Viamba upishi
Unga 1 Magi (vikombe vya chai)
Sukari ya browni ยฝ Magi
Siagi iliyoyayushwa 125ย g
Nazi iliyokunwa ยฝ Magi
Mjazo wa karameli (Caramel filling)
Syrup 1/3 kikombe cha chai
Siagi iliyoyayushwa 125ย g
Maziwa matamu ya mgando 2 vikopo (condensed milk)
Mjazo wa chokoleti (Chocolate filling)
Chokoleti 185ย g (dark chocolate)
Mafuta 3 Vijiko vya chai
Jinsi ya kuandaa na kupika
1. Changanya unga, sukari, siagi na nazi iliyokunwa kwenye bakuli mpaka unga ushikamane.
2. Paka mafuta treya ya kuchomea kisha utandaze kwenye treya ya 20cm kwa 30ย cm au (8 in kwa 12 in) unaweza kuweka karatasi ya kuchomea chini ukipenda.
3. Choma kwenye moto 325หC kwa muda wa dakika 15 mpaka 18 au mpaka ibadilike kuwa rangi ya browni.
4. Kwenye sufuria ndogo tia syrup siagi na maziwa matamu ya mgando na changanya kwa moto mdogo mpaka uwe mzito kasha mimina juu ya keki uliyochoma na choma tena kwa muda wa dakika 20 mpaka karameli iwe rangi ya dhahabu.
5. Kwenye sufuria ndogo nyingine tia vipande vya chokoleti na mafuta na ukoroge kwa moto mdogo mpaka iyayuke kisha wacha ipoe kidogo mimina juu ya mjazo wa karameli kisha weka kwenye friji mpaka ishikamane.
6. Kata vipande weka kwenye sahani tiyari kwa kuliwa
No comments yet. Be the first to share your thoughts!