Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Duh! Angalia alichokula huyu mwizi! Wizi mwingine bwana!
Updated at: 2024-05-25 17:57:04 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Baada ya mwizi kuvunja mlango huko Tarime, akaingia kwenye stoo akaona vinyama kwenye bakuli vikiwa vimekauka. Akaonja 1 akaona kitamu na kina chumvi! Akavila vyote. Alipomaliza akaangalia juu ya mlango akaona pameandikwa; "chumba cha UKEKETAJI WANAWAKE". Unafikiri atakuwa amekula nini?
Madhara ya kubeba nauli kamili tuu. Cheki kilichonipata
Updated at: 2024-05-25 17:49:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kubeba nauli kamili nayo ni shida Yani nimepanda daladala Kondakta mmoja akaingia kwenye Gari amevaa suti za blue za daladala na miwani Kisha akakusanya pesa Gari Zima alafu akakaa siti ya nyuma baade Kondakta mwingine akaanza kukusanya pesa watu wakalalamika na kusema tayari tumelipa na kumuonyesha tuliemlipa Kondakta akacheka na kusema huyo tuliemlipa ni kipofu na alikuwa anaomba msaada..!!
Dokta: Mama tumemchunguza mumeo kwa makini sana, jopo lote la madaktari tumekubaliana mumeo anahitaji mapumziko japo ya mwezi. Sasa tafadhali chukua hivi vidonge vya usingizi vitasaidia sana.
Updated at: 2024-05-25 18:04:24 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Dokta: Mama tumemchunguza mumeo kwa makini sana, jopo lote la madaktari tumekubaliana mumeo anahitaji mapumziko japo ya mwezi. Sasa tafadhali chukua hivi vidonge vya usingizi vitasaidia sana.
Mama: Asanteni sana, sasa niwe nampa mara ngapi?
Dokta: Unatakiwa wewe uwe unakunywa vidonge hivi kutwa mara tatu kwa mwezi mzima, mumeo atapona.
Updated at: 2024-05-25 18:00:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa fulani alikuwa ame2lia beach mzungu akapita akamuliza "Are u relax ? Jamaa akawa hamuelewi akamjibu No! Mzungu mwengine akapita akamuliza vilevile akajibu No!
Akaona hapa anasumbuliwa akasogea mbele kidogo ya maji akamuona mzungu mmoja alikuwa ame2lia. Akamuliza "are u relax? Mzungu akajibu yes jamaa akamkata makofi mawili na kumwambia kumbe we ndo relax inuka unatafutwa na wenzako…..Shenz mkubwa mie nasumbuliwa na wenzako kule we umejikausha!!
Updated at: 2023-04-29 22:53:40 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Ladha ya bia ya 1 hadi ya 6..
Kwa wanywaji wazuri wa bia,
chupa ya kwanza 🍺 huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza koo… Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.
chupa ya pili 🍺🍺 kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihi….
Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wachezaji wa Yanga bila kukosea.. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.
Bia ya tatu 🍺🍺🍺 huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sana…. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokeza…..
Bia ya nne 🍺🍺🍺🍺 huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikia….. bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.
Bia ya tano 🍺🍺🍺🍺🍺 ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipu……na kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; ‘Mi sipendwi mpaka leo sijaolewa’ au ‘ Mume wangu sijui yukoje hanijali’
Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.
Kuanzia bia ya sita 🍺🍺🍺🍺🍺🍺 na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana. ……. …Kuna watu husema ukilewa ndipo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamueleza ukweli jinsi alivyo fala na hajui kuendesha kampuni.
Au unasema ukweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Kimsingi uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao pia uchumba unaweza kuvunjika…….
Dereva alikamatwa kwa kosa la kusababisha ajari ya watu wa5 aliowagonga. Trafik akamuliza kwanin umewagonga awa watu? Jamaa akajibu,"nilikua mwendo wa kasi sana, alafu nimejaza abiria ndani, gari likawa linakuja mbele yangu nilipokanyaga breki zikakatika, sasa ningefanya nin?"
Updated at: 2024-05-25 18:03:22 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Dereva alikamatwa kwa kosa la kusababisha ajari ya watu wa5 aliowagonga. Trafik akamuliza kwanin umewagonga awa watu? Jamaa akajibu,"nilikua mwendo wa kasi sana, alafu nimejaza abiria ndani, gari likawa linakuja mbele yangu nilipokanyaga breki zikakatika, sasa ningefanya nin?" Trafki akamwmbia, kwanin ucngeenda upande ambao una watu wachache ili uokoe wengi? Jamaa akajibu, "nilifanya hivo, huku kushoto alikua m1 na kulia walkua wa4, nikamfuata uyu wa kushoto et akakambilia upande wakulia akazani cjamwona, nikamfata huko huko alipoenda, nikampa kitu mbwa yule"
Eti kwa nini Watu hawapostigi hii? Hata selfie sijaonaga
Updated at: 2024-05-25 16:59:02 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vijana mkiwa mnaendesha magari mna post mukiwa mpo beach mna post mkiwa kwenye masherehe mna post Lakin mkiwa mmeenda kwa mganga siwaoni kupost mitunguli na vibuyu vya mganga unakuwa je wa zee tena. 😀😀😀😀