Maswali na Majibu kuhusu Rehema

✍️ DIN - Melkisedeck Leon ShineπŸ“… 2016-02-28 03:34:00πŸ’¬ 50 comments⏱️ ~2 min read
πŸ“„ PDF
Rehema ni nini?
Rehema ni msamaha au ondoleo la adhabu ya dhambi tulizostahili sababu ya dhambi zilizokwisha ondolewa

Rehema hutolewa na nani?
Rehema hutolewa na Kanisa Katoliki kwa kutugawia mastahili ya Yesu Kristo, Bikira Maria na Ya Watakatifu

Kuna Rehema za namna ngapi?
Rehema za namna mbili
1. Rehema kamili 2. Rehema pungufu (Rehema isiyo kamili)

Rehema kamili ni nini?
Rehema kamili ni msamaha wa kufutiwa adhabu zote za muda za dhambi

Rehema isiyo kamili (pungufu) ni nini?
Rehema isiyo kamili (pungufu) ni msamaha wa kupunguziwa adhabu ya dhambi

Adhabu za dhambi huondolewa kwa namna gani? Jinsi ya kupata rehema
Adhabu za dhambi huondolewa kwa; 1. Kufanya malipizi au majuto kamili 2. Kuvumilia taabu na mateso katika maisha 3. Kuvishinda vishawishi na majaribu
4. Kusali sala mbalimbali 5. Kuomba Misa kwa ajili hiyo. 6. Kusoma neno la Mungu na kulitafakari na kulinganisha na maisha yetu ya kila siku 7. Utakaso wa Toharani kama adhabu hizi hazikuondolewa duniani

Kipimo cha Rehema ni nini?
Kipimo cha Rehema hutegemea uzito wa majuto na mapendo mtu aliyonayo kwa Mungu Muumba wake. (1Kor 9:11)

Mtu akitaka kupata Rehema za Kanisa Katoliki yampasa nini?
Mtu akitaka kupata Rehema za Kanisa Katoliki yampasa; 1. Kujua na kufuata utaratibu unaotolewa na Kanisa Katoliki wa kupata Rehema 2. Awe katika hali ya neema ya Utakaso 3. Kufanya matendo yote yanayotakiwa kwa kupata rehema hiyo, kwa mfano;
a). Hija au Kuhiji katika mwaka wa Jubilei katika Kanisa lililo teuliwa na Askofu b). Kufanya mafungo - Kama vyama vya kitume c). Kuzuru makaburi (Kutembelea) yaliyobarikiwa d). Katika hatari ya kufa padri hutoa rehema pamoja na Sakramenti ya wagonjwa e). Kusali kwa nia za Baba Mtakatifu
πŸ’¬

Discussion

Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.

50 comment(s)
πŸ” Login required to comment or reply

You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.

Log in to participate
M
Miriam Mchome2016-11-10 11:20:05
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
G
Grace Wairimu2016-10-09 08:21:46
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
A
Agnes Njeri2016-06-22 07:16:47
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
C
Christopher Oloo2016-04-15 04:37:10
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
M
Mary Mrope2016-03-02 01:02:35
Mungu akubariki!
P
Paul Ndomba2016-02-20 19:22:52
Mwamini Bwana; anajua njia
P
Peter Tibaijuka2015-09-16 00:46:42
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
A
Anna Mchome2015-08-30 11:56:55
Kwa Mungu, yote yanawezekana
I
Isaac Kiptoo2015-07-26 00:51:49
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
L
Linda Karimi2015-07-18 01:41:12
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu