Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 17:50:05 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
If… 99 is: Ninety nine, 88 is: Eighty eight, 77 is: Seventy seven, 66 is: Sixty six, 55 is: Fifty five, 44 is: Forty four, 33 is: Thirty three, 22 is: Twenty two, Why 11 not Onety one?
Updated at: 2024-05-25 16:53:49 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ndoto zingine bwana usiombe zikupate
Mimi usiku wa kuamkia Leo nikiwa nimelala nimeota naendesha gari Yangu aina ya BMW mpya Mara gafla ikakwama kwenye tope .hivyo ikabidi nishuke ili kuisukuma loh! Yani kudadeki ile kuamka nikakuta nimesukuma kitanda hadi sebleni Daaa ilinisikitisha sana jiangalie sana sese hivi ndio narudisha kitanda chumbani .angalizo angalia ndoto unazo ota unaweza kuota upo baharini ukaamka unajikukuta unaogelea kwenye Jaba la Maji shauri yako.
Kilichompata huyu anayependa kusoma SMS za watu kwenye daladala
Updated at: 2024-05-25 17:01:56 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jana nilipanda daladala nikapata seat nikaketi, nikawa nimejiachia ninachati kwenye simu yangu(Smart phone), kukawa na jamaa kasimama pembeni yangu, ye hakupata seat. Sasa akawa anasoma message zangu bila aibu yani anafutilia ninavyochati…
Basi nikasema ngoja nimtie Adabu mshenzi huyu…. Nikacheck saa yangu yamkononi kisha nikatext: "Oya Ben Kwaheri bwana, zimebaki sekunde 30 tu hili bomu💣 lilipuke… najua hatutaonana tena, nitunzie Familia yangu, wambie nawapenda sana…" Yule jamaa akajirusha dirishani……😂😅
Updated at: 2024-05-25 17:08:18 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Sitasahau mwaka ule ambapo nilipeleka barua ya maombi yangu ya kazi kwenye kampuni moja maarufu. Wakati nasubiri majibu siku moja nikaenda kwa mama ntilie kununua maandazi akanifungia vizuri, kufika nyumbani hamu yote ya maandazi iliniishia pale nilipogundua karatasi iliyofungiwa maandazi ni barua yangu ya kuombea kazi😂😂
Huyu bwana leo kapatikana, Jamani nyodo nyingine mbaya
Baada ya kumaliza Degree yake ya sheria Bwana Rwegashora aliamua kurudi nyumbani Bukoba mjini na kufungua ofisi yake kwa ajili ya huduma kwa wateja.
Siku moja akiwa ndani ya ofisi yake alimuona mtanashati na mdada mmoja mrembo anakuja ofisini kwake akajua ni mteja anamletea kesi.
Ndipo akanyanyua mkoni wa wa simu ya TTCL na kuanza kuongea huku anajizunguusha kwenye kiti cha kuzunguuka.
Updated at: 2023-04-29 22:52:17 (3 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Baada ya kumaliza Degree yake ya sheria Bwana Rwegashora aliamua kurudi nyumbani Bukoba mjini na kufungua ofisi yake kwa ajili ya huduma kwa wateja. Siku moja akiwa ndani ya ofisi yake alimuona mtanashati na mdada mmoja mrembo anakuja ofisini kwake akajua ni mteja anamletea kesi.
Ndipo akanyanyua mkoni wa wa simu ya TTCL na kuanza kuongea huku anajizunguusha kwenye kiti cha kuzunguuka. Wakati mdada alipokaribia Rwegashora alimkaribisha kwa ishara maana alijifanya yupo busy na kuongea na simu ya umuhimu. Wakati anaongea na simu akisikika akisema No, No, No….. Absolutely No. Wajuulishe hao lay person wa New York kua siwezi kushuhulika na kesi ambayo itanilipa chini ya 50 million. Mimi ni profesional lawyer and im crossing the border to sarve international community.
Aka pose kidogo na akanywa maji kisha akaendelea….. Naweza kuanza kukusanya primary evidence next weak but tell them watume kwanza ten million kwa kuanza… Hahahahaha you dont know my Account Mr Roger. Ok waambie watume kwenye Account ileile walionitumia million 100 last month…
Aka pose tena akameza fundo la maji na kurekebisha tai yake kisha akaendelea… Ok usisahau kumueleza muendesha mashtaka mkuu wa marekani kua nitakuja New York mwezi ujao maana nitapita kwanza Amsterdam kuwasilisha utetezi wa yule mteja wangu mholanzi kisha nitaenda Tokyo kulipia ile gari yangu niloagiza.
Wakati anaongea hayo yote yule mdada alikua ametulia na anamuangalia Bwana Rwegashora anavyojizunguusha kwenye kiti chake huku akiongea kwa tambo kwenye ile simu ya TTCL. Baada ya kumaliza kuongea na simu Bwana Rwegashora aliweka mkono wa simu yake ya TTCL chini kisha akamgeukia mdada mrembo.
Samahan sana kwa kukupotezea muda wako unajua tena kazi zetu zinaumiza kichwa sana kama unavyoona mwenyewe yaani niko busy sana ninapokea simu sana mpaka nimechoka na simu nyingi ni za wateja wa njee ya nchi.
Anyway nikusaidie nn? Mdada akajibu mimi ni mfanyakazi wa kampuni ya TTCL nimekuja kuunganisha line yako ya simu kwani haipo hewani tangu wiki iliyopita…!!!