Sidebar with Floating Button
AckySHINE 🔁

Mambo ya Msingi unayotakiwa kufahamu kuhusu Sakramenti ya Daraja

Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image
Daraja na ndoa ni tofauti na sakramenti nyingine kwa sababu gani?
Daraja na ndoa ni tofauti na sakramenti nyingine kwa sababu hazilengi hasa faida ya mtu anayezipokea, bali huduma zake kwa ajili ya Kanisa na jamii. Daraja inatia uwezo wa Kristo kwa ustawi wa Kanisa, Bibi arusi wake. Ndoa inatia upendo wake mwaminifu kwa ustawi wa familia, kanisa dogo la nyumbani.
“Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe” (Mdo 20:28).
“Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa. Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake. Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa” (Ef 5:29-32).

Je, daraja takatifu zinahitajiwa kabisa na Kanisa?
Ndiyo, daraja takatifu zinahitajiwa kabisa na Kanisa kwa sababu kazi ya wokovu haimtegemei binadamu, bali Mungu.
“Hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni. Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu” (Eb 5:4-5),
Yesu alisisitiza alivyopewa na Baba uwezo wa kutuokoa. “Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake” (Yoh 3:35).
“Kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele” (Yoh 17:2)
.
Kisha kufufuka alitumia mamlaka hiyo kuwatuma wanafunzi kumi na mmoja waliobaki:
“Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa dahari” (Math 28:18-20).
Mpaka mwisho wa dunia uwezo huo wa Kimungu utatolewa tu kwa sakramenti ya daraja, inayounganisha mtu na Mitume kupitia mlolongo usiokatika wa kuwekewa mikono ili kushirikishwa mamlaka. Bila yake, kuna upungufu katika ufundishaji, utoaji wa sakramenti na uongozi.

Je, wenye daraja wanastahili heshima?
Ndiyo, wenye daraja wanastahili heshima kwa sababu ya mamlaka ya Kiroho waliyonayo kutoka kwa Kristo.
“Amin, amin, nawaambieni: Yeye ampokeaye mtu yeyote nimpelekaye, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi ampokea yeye aliyenipeleka” (Yoh 13:20).
“Jaribu lililowapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa, bali mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama Kristo Yesu” (Gal 4:14).
“Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii” (Tito 3:1).
Wenye daraja wanaotimiza kazi zao vizuri wanastahili heshima kwa uaminifu wao pia.
“Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu, hasa hao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha” (1Tim 5:17).

Je, wenye daraja wanaweza wakatenda dhambi?
Ndiyo, wenye daraja wanaweza wakatenda dhambi kwa sababu ni binadamu kama sisi sote. Yesu alionja ukosefu wa Mitume hasa wakati wa mateso.
“Je, mimi sikuwachagua ninyi Thenashara, na mmoja wenu ni shetani?” (Yoh 6:70).
“Tazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao, na kuniacha mimi peke yangu” (Yoh 16:32).
Paulo alionya mapadri, “Katika ninyi wenyewe watainuka watu, wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao” (Mdo 20:30).

Ili tuwe na wachungaji wengi waaminifu tunapaswa kufanya nini?
Ili tuwe na wachungaji wengi waaminifu tunapaswa hasa kusali.
“Mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake” (Math 9:38).
Halafu yanahitajika maandalizi ya muda mrefu, juhudi na ushirikiano wa kidugu.
“Asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi… Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia… Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine” (1Tim 3:6; 4:16; 5:22).

Je, wanawake wanaweza kupewa daraja?, Mwanamke anaweza kuwa padri?
Hapana, wanawake hawawezi kupewa daraja, kwa sababu kwa karibu miaka elfu mbili mfululizo Kanisa limejiona halina mamlaka ya kufanya tofauti na Yesu. Yeye alichagua wanaume tu kuwa Mitume wake, ingawa walikuwepo wanawake waaminifu kuliko wengi wao, hasa Maria, mtakatifu kuliko wote.
“Petro, na Yohane, na Yakobo, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo wa Alfayo, na Simoni Zelote, na Yuda wa Yakobo. Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake… Wakaweka wawili, Yusufu, aitwaye Barsaba, aliyekuwa na jina la pili Yusto, na Mathiya… kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja” (Mdo 1:13-14,23,26).
“Walimchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia; ambao wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao” (Mdo 6:5-6).

