Mahitaji
Nyama Ya Mbuzi - 1 Kilo
Mchele - 4 Magi
Vitunguu - 3
Nyanya - 2
Nyanya kopo - 3 vijiko vya chai
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 2 vijiko vya supu
Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
Garam Masala (mchanganyiko wa bizari) - 2 vijiko vya supu
Hiliki - 1 kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Mafuta - ยฝ kikombe
Zaafarani au rangi za biriani za kijani na manjano/orenji
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Sosi Ya Nyama
Changanya nyama na thomu, pilipili, chumvi na nusu ya garam masala. Tia katika treya ya oveni uipike nyama (Bake) hadi iwive. Au iwivishe kwa kuichemsha.
Katika kisufuria kingine, tia mafuta (bakisha kidogo ya wali) kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi, kisha tia nyanya, nyanya kopo, bizari zote nyingine zilizobakia.
Namna Ya Kupika Wali
Mchele - 4 magi
Mdalasini - 1 kijiti
Hiliki - 3 chembe
Kidonge cha supu - 1
Chumvi
Osha na roweka mchele wa basmati.
Tia maji katika sufuria uweke jikoni. Tia kidonge cha supu, mdalasini, hiliki na chumvi .
Yakichemka maji tia mchele, funika upike hadi nusu kiini kisha uchuje kwa kumwaga maji.
Tia mafuta kidogo katika mchele na zaafarani iliyorowekwa au rangi za biriani kisha rudisha mchele katika sufuria ufunike na upike hadi uwive.
Pakua wali katika sahani kisha mwagia sosi ya nyama juu yake, pambia kwa kukatika nyanya, pilipili mboga na figili mwitu (Celery) au mboga yoyote upendayo.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!