
Kinga ya magonjwa na madhara yote
Katika maisha, kinga kuu ya magonjwa na majanga yote ni kujikatalia au kujinyima.
Browse published Articles by category, tag or language. Random discovery is the default and keeps a stable order while you move through pages.

Katika maisha, kinga kuu ya magonjwa na majanga yote ni kujikatalia au kujinyima.

Kama vile moto unavyozimwa na maji ndivyo vivyo hivyo hasira inamalizwa na maneno ya upole.

Amini kuwa unashinda na wewe utashinda. Hata vita wanashinda wale wanaoamini katika ushindi. Kutokujiamini ni sawa na kushindwa tayari.

Kila mtu ni mrithi wake yeye mwenyewe. Mafanikio yako ya baadae ni urithi wako ulioutengeneza hapo awali. Utajiri wako wa sasa unatokana na uliyoyawekeza miaka β¦

Huwezi kuona thamani ya kitu ambacho hujakigharamia. Faida haina thamani kama haijagharamiwa.

Hakuna uwezo bila fursa. Huwezi kusema unauwezo wa kitu kama hauna fursa ya kukifanya.

Uzuri wa kitu huvutia MACHO lakini ubora wa kitu huuteka MOYO daima. Uzuri haudumu.

Changamoto na ugumu wa jambo upo kwa wale wanaolifanya. Huwezi kukaa na kutazama jambo bila kulifanya na kisha kujua changamoto zake.

Matendo ya mtu ni tafsiri kuu ya mawazo yake.

Maisha ya ujana ni kufanya mema au mabaya, kushinda au kushindwa. Uzee ni sherehe au majuto ya ujana.

Vile unavyotoa ndivyo unavyopokea. Yule anayetoa sana ndiye ansyepokea sana. Kutoa ni kuhifadhi.

Kuacha kitu chochote kabisa moja kwa moja ni rahisi sana kuliko kufanya kitu hicho kidogokidogo kwa wastani. Usijidanganye utafanya kidogo au utaacha kidogo. Acβ¦

Kujaribu kufanya jambo kubwa la kipekee ni kushinda hata kama halijafanikiwa.

Tunatakiwa tujenge uhodari na uwezo utakaotusaidia kutumia fursa zilizo wazi mbele yetu.

Ukitaka kufanya biashara kwa ufanisi; wakati wa kununua nunua ukiwa na mtazamo wa muuzaji kwa kufikiri kama wewe ungekua ndio unauza ungeuzaje, na Wakati wa kuuβ¦

Jarbu Mambo mengi kadiri uwezavyo kwani kwa kujaribu ndivyo tunajua tunaweza au hatuwezi. Kamwe usiseme huwezi jambo kabla ya kujaribu.

Kukosa mtu, kitu au jambo fulani kunasababila Moyo kujenga upendo kwenye mtu, kitu au jambo ulilolikosa.

Usimpe mtu ushauri ambao unahisi ataukubali sana, mpe mtu ushauri wenye manufaa kwake japo ni mgumu kuukubali.

Inapendeza kweli mke na Mume kusaidiana. Kusaidiana ni Kushirikiana lakini kugawana majukumu ni kupeana mzigo

Tofauti ya maskini, tajiri na mwenye uchu/tamaa ni kwamba; Mtu maskini anafanyakazi ili apate chochote, tajiri anafanya kazi apate vitu vingi lakini mwenye uchuβ¦

Siri kuu ya kuishinda hasira yako ni kusubiri kabla ya kutenda unapokuwa na hasira.

Huwezi kupata maendeleo kwa kusitasita na kuogopaogopa. Hata kobe anayesonga mbele ni yule anayetoa kichwa chake kwenye gamba/nyumba yake.

Unapokosa kitu ukipendacho kwa muda mfupi kinapungua thamani, ukikikosa kwa muda mrefu thamani yake yote hupotea.

Tunatakiwa tujithaminishe wenyewe kwa yale tunayoona tunauwezo wa kuyafanya japokuwa watu wengine wanatuthamanisha kwa yale wanayoyaona tumeshayafanya