Je, kutoa daraja kwa wanaume tu ni kuwakosea haki wanawake?
Hapana, kutoa daraja kwa wanaume tu si kuwakosea haki wanawake, kwa kuwa hizo ni huduma zinazofaidisha wote.
“Maana aliye mkubwa ni yupi? Yeye aketiye chakulani, au yule atumikaye? Siye yule aketiye chakulani? Lakini mimi kati yenu ni kama atumikaye” (Lk 22:27).
Mwenye daraja anahudumia Kanisa kwa kumwakilisha Yesu; hivyo anatakiwa kuwa mwanamume kama yeye mbele ya Bibiarusi wake. Kukubali mgawanyo wa majukumu maishani ni kusifu hekima ya Mungu aliyetuumba watu wa jinsia mbili tofauti ili kustawisha familia, jamii na Kanisa.
“Walakini si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke, katika Bwana… Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake” (1Kor 11:11; 12:27).

Je, mwenye daraja anaweza kuwa na ndoa?
Ndiyo, mwenye daraja anaweza kuwa na ndoa.
“Hatuna uwezo kuchukua pamoja nasi mke aliye ndugu, kama wao mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa?” (1Kor 9:5).
Paulo, akiwa mseja, hakudai kila mmojawao aoe, ila asiwe ameoa mara mbili, bali “mume wa mke mmoja” (1Tim 3:2; Tit 1:6), kama alivyoagiza mjane aandikishwe akiwa tu “mke wa mume mmoja” (1Tim 5:9).
Polepole mang’amuzi yakaelekeza Kanisa kubana nafasi hiyo kwa Maaskofu, na katika majimbo mengi kwa mapadri pia. Useja mtakatifu unawalinganisha zaidi na Yesu na kuwaachia uhuru wa moyo na wa muda kwa ajili ya huduma.
“Wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee” (Math 19:12).

Ni zipi Sakramenti za Huduma ya ushirika na utume?
Ni Sakramenti mbili ambazo ni Sakramenti ya Daraja na Sakramenti ya Ndoa

Sakramenti ya Daraja ndiyo nini?
Sakramenti ya Daraja ndiyo Sakramenti ambayo mwanamme mkatoliki aliyeitwa na Mungu hupata mamlaka na neema ya kuendeleza ndani ya Kanisa Utume Kristo aliowakabidhi Mitume wake

Ni kwa nini inaitwa Sakramenti ya Daraja?
Inaitwa Sakramenti ya Daraja kwa sababu mtu anapata Sakramenti hii kwa kuweka wakfu kwa ibada ya pekee inayomwezesha kwa nguvu ya Roho Mtakatifu atumie uwezo Mtakatifu kwa niaba na mamlaka ya Yesu Kristo ili kuhudumia Taifa la Mungu

Sakramenti ya Daraja ina ngazi ngapi?
Sakramenti ya Daraja inazo ngazi tatu, nazo ni Ushemasi, Upadre, Uaskofu

Ibada ya kutolea Daraja ya uaskofu ina matokeo gani?
Ibada ya kutolea Daraja ya uaskofu ina matokeo yafuatayo;
1. Inampa utimilifu wa SSakramenti ya Daraja Takatifu 2. Askofu anakuwa Mwandamizi rasmi wa Mitume 3. Inampa Askofu ushirika na Papa na maaskofu wengine wa kuwajibikia Makanisa yote 4. Inampa uwezo wa kufundisha, kutakasa na kuongoza

