Vipimo Vya Wali
Mchele wa Basmati/Pishori - 1 kilo moja
Vitunguu maji - 3
Karoti - 2
Siagi - 3 vijiko vya supu
Kidonge cha supu (stock) - 1 kimoja
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
รsha mchele uroweke kama saa moja au mbili
Katakata vitunguu vipande vidogodogo (chopped) weka kando.
Kwaruza karoti (grate) weka kando.
Tia siagi katika sufuria ya kupikia wali, weka katika moto iyayuke
Kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi kiasi tu.
Tia maji kiasi ya kupikia wali, changanya na kidonge cha supu.
Yakichemka tia mchele, koroga, funika uweke moto mdogo mdogo.
Kabla ya maji kukauka tia karoti changanya wali kisha funika uive kama unavyopika pilau.
Vipimo Vya Kuku Wa Kukaanga
Kuku alokatwakatwa - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa - 2 vijiko vya supu
Bizari ya mchanganyiko/garam masala - kijiko cha supu
Mtindi/Yoghurt - 1 kijiko cha supu
Ndimu - 1
Chumvi - kiasi
Mafuta ya kukaangia - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Ukishamuosha kuku, mchuje atoke maji yote.
Changanya viungo vyote katika kibakuli kidogo.
Changanya pamoja na kuku kisha acha akolee viungo (marinate) kwa muda wa masaa mawili takriban.
Weka mafuta katika karai na kaanga kuku, akiwiva yu tayari kuliwa na wali.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!