Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Jamaa alikuwa anagombana na mkewe,hatimae
akamwambia kwa ukali
"Unajua nimechoka sasa, haya kusanya nguo
zako naβ¦β¦..
Kabla hajamalizia sentensi simu
ya mkewe ikaita, kumbe alikuwa ni baba yake.
Basi mzee akaanza kuongea na binti yake huku
jamaa anasikia
"Aisee mwanangu nimebahatika kuuza ile
nyumba yangu sasa nimeona niwatumie milioni
20 mjaribu kuanzisha mradi na mwenzio.
Haya mwambie yeye nitampigia kesho kama
ana mradi mwingine nimpe hela kidogo".Baada
ya simu kukatwa mke akamgeukia jamaa
akamuuliza,"eeenhee!!! ulikuwa unasema
umenichoka nikusanye nguo zangu halafu
iweje? Jamaa kwa upole akajibu "Nilikuwa
nasema ukusanye nguo zako na unipe nifue".