Askofu ni nani?
Askofu ndiye mchungaji mkuu wa kanisa Mahalia au Jimbo lake

Askofu ana kazi gani katika Jimbo lake?
Askofu katika Jimbo lake anamwakilisha Kristo akitimiza kazi ya kichungaji akisaidiwa na mapadri na mashemasi wake.
Askofu ni kiongozi wa kiroho katika jimbo mahalia. Na sio mambo ya kiroho tu ila hata ya kijamii lakini watu/mtu akiitaji ufafanuzi na msaada toka kwake.
Kazi zake ni:- 1. Kuliongoza taifa la Mungu alilopewa yaani wakristo/wengineo pia 2. Kusimamia na kuongoza Litrujia katika eneo husika. 3. Kueneza amani kwa kupitia karama na wadhifa aliopewa na Mungu. 4. Kueneza upendo katika eneo/jimbo mahalia. 5. Mtoa kauli ya mwisho kwa mambo ya kikanisa katika jimbo. 6. Kusimamia miito ya kanisa na kuchochea bila kukata tamaa 7. Kusimamia baraza la walei na kulishauri kwa kutolea kauli ya Mwisho kabla ya kwenda kwingine 8. Kuwashauri watu waliokata tamaa au kushindikana katika ngazi za chini
NB. Hivyo ndani ya kanisa kuna miogozo ili kupata nafasi zisizokinzana

Ni nani ampaye padri Daraja la Uaskofu?
Ni Baba Mtakatifu pekee au humteua Askofu mmoja akisaidiwa na maaskofu wengine wawili humweka wakfu Padri huyo kuwa Askofu (Mt 13:2-3)

Baba Mtakatifu ni nani?
1. Ndiye Askofu Mkuu wa Maaskofu wote
2. Ndiye mchungaji mkuu wa Wakatoliki wote hapa duniani 3. Ni Wakili wa Yesu Kristo hapa duniani. (Mt 16:18-19; Yoh 21:15-17).

Ibada ya Daraja inachapa alama gani nafsini mwa aliyepewa?
1. Ibada ya Daraja inatia rohoni alama isiyofutika
2. Inamlinganisha mpokeaji na Kristo Kuhani 3. Inamwezesha mwenye Daraja kutenda kwa Jina la Yesu aliye Kichwa cha Kanisa

Kwa Sakramenti ya Daraja Padri anapata mamlaka gani?
Kwa Sakramenti ya Daraja Padri anapata mamlaka ya 1. Kuadhimisha sadaka ya Misa Takatifu na kutakasa watu kwa njia ya Sakramenti.
2. Kuhubiri neno la Mungu 3. Kuwaongoza watu (Ebr 5:1-4)

Ni nani wenye uwezo wa kutoa Sakramenti ya Daraja?
Wanaotoa Sakramenti ya Daraja Katika ngazi tatu Uaskofu, Upadre, Ushemasi ni Maaskofu waliopewa Daraja halisi kama waandamizi wa Mitume.

Ni nani aweza kupewa kihalali Sakramenti ya Daraja Takatifu?
Mwenye kupewa kihalali Sakramenti ya Daraja Takatifu ni Mwanaume peke yake aliyebatizwa, akiwa na wito nasifa zinazotakiwa na kukubaliwa na Mamlaka ya Kanisa. Ndivyo Yesu Kristu alivyotaka mwenyewe

Alama wazi ya Sakramenti ya Daraja Takatifu ni nini?
Alama wazi ya Sakramenti ya Daraja Takatifu ni kuweka mikono juu ya yule anayepewa Daraja na kutamka maneneo ya sala ya wakfu.

Anayetaka kuwa padri yampasa nini?
Yampasa; 1. Awe na tabia njema, akili za kutosha na afya nzuri.
2. Apende sana wokovu wa watu na kujitolea kwa huduma ya Mungu 3. Awe tayari kuishi hali ya useja maisha yake yote

Kwa sababu gani cheo cha Padri ni kikubwa sana?
Kwa sababu Padri anashiriki Upadri wa Yesu Kristo na ni mjumbe kati ya Mungu na Mwanadamu

Yatupasa nini kwa wenye Daraja Takatifu?
Yatupasa 1. Kuwaheshimu
2. Kuwasikiliza na kufuata mafundisho yao 4. Kuwasaidia katika utumishi wao kwa Sala na sadaka zetu

Matokeo ya Sakramenti ya Daraja ni yapi?
1. Inaleta mmiminiko wa kipekee wa Roho Mtakatifuambao unamlinganisha mhusika na Kristo
2. Inatia alama ya kiroho isiyofutika. kwa hiyo haiwezi kurudiwa au kutolewa kwa muda tuu.
AckySHINE Solutions
✨ Join AckySHINE for more features! ✨

