Viamba upishi
Mboga za majani makavu ΒΌ kg
Mafuta vijiko vikubwa 3-4
Karanga zilizosagwa kikombe Β½
Maziwa au tui la nazi kikombe 1
Kitunguu 1
Nyanya 2
Chumvi (kama kuna ulazima)
Maji baridi
Hatua
β’ Loweka mboga za majani makavu na maji kwa dakika 10-15.
β’ Osha , mboga na katakata nyanya na vitunguu.
β’ Kangaa, pukusua na saga karanga zilainike.
β’ Kanga kitunguu, weka nyanya, koroga zilainike.
β’ Ongeza mboga zilizolowekwa na maji yake kwenye rojo, koroga na funikia mpaka maji yakaukie na ive. Punguza moto.
β’ Koroga karanga zilizosagwa na maji, ongeza kwenye mboga ukikoroga kwa dakika 5.
β’ Onja chumvi, pakua kama kitoweo.
Uwezekano
Weka nyanya kidogo.
Tumia tui la nazi au krimu badala ya maziwa.
Weka nyama au dagaa au Mayai badala ya Karanga.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!