Mahitaji
Mchele - 2 vikombe
Adesi -1 Β½ vikombe
Nazi ya unga - 1 Kikombe
Maji (inategemea mchele) - 3
Chumvi - Kiasi
Vipimo Vya Bamia:
Bamia - Β½ kilo
Vitunguu maji - 2 vya kiasi
Nyanya iliyosagwa - 1 kubwa
Nyanya ya kopo - 2 vijiko vya chai
Pilipili manga - Β½ kijiko cha chai
Mafuta - 3 vijiko vya chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
Wali wa adesi
Osha na roweka mchele na adesi .
Chuja nazi kwa vikombe 3 vya maji tia chumvi kisha weka jikoni.
Tui la nazi likishachemka tia mchele na adesi pamoja. Punguza moto, funika wali upikike kwa moto mdogo mpaka ukauke vizuri.
Bamia
Katakata bamia vipande vya kiasi/ Katakakata vitunguu weka kando.
Katika sufuria tia mafuta na kaanga vitunguu hadi viwe rangi ya hudhurungi.
Tia nyanya ilosagwa na nyanya ya kopo na pilipili manga na chumvi.
Kisha Tia bamia punguza moto mdogo mdogo mpaka ziwive.
Vipimo: Mchuzi Wa Kamba
Kamba - 1Lb
Vitunguu vilokatwa katwa - 2
Nyanya ilokatwa katwa - 2
Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 Kijiko cha chai
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 Kijiko cha chai
Bizari ya mchuzi (curry powder) - Β½ Kijiko cha chai
Haldi β bizari ya manajano - Β½ kijiko cha chai
Nyanya ya kopo - Β½ Kijiko cha chai
Ndimu - 1
Chumvi - Kiasi
Mafuta ya kukaangia - 2 Vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Kaanga vitunguu kidogo hadi vilainike,
Tia nyanya, thomu na piilipili mbichi. Endelea kukaanga, tia nyanya ya kopo, chumvi, bizari zote.
Tia tia kamba na huku unakoroga mpaka wabadilike rangi na kuwiva. Kamulia ndimu na mchuzi uko tayari.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!