Comments 50

Please log in or register to comment or reply.
👥 Diana Mumbua Guest Jul 2, 2024
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
👥 Alex Nakitare Guest Jun 9, 2024
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
👥 Anna Mchome Guest Feb 9, 2024
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
👥 Alex Nyamweya Guest Feb 9, 2024
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
👥 Peter Mugendi Guest Oct 2, 2023
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
👥 Diana Mumbua Guest Jul 18, 2023
Imani inaweza kusogeza milima
👥 John Mwangi Guest Feb 9, 2023
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
👥 Agnes Lowassa Guest Jan 23, 2023
Nguvu hutoka kwa Bwana
👥 Tabitha Okumu Guest Oct 20, 2022
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
👥 Dorothy Majaliwa Guest Aug 7, 2022
Neema ya Mungu inatosha kwako
👥 Moses Kipkemboi Guest Aug 5, 2022
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
👥 Jane Muthoni Guest Aug 5, 2022
Mwamini katika mpango wake.
👥 Nora Kidata Guest Jun 4, 2022
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
👥 Grace Mushi Guest Jan 30, 2022
Nakuombea 🙏
👥 Nancy Kabura Guest Jan 24, 2022
Sifa kwa Bwana!
👥 Faith Kariuki Guest Jan 10, 2022
Rehema zake hudumu milele
👥 Frank Macha Guest Nov 14, 2021
Tembea kwa imani, si kwa kuona
👥 Peter Mugendi Guest Oct 21, 2021
Dumu katika Bwana.
👥 Mariam Kawawa Guest Sep 22, 2021
Katika imani, yote yanawezekana
👥 Victor Mwalimu Guest Aug 6, 2021
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
👥 Janet Sumaye Guest Mar 7, 2021
Mungu ni mwema, wakati wote!
👥 Simon Kiprono Guest Jul 10, 2020
Wakati wa Mungu ni kamilifu
👥 John Lissu Guest Jun 15, 2020
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
👥 Grace Njuguna Guest May 29, 2020
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
👥 Rose Kiwanga Guest Apr 22, 2020
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
👥 Peter Mbise Guest Feb 26, 2020
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
👥 Benjamin Masanja Guest Oct 4, 2019
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
👥 Moses Kipkemboi Guest Sep 24, 2019
Mwamini Bwana; anajua njia
👥 Alice Mrema Guest Mar 6, 2019
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
👥 Edward Chepkoech Guest Jan 16, 2019
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
👥 John Mushi Guest Dec 8, 2018
Kwa Mungu, yote yanawezekana
👥 Andrew Mahiga Guest May 22, 2018
Tumaini ni nanga ya roho
👥 Elizabeth Mrope Guest May 16, 2018
Baraka kwako na familia yako.
👥 Lucy Wangui Guest Feb 7, 2018
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
👥 John Malisa Guest May 28, 2017
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
👥 Raphael Okoth Guest May 17, 2017
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
👥 Kenneth Murithi Guest Apr 9, 2017
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
👥 Edward Lowassa Guest Dec 13, 2016
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
👥 Francis Mrope Guest Oct 28, 2016
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
👥 Robert Okello Guest Sep 19, 2016
Endelea kuwa na imani!
👥 Victor Mwalimu Guest Sep 13, 2016
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
👥 Betty Kimaro Guest Jun 21, 2016
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
👥 Victor Kamau Guest Feb 26, 2016
Rehema hushinda hukumu
👥 Patrick Akech Guest Dec 14, 2015
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
👥 Josephine Nekesa Guest Dec 9, 2015
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
👥 Raphael Okoth Guest Sep 1, 2015
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
👥 John Lissu Guest Aug 27, 2015
Mungu akubariki!
👥 Mary Kendi Guest Aug 7, 2015
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
👥 Kevin Maina Guest May 18, 2015
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
👥 Esther Nyambura Guest Apr 4, 2015
Neema na amani iwe nawe.

🔗 Related Posts

🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About