydia Wanyama Guest Jul 11, 2018
Mwamini Bwana; anajua njia
πŸ‘₯ Stephen Kangethe Guest Apr 4, 2018
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
πŸ‘₯ Benjamin Masanja Guest Jan 21, 2018
Rehema hushinda hukumu
πŸ‘₯ Joseph Kiwanga Guest Sep 16, 2017
Mwamini katika mpango wake.
πŸ‘₯ Andrew Mchome Guest Aug 20, 2017
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
πŸ‘₯ Paul Ndomba Guest Jul 26, 2017
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
πŸ‘₯ Diana Mumbua Guest Apr 17, 2017
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
πŸ‘₯ Nora Lowassa Guest Apr 12, 2017
Dumu katika Bwana.
πŸ‘₯ Jackson Makori Guest Feb 16, 2017
Katika imani, yote yanawezekana
πŸ‘₯ Rose Mwinuka Guest Feb 2, 2017
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
πŸ‘₯ Anna Mahiga Guest Dec 10, 2016
Neema na amani iwe nawe.
πŸ‘₯ Hellen Nduta Guest Sep 11, 2016
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
πŸ‘₯ Charles Mboje Guest Nov 3, 2015
Nguvu hutoka kwa Bwana
πŸ‘₯ Janet Mbithe Guest Sep 7, 2015
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
πŸ‘₯ Catherine Naliaka Guest Jul 26, 2015
Baraka kwako na familia yako.
πŸ‘₯ Francis Mrope Guest Jul 13, 2015
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
πŸ‘₯ Edwin Ndambuki Guest Jun 1, 2015
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
πŸ‘₯ Francis Njeru Guest May 12, 2015
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida

πŸ”— Related Posts

🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About