Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ

Jifunze kupitia mfano huu Ili uishi kwa amani na watu

โ€ข
Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image

Siku moja nilichukua taxi aina ya UBER nikiwa naelekea uwanja wa Ndege Mwl. Nyerere Dereva huku akiendesha kwa ustaarabu sana mara ghafla pasipo kutegemea gari ya taka ikajitokeza mbele yetu kutokea nje ya barabara. Dereva wa taxi kwa umakini na neema ya Mungu akalikwepa gari hilo na ilikuwa kidogo agonge gari zingine mbele yetu.

Pasipo kutegemea dereva wa gari la taka akaanza kufoka na kutoa matusi kwa kelele kubwa!

Katika hali ya kushangaza dereva wa taxi alitabasamu na kuwapungia mkono waliokuwa kwenye gari la taka na ndipo kwa mshangao nilimuuliza; "Inakuwaje ufanye hivyo wakati walitaka kutuua na hata kuharibu mali yako?"

Akajibu kwa upole akinitazama kwa tabasamu akasema. โ€œKatika maisha yetu, kuna watu wako kama gari la taka. Wamejaa misongo, hasira, maumivu, wamechoka kifikra, kiuchumi na kimaisha, na wamejaa masikitiko mengi. Watu hao takataka zao zinazopowazidi hutafuta mahali pa kuzitupa na haijalishi mazingira wanakozitupia.

FUNZO!
Jifunze kutogombana nao. Wapungie mkono, wape tabasamu, songa mbele. Haikupunguzii kitu. Wala usiruhusu takataka zao zikupate."

Uliumbwa kuyafurahia maisha. Usiyafupishe kwa kuamka asubuhi na kinyongo, na hasira, na ghadhabu kwa sababu ya mtu fulani.

Watafiti wanasema 10% ya maisha ni vile ulivyoyatengeneza lakini 90% ya maisha ni vile unavyochukuliana nayo.

Jifunze kuchukuliana na maisha kuliko vile unavyoyatengeneza huku ukimtegemea Mungu.

ANGALIZO!
Ukiona umeanza kueleweka, kukubalika, kutambulika, kufahamika, kuheshimika na kupata nafasi zaidi kwa kile unachokifanya kumbuka kuendelea kuzingatia misingi, nguzo, miiko na nidhamu iliyokuwezesha kufika hapo ulipo ili uende mbali zaidi.

MUNGU AKUBARIKI SANA.

AckySHINE Solutions
โœจ Join AckySHINE for more features! โœจ

Comments 0

Please log in or register to comment or reply.
No comments yet. Be the first to share your thoughts! ๐Ÿ“

๐Ÿ”— Related Posts

๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About