Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰

Ziara za kushtukiza zinachekesha sana

β€’
Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image

Mimi Nimecheka sana
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

ZIARA ZA KUSHTUKIZAπŸ˜€πŸ˜€
Mimi ni msomaji mzuri wa magazeti, na msikilizaji mzuri wa redio, huwa naangalia luninga mara chache sana kama nikibahatika kupita mahala kuna luninga. Sasa wiki hii nimesikia mengi kuhusu hizi ziara za kushtukiza za viongozi wetu, nikaona hili ni jambo zuri tena linafaa kuigwa na sisi wananchi wapenda maendeleo. Nikaona nijipange na mimi nifanye ziara kadhaa za kushtukiza katika sehemu mbalimbali zinazonihusu.

Nikaona nianze na ziara ya kushtukiza pale shuleni kwa huyu mwanangu, maana kila siku anakunywa chai na kuondoka na daftari zake na mie sijawahi kwenda shuleni kwao toka nilipomuandikisha shule mwezi Januari. Nilifika shuleni na kumuona mwalimu mkuu, ambae alianza kutetemeka nilipomuambia kuwa nimekuja pale kwa ziara ya kustukiza, sijui alidhani mi ni mmoja wa Mawaziri wapya, maana nilimuona jasho linamtiririka ghafla. Akanikaribisha ofisi yake iliyokuwa na vitabu kila kona, na kuita waalimu wote na kunitambulisha kuwa ni kiongozi nimekuja kwenye ziara ya kustukiza.

Nilipojitambulisha kuwa ni mzazi, waalimu wote nikawaona waanza kupumua kwa raha. Nikawaambia kuwa mimi nina mwanafunzi pale na nilikuja ziara ya kustukiza kujua maendeleo yake. Baada ya mwalimu mkuu kusaka jina la mwanangu nae akanambia, β€œMzee huyu mtoto hajaja shule mwezi wa tatu sasa, tulijaribu kukutafuta ikashindikana, hatujui yu wapi” Jasho likaanza kunitoka mimi, yule mtoto kila asubuhi nampa nauli anaenda shule, na mara nyingi ananiomba michango kumbe hata shule haji. Niliondoka bila kuaga presha ikiwa juu.

Nikaona niende kwenye genge la mke wangu nae nikamfanyie ziara ya ghafla nimhadithie mambo ya mwanae, nilipofika pale nikakuta kuna mdada mwingine anauza genge. Nikamsalimu, na kumuuliza mwenye genge ntampataje, jibu lake lingeniua kama ningekuwa si mkakamavu, β€œMume wake kaja kumchukua na gari wameenda kununua shamba Bagamoyo”. Nikaondoka nimechanganyikiwa, nikajuwa hapa dawa yangu moja tu, nayo ni Sabrina, mtoto wa Kinyaturu pale ambapo nikipata maudhi huwa naenda kubembelezwa.

Nikatwanga mguu kwa Sabrina nae nikamfanyie ziara ya ghafla ili anipoze moyo. Nilipogonga mlango wa chumba chake akatoka mbaba wa miraba minne, akanisalimia kwa upole, β€œSalama kaka unasemaje?” Jibu likanitoka β€œSamahani mie nilimkopesha huyu dada wa chumba hiki vitenge, nilikuja kuuliza kama ameshapata hela yangu” Ziara za kushtukiza zinataka moyo wa chuma jamani

