Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Piga piga mayai vizuri kwenye bakuli na weka chumvi kidogo kisha weka kikaango kwenye moto na mafuta kidogo.
Kikisha pata moto miminia mchanganyiko wa mayai na uanze kukorogo pale tu unapomiminia, endelea kukoroga hadi uone yanakuwa magumu na kuanza kuiva. Pika kwa kiwango unachopendelea na kusha epua na weka kwenye sahani.
Weka mafuta kijiko kimoja kwenye kikaango na kisha weka soseji zako na uzipike kiasi pande zote kisha epua na weka pembeni.
Weka slesi za mikate kwenye toster na zikiwa tayari unaweza weka siagi ili kuongeza ladha na mvuto. Andaa mlo wako pamoja na juice, maziwa au chai.
Updated at: 2024-05-25 10:34:46 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
1 kilo unga wa ngano 240 ml maji ya vugu vugu 2 olive oil kijiko kikubwa cha chakula 2 asali kijiko kidogo cha chai 1 chumvi kijiko kidogo cha chai 1 hamira ya chenga kijiko kidogo cha chai
JINSI YA KUPIKA
Chukua bakuli weka maji ya uvugu vugu, amira ya chenga, asali na chumvi kisha koroga ichanganyike vizuri acha itulie kwa dakika 10. Kisha chukua olive oil na unga wa ngao mimina kidogo kidogo changanya mpaka ichanganyike safi kabisa kisha anza kukanda kama mchanganyiko wa chapati au maandazi. Baada ya mchanganyiko wako kua mgumu safi kabisa funika bakuli lako na mfuko wa plastiki au cling film kwa muda wa saa 1 katika joto la chumba na mchanganyiko wako utaumuka baada ya muda huo. kisha ukandamize mchanganyiko huo wa unga na kua flati kama mwanzo. Kata mafungu matano hadi saba ya ujazo sawa inategemea na ukubwa wa piza unaopenda we mlaji kisha sukuma umbo la duara. Tengeneza mchuzi mzito wa nyanya kisha weka juu ya kitako cha piza na kuitandaza vizuri kwenye pizza yako kama unavyopaka siagi kwenye mkate. Usisahau kuweka chumvi na sukari kidogo katika mchuzi wa nyanya ili kukata uchachu. Katakata nyanya, kitunguu, pili pili hoho, na bilinganya na kuziweka juu ya pizza yako kwa mpangilio ukitanguliza biringanya, ikifuatiwa na pili pili hoho, kitunguu maji na nyanya. Kisha chukua mozarella cheese ikwaruze katika mkato mdogo rahisi kuyeyuka kwa kutumia kwaruzo la karoti linafaa. kisha chukua mkwaruzo wa mozarella cheese na unyunyizie juu ya hizo mboga. Weka pizza yako kwenye sahani ya bati au pizza pan ili isaidie kuiva upande wa chini. Weka pizza yako kwenye oven ambayo imeshawashwa na ina joto 400 - 450 F. Choma kwa dakika 20 hadi 25 iwe kaukau na rangi ya kahawia pia cheese itakua imyeyuka na kusambaa vizuri juu ya pizaa.
NB: Unaweza weka mchanganyiko wa nyama yeyote ile kama salami, nyama ya ngombe, nyama ya kuku au samaki kwa kufata maelekezo sawa sawa na hii piza ya mboga, tofauti yake itakua huweki mboga unaweka nyama.
Updated at: 2024-05-25 10:34:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Chenga za biskuti - 3 gilasi
Mtindi (yogurt) - 1 Kopo (750g)
Maziwa ya unga - 1 gilasi
Siagi - 10 Vijiko vya supu
Sukari - ½ gilasi
Lozi zilizomenywa vipande vipande - ½ gilasi
Nazi iliyokunwa - ½ gilasi
Vanilla - 1 Kijiko cha supu
MAPISHI
Katika mashine ya kusagia (blender), tia mtindi, sukari, siagi na vanilla na usage pamoja hadi ichanganyike. Mimina katika bakuli la kiasi. Tia vitu vilivyobakia na uchanganye vizuri. Mimina kwenye treya ya kuchomea na uvumbike katika oveni moto wa 350° hadi ishikamane na kuwa tayari. Iaache ipoe kisha katakata vipande na tayari kwa kuliwa.
