Mahitaji
Nyama (kata vipande vidogodogo) - Β½ kilo
Maharage - 3 vikombe
Mahindi - 2 vikombe
Kitunguu - 1
Nyanya - 2
Kabichi lililokatwa - 2 vikombe
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha chai
Vidonge vya supu - 2
Chumvi - kiasi
Mafuta -1au 2 vijiko vya chakula
Namna Yakutayarisha
Chemsha mahindi mpaka yawive na maji yakauke kiasi.
Chemsha maharage pembeni nayo mpaka yawive na maji yakaukie kiasi.
Tia mafuta kwenye sufuria anza kukaanga vitunguu , thomu na vidonge vya supu koroga kiasi.
Kisha mimina nyama iliyokatwa vipande acha ikaangike kidogo na chumvi.
Nyama ikishakaangika tia nyanya funika kwa moto mdogo mpaka nyama iwive.
Kisha mimina mahindi na maharage yaliyochemshwa na maji yake kiasi koroga mpaka ichanganyike na mwisho mimina kabichi funikia mpaka kabichi iwive onja chumvi kama imekolea
Halafu malizia kukoroga mpaka ichanganyike na ikaukie kisha pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa.







Discussion
Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.
You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.
Log in to participate