AckySHINE Solutions
✨ Join AckySHINE for more features! ✨

Comments 236

Please log in or register to comment or reply.
πŸ‘₯ Grace Mushi Guest Jun 4, 2024
🀣 Hiyo twist mwishoni, ingawa!
πŸ‘₯ Jamila Guest Jun 3, 2024
πŸ˜‚ Siwezi kuacha kucheka!
πŸ‘₯ Kiza Guest May 25, 2024
Nilikuwa na siku mbaya hadi niliposoma hii! πŸ˜…
πŸ‘₯ Catherine Naliaka Guest May 14, 2024
Umesema kweli! πŸ‘ŒπŸ˜‚
πŸ‘₯ Sarah Mbise Guest May 10, 2024
Hii kichekesho imebadilisha kabisa hali yangu! πŸ˜ƒ
πŸ‘₯ Esther Nyambura Guest May 1, 2024
πŸ˜„ Kali sana!
πŸ‘₯ Nyota Guest Apr 26, 2024
πŸ˜‚ Hii ni ya kuhifadhi!
πŸ‘₯ Rose Kiwanga Guest Apr 19, 2024
Kweli mna ucheshi wa kipekee sana! πŸ˜„πŸ˜‚
πŸ‘₯ Salima Guest Apr 12, 2024
Lazima niihifadhi hii, ni kichekesho kali sana! πŸ˜†
πŸ‘₯ Khatib Guest Apr 3, 2024
πŸ˜„ Umenishika vizuri!
πŸ‘₯ Chris Okello Guest Mar 24, 2024
πŸ˜‚ Kali sana!
πŸ‘₯ Victor Kamau Guest Mar 10, 2024
Ucheshi wenu ni wa hali ya juu! πŸ‘πŸ€£
πŸ‘₯ Zakaria Guest Mar 3, 2024
🀣 Ninashiriki hii sasa hivi!
πŸ‘₯ Faith Kariuki Guest Jan 15, 2024
Hii imenifurahisha hadi nacheka kwa sauti! πŸ€£πŸ˜‚
πŸ‘₯ Alice Mrema Guest Dec 28, 2023
πŸ˜‚πŸ‘Œ
πŸ‘₯ Rose Amukowa Guest Dec 26, 2023
Haha, hii ni kicheko bora zaidi nilichopata wiki hii! 😁
πŸ‘₯ Victor Kimario Guest Dec 20, 2023
Nimecheka hadi nina furaha sana! πŸ˜ŠπŸ˜‚
πŸ‘₯ Francis Njeru Guest Dec 20, 2023
Hii imenipa kicheko cha siku! πŸ˜‚πŸ€£
πŸ‘₯ Lydia Mahiga Guest Dec 2, 2023
πŸ€£πŸ‘πŸ‘Œ
πŸ‘₯ Mary Sokoine Guest Nov 7, 2023
πŸ˜† Ninakufa hapa!
πŸ‘₯ Ann Awino Guest Oct 17, 2023
Hii imenikuna sana! πŸ˜†πŸ˜…
πŸ‘₯ Faiza Guest Aug 20, 2023
Hii ni aina ya kichekesho usichosahau! πŸ˜‚
πŸ‘₯ Alex Nakitare Guest Jul 9, 2023
🀣 Ninashiriki hii na kila mtu!
πŸ‘₯ Jane Muthoni Guest Jul 4, 2023
Hii ni ya kufurahisha sana! πŸ˜ŠπŸ˜„
πŸ‘₯ David Sokoine Guest Jun 28, 2023
😁 Imeongezwa kwenye vipendwa!
πŸ‘₯ Jacob Kiplangat Guest Jun 22, 2023
Napenda vile mnaweka jokes kila siku! πŸ˜†πŸ‘
πŸ‘₯ Samson Tibaijuka Guest Jun 21, 2023
πŸ˜ŠπŸ˜‚πŸ€£
πŸ‘₯ Lucy Mushi Guest Jun 21, 2023
πŸ˜† Ninaihifadhi kwa baadaye!
πŸ‘₯ Nancy Komba Guest Jun 8, 2023
πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜†πŸ˜…
πŸ‘₯ Charles Mchome Guest Jun 3, 2023