Baada yakuwa imeshaiva, ukipenda unaweza kupakiza jamu au karameli ya tayari kwa juu, kisha ukarudisha kwenye oveni moto wa juu kidogo kwa ladha nzuri zaidi
Jinsi ya kutengeneza Slesi Za Chokoleti Na Karameli
Updated at: 2024-05-25 10:34:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga - 1 Magi (vikombe vya chai)
Sukari ya browni - ½ Magi
Siagi iliyoyayushwa - 125 g
Nazi iliyokunwa - ½ Magi
MJAZO WA KARMEL (Caramel filling)
Syrup - 1/3 kikombe cha chai
Siagi iliyoyayushwa - 125 g
Maziwa matamu ya mgando - 2 vikopo (condensed milk)
MJAZO WA CHOKOLETI (Chocolate filling)
Chokoleti - 185 g (dark chocolate)
Mafuta - 3 Vijiko vya chai
MAANDALIZI
Changanya unga, sukari, siagi na nazi iliyokunwa kwenye bakuli mpaka unga ushikamane. Paka mafuta treya ya kuchomea kisha utandaze kwenye treya ya 20cm kwa 30 cm au (8 in kwa 12 in) unaweza kuweka karatasi ya kuchomea chini ukipenda. Choma kwenye moto 325˚C kwa muda wa dakika 15 mpaka 18 au mpaka ibadilike kuwa rangi ya browni. Kwenye sufuria ndogo tia syrup siagi na maziwa matamu ya mgando na changanya kwa moto mdogo mpaka uwe mzito kasha mimina juu ya keki uliyochoma na choma tena kwa muda wa dakika 20 mpaka karameli iwe rangi ya dhahabu. Kwenye sufuria ndogo nyingine tia vipande vya chokoleti na mafuta na ukoroge kwa moto mdogo mpaka iyayuke kisha wacha ipoe kidogo mimina juu ya mjazo wa karameli kisha weka kwenye friji mpaka ishikamane. Kata vipande weka kwenye sahani tiyari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:23:06 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga wa ngano - magi 2 (vikombe vikubwa)
Hamira kijiko 1 cha chai
Sukari Vijiko 2 vya supu
Maziwa ¾ Magi
Siagi Vijiko 2 vya supu
Mafuta ya kukaangia kiasi
VIAMBAUPISHI:SHIRA
Sukari ¾ Kikombe
Maji ¾ Kikombe
Illiki ya unga kiasi
Zafarani kiasi
JINSI YA KUPIKA
Katika bakuli, changanya vipimo vyote pamoja na ukande unga usiwe mgumu wala laini sana uwe kiasi. Kisha fanya donge moja na iache pahali penye joto mpaka iimuke. Halafu weka mafuta ya kukaangia kwenye moto. Sukuma donge hadi liwe duara sio nyembamba sana, kisha katakata kama maandazi. Mafuta ya kisha pata moto choma mittai hukuunazigeuza hadi ziwive na kugeuka rangi. Katika sufuria tia vipimo vya shira na iache ichemke isiwe nzito sana. Mimina mitai kwenye shira na uzipepete, kisha weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:04 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa dengu (gram flour 1/4 kilo) Kitunguu kilichokatwa (onion 2) Hoho (green pepper 1/2) Pilipili iliokatwakatwa (scotch bonnet pepper 1/2) Barking powder (1/4 ya kijiko cha chai) Chumvi (salt) Kitunguu swaum (garlic cloves 2) Mafuta ya kukaangia (vegetable oil) Binzari manjano (turmeric 1/4 ya kijiko cha chai)
Matayarisho
Changanya unga, chumvi, binzari, barking powder kwanza kisha weka maji kiasi na vitu vyote vilivyobakia (isipokuwa mafuta) na ukoroge vizuri kuhakikisha unga hauna madonge.Hakikisha unga hauwi mzito wala mwepesi sana. Kisha uache kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo choma bagia katika mafuta. Ukiwa unachoma hakikisha bagia zinakuja juu ya mafuta na hazigandi chini. Ikitokea zinaganda chini hapo itakuwa umekosea kitu. Pika mpaka ziwe za light brown kisha zitowe na uziweke katika kitchen towel ili zikauke mafuta na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mihogo kilo 1 Kidali cha kuku 1 kikubwa Nyanya 1 kubwa Kitunguu maji 1 cha wastani Swaum/tangawizi i kijiko cha chai Nazi kopo 1 curry powder 1 kijiko cha chai Binzari manjano 1/2 kijiko cha chai Limao 1/2 Pilipili 1 Chumvi kiasi
Matayarisho
Saga pamoja nyanya, kitunguu na swaum/ginger pamoja na vimaji kidogo. Kisha vitie kwenye sufuria isiyoshika chini na uvishemshe mpaka maji yote yakauke kisha tia mafuta na upike ktk moto mdogo mpaka viive.Baada ya hapo tia spice na uzipike kidogo kisha tia mihogo na kuku (kuku na mihogo vikatwe vipande vya wastani) vichanganye vizuri kisha tia nazi na vimaji kiasi,limao chumvi na pilipili na ufunike kisha punguza moto. Pika mpaka mihogo na kuku viive na ibaki rojo kidogo kisha ipua na mihogo yako itakuwa tayari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:23:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele - 1 kilo
Kuku - 1
Vitunguu - 3
Viazi/mbatata - 5
Jira/bizari ya pilau nzima - 3 vijiko vya supu
Mdalasini - 1 kijiti
Pilipili manga - 1 kijiko cha supu
Hiliki - 3 chembe
Karafuu - 5 chembe
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 3 vijiko vya supu
Tangawizi mbichi ilosagwa - 3 vijiko vya supu
Mafuta ya kupikia - ½ kikombe
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Baada ya kumsafisha kuku na kumkatakata, mchemshe kwa chumvi na ndimu, kijiko kimoja cha kitunguu thomu/somu na tangawizi yote.. Menya viazi, katakata vipande vya kiasi. Katakata vitunguu maji kisha kaanga kwa mafuta katika sufuria ya kupikia pilau. Tia bizari zote isipokuwa hiliki. Saga hiliki kisha tia pamoja na kitunguu thomu/somu ukaange kidogo. Mimina kuku na supu yake ikichemka kisha tia mchele na viazi. Koroga kisha acha katika moto mdogomdogo wali uwive kama kawaida ya kupika pilau.