MAHITAJI
Nyama iliyokatwa vipande - 1 Ratili(LB)
Mchele Basmati - 2 Magi
Chumvi ya wali - kiasi
Kitungu kilichokatwa katwa - 1 kikubwa
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi - 1 kijiko cha supu
Mtindi (yogurt) - ยฝ kikombe
Mchanganyiko wa bizari ya pilau ya tayari - 2 vijiko vya supu
Mafuta kidogo yakukaangia
Rangi ya manjano (ukipenda)
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
Osha mchele na roweka nusu saa .
Weka mafuta katika sufuria na kaanga vitungu mpaka viwe rangi ya hudhurungi (brown).
Tia thomu na tangawizi na ukaange kidogo.
Kisha weka bizari ya pilau halafu nyama huku unakaanga hadi nyama isiwe nyekundu tena.
Tia maji gilasi 1ยฝ- 2 ichemke mpaka nyama iwive na karibu kukauka.
Mimina mtindi na iachie moto mdogo ikauke kidogo.
Kwenye sufuria nyingine chemsha mchele pamoja na chumvi na mafuta kidogo mpaka uive.
Mimina wali juu ya nyama, kisha nyunyiza rangi (ukipenda) kama vile wali wa biriani na ufunike kwa dakika kumi hivi.
Changanya wali na nyama pamoja ikiwa tayari kuliwa.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!