Je, ninaweza kuambukizwa na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI kwa kuumwa na mbu?

✍️ SW - Melkisedeck ShineπŸ“… 2022-04-17 08:24:41πŸ’¬ 0 comments⏱️ ~1 min read
πŸ“„ PDF

Hapana, mbu na wadudu wengine hawawezi i kukuambukiza virusi vya UKIMWI kutokana na mfumo wa mii li yao. Virusi vya UKIMWI haviwezi kuishi kwenye mii li yao, kwa sababu siyo mazingira vinavyoyapenda. Virusi vya UKIMWI vinajilisha na kuzaliana katika chembechembe nyeupe za damu, lakini chembechembe za aina hii hazipo katika mwili wa mbu. Kwa hiyo, virusi vya UKIMWI vinakufa mara baada ya mbu kufyonza damu na akingβ€˜ata mtu mwingine baadaye hakuna hatari ya kuambukizwa.
Thibitisho jingine la ukweli huu ni kwamba sisi sote tungekuwa tumebeba virusi vya UKIMWI kama mbu angelikuwa anaambukiza kwa sababu sisi sote tunaishi katika mazingira yenye mbu na karibu na watu wengine.

πŸ’¬

Discussion

Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.

0 comment(s)
πŸ” Login required to comment or reply

You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.

Log in to participate
No comments yet.