Log in to access your menu with tools for managing ๐ tasks, ๐ฅ clients, ๐ฐ finances, ๐ learning, ๐ personal growth, and ๐ spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Dunia haijali mazuri yako ila ubaya wako, jiamini songa mbele
Hivyo, hili ni somo kwenu: `"Dunia haijali mazuri unayofanya hata ukiyafanya mara milioni, lakini fanya baya moja uone jinsi watakavyo kulaumu..."` "`Hata hivyo usikatetamaa, MARA ZOTE SIMAMA IMARA NA USHINDE VIKWAZO VYOTE." ` JIAMINI
Updated at: 2024-05-23 16:07:11 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Siku moja mwalimu wa shule aliandika ubaoni kama ifuatavyo: 9ร1=7 9ร2=18 9ร3=27 9ร4=36 9ร5=45 9ร6=54 9ร7=63 9ร8=72 9ร9=81 9ร10=90 Alipo maliza kuandika tu, akaona wanafunzi wote walikua wanamcheka, kwasababu alikua amekosea swali la kwanza.
Mwalimu aliwatazama wanafunzi, kisha akawaambia yafuatayo: `"Nimejikosesha lile swali la kwanza makusudi, kwasababu nilihitaji mjifunze kitu kimoja muhimu sana. Mnapaswa kujua namna ambavyo dunia inaweza kuwachukulia. Unaona hapo, nimeandika kwa usahihi mswali tisa (9), lakini hakuna kati yenu aliyenipongeza kwa hilo; wote mmecheka na kunilaumu kwasababu ya kosa moja tu nililofanya."` Hivyo, hili ni somo kwenu: `"Dunia haijali mazuri unayofanya hata ukiyafanya mara milioni, lakini fanya baya moja uone jinsi watakavyo kulaumu..."` "`Hata hivyo usikatetamaa, MARA ZOTE SIMAMA IMARA NA USHINDE VIKWAZO VYOTE." ` JIAMINI