πŸ˜†πŸ‘πŸ˜‚πŸ˜„
πŸ‘₯ Maneno Guest Jun 3, 2023
🀣 Ujuzi wa hali ya juu!
πŸ‘₯ Henry Sokoine Guest Apr 16, 2023
πŸ˜ŠπŸ˜‚πŸ˜…πŸ‘
πŸ‘₯ Grace Majaliwa Guest Apr 10, 2023
πŸ˜‚πŸ‘πŸ˜…πŸ€£
πŸ‘₯ Charles Wafula Guest Mar 20, 2023
πŸ‘πŸ€£πŸ˜†πŸ˜‚
πŸ‘₯ Alice Mwikali Guest Feb 19, 2023
Nimecheka hadi nimesahau shida zangu! πŸ˜…πŸ˜Š
πŸ‘₯ Edith Cherotich Guest Feb 17, 2023
Hii imenibamba sana! πŸ˜‚πŸ˜…
πŸ‘₯ Benjamin Masanja Guest Feb 10, 2023
Hii imenifurahisha sana! 🀣😊
πŸ‘₯ Jane Muthoni Guest Feb 7, 2023
πŸ˜‚ Siwezi kusubiri kushiriki hii!
πŸ‘₯ Khatib Guest Jan 21, 2023
πŸ˜… Bado nacheka!
πŸ‘₯ Rose Amukowa Guest Dec 28, 2022
Kweli mna ucheshi! πŸ˜‚πŸ€£
πŸ‘₯ David Chacha Guest Dec 28, 2022
Ucheshi wenu unanifurahisha sana! πŸ˜‚πŸ‘
πŸ‘₯ Charles Mrope Guest Dec 24, 2022
Kweli mna ucheshi wa hali ya juu! πŸ˜‚πŸ€£
πŸ‘₯ Zawadi Guest Dec 22, 2022
🀣 Hii imenigonga vizuri!
πŸ‘₯ Sultan Guest Dec 18, 2022
πŸ˜† Kali sana!
πŸ‘₯ Grace Mushi Guest Dec 17, 2022
Nimecheka hadi nimesahau shida zangu! πŸ˜‚πŸ˜…
πŸ‘₯ Peter Mwambui Guest Nov 26, 2022
Hii kichekesho ni ya kuhifadhi bila shaka! 😁
πŸ‘₯ Alex Nakitare Guest Nov 14, 2022
🀣πŸ”₯😊
πŸ‘₯ Josephine Nekesa Guest Nov 4, 2022
Ucheshi wa hali ya juu! πŸ˜‚πŸ‘
πŸ‘₯ Mary Kidata Guest Sep 30, 2022
Nimecheka hadi nina furaha sana! πŸ˜†πŸ˜‚
πŸ‘₯ Mariam Guest Aug 7, 2022
Ninashiriki hii na marafiki zangu mara moja! πŸ˜†
πŸ‘₯ Brian Karanja Guest Jul 14, 2022
πŸ˜… Ilibidi nishiriki hii na kila mtu!
πŸ‘₯ Lucy Wangui Guest Jun 18, 2022
Hii imenikuna hadi nina furaha! πŸ˜ŠπŸ˜‚
πŸ‘₯ Patrick Akech Guest Jun 17, 2022
πŸ˜† Bado nacheka!
πŸ‘₯ Mohamed Guest May 28, 2022
πŸ˜… Nilihitaji hii!
πŸ‘₯ Rose Lowassa Guest May 2, 2022
Lazima nikumbuke hii kwa baadaye! πŸ˜†
πŸ‘₯ Anna Sumari Guest Apr 18, 2022
Napenda jokes zenu! πŸ˜ŠπŸ˜…
πŸ‘₯ Victor Malima Guest Apr 12, 2022
Hii joke imenikumbusha enzi zile! πŸ˜ŠπŸ˜‚
πŸ‘₯ Daniel Obura Guest Apr 9, 2022
πŸ˜† Hiyo punchline ilikuwa kali!
πŸ‘₯ John Mushi Guest Mar 27, 2022
Nimecheka hadi nimesahau shida zangu! πŸ˜ŠπŸ˜…
πŸ‘₯ David Ochieng Guest Mar 22, 2022
Ucheshi wenu unanifurahisha kila siku! πŸ˜ŠπŸ˜‚

πŸ”— Related Posts

🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About