Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰

Ziara za kushtukiza zinachekesha sana

β€’
Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image

Mimi Nimecheka sana
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

ZIARA ZA KUSHTUKIZAπŸ˜€πŸ˜€
Mimi ni msomaji mzuri wa magazeti, na msikilizaji mzuri wa redio, huwa naangalia luninga mara chache sana kama nikibahatika kupita mahala kuna luninga. Sasa wiki hii nimesikia mengi kuhusu hizi ziara za kushtukiza za viongozi wetu, nikaona hili ni jambo zuri tena linafaa kuigwa na sisi wananchi wapenda maendeleo. Nikaona nijipange na mimi nifanye ziara kadhaa za kushtukiza katika sehemu mbalimbali zinazonihusu.

Nikaona nianze na ziara ya kushtukiza pale shuleni kwa huyu mwanangu, maana kila siku anakunywa chai na kuondoka na daftari zake na mie sijawahi kwenda shuleni kwao toka nilipomuandikisha shule mwezi Januari. Nilifika shuleni na kumuona mwalimu mkuu, ambae alianza kutetemeka nilipomuambia kuwa nimekuja pale kwa ziara ya kustukiza, sijui alidhani mi ni mmoja wa Mawaziri wapya, maana nilimuona jasho linamtiririka ghafla. Akanikaribisha ofisi yake iliyokuwa na vitabu kila kona, na kuita waalimu wote na kunitambulisha kuwa ni kiongozi nimekuja kwenye ziara ya kustukiza.

Nilipojitambulisha kuwa ni mzazi, waalimu wote nikawaona waanza kupumua kwa raha. Nikawaambia kuwa mimi nina mwanafunzi pale na nilikuja ziara ya kustukiza kujua maendeleo yake. Baada ya mwalimu mkuu kusaka jina la mwanangu nae akanambia, β€œMzee huyu mtoto hajaja shule mwezi wa tatu sasa, tulijaribu kukutafuta ikashindikana, hatujui yu wapi” Jasho likaanza kunitoka mimi, yule mtoto kila asubuhi nampa nauli anaenda shule, na mara nyingi ananiomba michango kumbe hata shule haji. Niliondoka bila kuaga presha ikiwa juu.

Nikaona niende kwenye genge la mke wangu nae nikamfanyie ziara ya ghafla nimhadithie mambo ya mwanae, nilipofika pale nikakuta kuna mdada mwingine anauza genge. Nikamsalimu, na kumuuliza mwenye genge ntampataje, jibu lake lingeniua kama ningekuwa si mkakamavu, β€œMume wake kaja kumchukua na gari wameenda kununua shamba Bagamoyo”. Nikaondoka nimechanganyikiwa, nikajuwa hapa dawa yangu moja tu, nayo ni Sabrina, mtoto wa Kinyaturu pale ambapo nikipata maudhi huwa naenda kubembelezwa.

Nikatwanga mguu kwa Sabrina nae nikamfanyie ziara ya ghafla ili anipoze moyo. Nilipogonga mlango wa chumba chake akatoka mbaba wa miraba minne, akanisalimia kwa upole, β€œSalama kaka unasemaje?” Jibu likanitoka β€œSamahani mie nilimkopesha huyu dada wa chumba hiki vitenge, nilikuja kuuliza kama ameshapata hela yangu” Ziara za kushtukiza zinataka moyo wa chuma jamani

