Nikitafuta rafiki kwa nia ya kuoana (mchumba), je ni sifa gani niangalie kwa msichana/mvulana?
Date: April 17, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Kuchagua mchumba ni moja ya maamuzi ambayo kijana anahitaji kuyafanya kwa uangalifu mkubwa sana. Kwa sababu huyo ndiye atakayekuwa mwenzi wake wa maisha. Katika kuchagua mchumba kila mtu ana mawazo yake kuhusiana na kilicho muhimu kuzingatiwa. Mara nyingi mhemuko una nguvu zaidi kuliko uamuzi wa kimantiki
Hata hivyo, vifuatavyo ni kati ya vigezo ambavyo vinaweza kuangaliwa:
β’ Chagua mtu anayekuheshimu wewe na wengine; Chagua mtu unayemwamini;
β’ Chagua mtu ambaye unaweza kuongea, kujadiliana, na kuhojiana naye kwa uwazi bila kugombana;
β’ Chagua mtu mwenye umri unaokaribiana na wa kwako;
β’ Chagua mtu anayependelea vile unavyopendelea;
β’ Chagua mtu ambaye ataelewa matatizo yako na yuko tayari kukusaidia kuyatatua; na
β’ Chagua mtu mwenye afya nzuri.
Hii inamaanisha pia kumpata mtu ambaye kabla ya kuanza kujaamiana naye, atakuwa tayari kwenda kupima kwa hiari kujua hali yake ya VVU na pia kuwa tayari kutumia kinga kwa maana ya kondomu hadi hapo mtakapojua hali zenu.
Wafahamishe wazazi wako mtu uliyemchagua kama mchumba na mtambulishe kwao i ili wamfahamu na yeye awafahamu wazazi wako. Wakati huohuo na wewe jaribu kuwafahamu wazazi wake. Usifanye uchumba wa haraka. Pata muda wa kutosha kumwelewa rafiki yako.
Please log in or register to leave a comment or reply.
Related Posts
Pombe ina tabia ya kufanya ubongo kushindwa kufikiri, na
kushindwa kujizuia na vishawishi vy...
Read More
Ndiyo, baada ya muda fulani karibia watu wote wenye maambukizi ya Virusi vya UKIMWI wataanza kuug...
Read More
Hapana, hamna njia ya kufahamu kama amempa msichana mimba siku i ileile wanapojamii ana. Inachuku...
Read More
Ngozi ya Albino haina jinsi ya kujilinda na mionzi ya jua. Inaungua
sana baada ya kupatwa na...
Read More
Kama kati ya mwanamke na mwanaume hakuna mwenye magonjwa ya zinaa, hakuna madhara yoyote kwa mwan...
Read More
Je, unajua kwamba wengi wetu tunapenda kufanya mapenzi ya kawaida? Na pia unajua kwamba kuna wale...
Read More
Je, ni muhimu kwa washiriki wote kufikia kilele wakati wa ngono/kufanya mapenzi?
Wakati wa...
Read More
Wakati mwingine kuwa na muonekano tofauti na watu wengine
huvuta udadisi. Na hasa tukikumbuk...
Read More
Kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na msichana ni jambo zuri sana. Hata hivyo, kuwa na ukaribu wa ...
Read More
Ndiyo. Unaweza kufa kutokana na kuvuta sigara au kunywa
pombe. Lakini pale tu utakapozidisha...
Read More
Kwa nini sio Sahihi Kufanya Ngono na Mtu Mmoja wa Marafiki? πΈπ
Jambo zuri siku zote ...
Read More
Je, Ni Vipi Kujilinda na Maambukizi ya Kisonono na Kaswende? π
Karibu, vijana wapendwa!...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!