AckySHINE Solutions
✨ Join AckySHINE for more features! ✨

Comments 236

Please log in or register to comment or reply.
πŸ‘₯ Moses Mwita Guest Sep 7, 2019
Wow, hii kichekesho ni mshindi kamili! πŸ†
πŸ‘₯ Rahim Guest Sep 4, 2019
Hii imeniboresha wakati wangu wa mapumziko! β˜•πŸ˜†
πŸ‘₯ John Lissu Guest Jul 16, 2019
😁 Kicheko bora ya siku!
πŸ‘₯ Moses Mwita Guest May 31, 2019
Hii ni ya kufurahisha! πŸ˜„πŸ˜…
πŸ‘₯ Fatuma Guest May 20, 2019
πŸ˜„ Umeimaliza kabisa!
πŸ‘₯ Irene Makena Guest May 14, 2019
Kweli mna kipaji cha ucheshi! πŸ‘πŸ€£
πŸ‘₯ Rose Mwinuka Guest May 3, 2019
Nimecheka hadi machozi yanatoka! 🀣😭
πŸ‘₯ David Nyerere Guest Apr 8, 2019
Nilihitaji kicheko hiki, asante kwa kushiriki! πŸ˜…
πŸ‘₯ Charles Mboje Guest Feb 16, 2019
πŸ˜„πŸ˜…πŸ‘πŸ˜‚
πŸ‘₯ Catherine Mkumbo Guest Feb 13, 2019
Haha! Sijacheka hivi kwa muda mrefu! 🀣
πŸ‘₯ Binti Guest Feb 11, 2019
πŸ˜‚ Nalia kwa kweli hapa!
πŸ‘₯ Mwajabu Guest Feb 8, 2019
🀣 Hiyo punchline ilikuwa haikutarajiwa!
πŸ‘₯ Joseph Njoroge Guest Nov 19, 2018
Hii imenifurahisha hadi ninacheka kwa sauti! πŸ˜„πŸ˜…
πŸ‘₯ Hellen Nduta Guest Nov 14, 2018
Nimefurahia sana hii! πŸ˜…πŸ˜Š
πŸ‘₯ Thomas Mtaki Guest Nov 2, 2018
πŸ€£πŸ€£πŸ˜„πŸ˜†
πŸ‘₯ Joy Wacera Guest Oct 30, 2018
Hii ni bomba sana! πŸ€£πŸ‘
πŸ‘₯ Samson Mahiga Guest Oct 17, 2018
πŸ€£πŸ€£πŸ˜‚
πŸ‘₯ Rose Lowassa Guest Oct 10, 2018
Hii ni joke ya kufurahisha sana! πŸ‘πŸ˜†
πŸ‘₯ Alice Wanjiru Guest Oct 7, 2018
Hii imenifurahisha sana! πŸ˜ŠπŸ˜…
πŸ‘₯ Stephen Kangethe Guest Oct 1, 2018
πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜‚πŸ˜…
πŸ‘₯ Patrick Akech Guest Oct 1, 2018
🀣 Kichekesho bora kabisa!
πŸ‘₯ Moses Kipkemboi Guest Aug 3, 2018
Hii ni dhahabu ya vichekesho! πŸ˜„
πŸ‘₯ David Ochieng Guest Aug 1, 2018
πŸ˜‚ Ninaituma hii kwa kila mtu ninayemjua!
πŸ‘₯ Philip Nyaga Guest Jul 27, 2018
Nimecheka hadi nimemiss kicheko! πŸ˜ŠπŸ˜‚
πŸ‘₯ Sarah Karani Guest Jul 8, 2018
πŸ˜‚πŸ˜†
πŸ‘₯ Nora Lowassa Guest Jun 30, 2018
Hii kichekesho imenifurahisha sanaβ€”imebamba! 🀣
πŸ‘₯ Selemani Guest Jun 26, 2018
πŸ˜‚ Nitaiiba hii bila shaka!
πŸ‘₯ Brian Karanja Guest Jun 26, 2018
πŸ˜‚πŸ˜‚
πŸ‘₯ Chris Okello Guest Jun 18, 2018
Kama kawaida! Bado nacheka! πŸ˜„
πŸ‘₯ George Mallya Guest May 23, 2018
Hii imenifurahisha sana! πŸ˜‚πŸ˜‚
πŸ‘₯ David Nyerere Guest May 4, 2018
πŸ˜† Nacheka hadi chini sasa hivi!
πŸ‘₯ David Kawawa Guest May 2, 2018
Mna kipaji cha ucheshi! πŸ‘πŸ˜‚
πŸ‘₯ Victor Malima Guest Apr 20, 2018
Kweli mnajua kuchekesha! πŸ˜‚πŸ˜‚
πŸ‘₯ Halimah Guest Apr 5, 2018
😁 Hii ni hazina ya kichekesho!
πŸ‘₯ David Sokoine Guest Mar 1, 2018
Nimecheka hadi nina furaha sana! 🀣😊
πŸ‘₯ Mwagonda Guest Feb 11, 2018
πŸ˜‚ Siwezi kuacha kucheka na hii!
πŸ‘₯ Nora Kidata Guest Jan 17, 2018
πŸ˜‚πŸ‘ŒπŸ˜†πŸ˜Š
πŸ‘₯ Kheri Guest Jan 16, 2018
πŸ˜‚ Ninaihifadhi hii!
πŸ‘₯ Samuel Omondi Guest Dec 26, 2017
Umeimaliza kabisa, kichekesho gani! πŸ˜„
πŸ‘₯ Elizabeth Mrope Guest Dec 4, 2017
Hii imenifurahisha hadi nacheka kwa sauti! πŸ€£πŸ˜…
πŸ‘₯ Arifa Guest Nov 8, 2017
πŸ˜† Siwezi kuacha kucheka!
πŸ‘₯ Alex Nyamweya Guest Oct 24, 2017
Umetisha! πŸ‘ŒπŸ˜‚
πŸ‘₯ Husna Guest Oct 3, 2017
Bado nacheka, hiyo ilikuwa nzuri sana! 🀣
πŸ‘₯ Philip Nyaga Guest Sep 15, 2017
🀣 Ninaituma sasa hivi!
πŸ‘₯ Stephen Mushi Guest Sep 10, 2017
Nimecheka hadi machozi yanatoka! 🀣😭
πŸ‘₯ Mgeni Guest Sep 5, 2017
Hii kichekesho ilikuwa bora! Nimeipenda! 🎯
πŸ‘₯ Wilson Ombati Guest Aug 24, 2017
πŸ€£πŸ€£πŸ‘πŸ˜†
πŸ‘₯ Sarah Karani Guest Jul 24, 2017
🀣 Sikutarajia hiyo!
πŸ‘₯ Philip Nyaga Guest Jul 17, 2017
πŸ˜† Ninacheka sana sasa hivi!
πŸ‘₯ Michael Mboya Guest Jun 22, 2017
πŸ˜‚πŸ˜…
πŸ‘₯ Mary Njeri Guest May 31, 2017
😁 Hii imenifanya siku yangu iwe bora!
πŸ‘₯ Azima Guest May 31, 2017
πŸ˜„ Umeshinda mtandao leo!
πŸ‘₯ Sharon Kibiru Guest May 27, 2017
πŸ˜‚ Lazima nihifadhi hii!
πŸ‘₯ Dorothy Nkya Guest May 17, 2017
πŸ˜†πŸ˜…πŸ˜‚
πŸ‘₯ James Mduma Guest Apr 27, 2017
😁 Hii ni dhahabu!
πŸ‘₯ Emily Chepngeno Guest Apr 15, 2017
🀣 Hii imenifanya siku yangu iwe bora kabisa!
πŸ‘₯ James Kawawa Guest Apr 14, 2017
Hii imenipa kicheko cha siku! πŸ˜ŠπŸ˜†
πŸ‘₯ Nora Lowassa Guest Apr 10, 2017
Hii kichekesho itaingia moja kwa moja kwenye vipendwa vyangu! πŸ˜‚
πŸ‘₯ John Malisa Guest Mar 30, 2017
Kweli ni jokes za ukweli! πŸ‘πŸ˜†
πŸ‘₯ Charles Mrope Guest Mar 1, 2017
Hii imenifurahisha hadi nacheka kwa sauti! πŸ˜‚πŸ€£

πŸ”— Related Posts

🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About