Jina asili kwa Kiaramu ni ΧΧ¨ΧΧ, MaryΔm lenye maana ya "Bibi"; watafsiri wa kwanza wa Biblia ya Kiebrania wanaojulikana kama Septuaginta (LXX) waliliacha kama lilivyo wakiandika kwa Kigiriki ΞΞ±ΟΞ―Ξ±ΞΌ, Mariam, au walilifupisha wakiandika ΞΞ±ΟΞ―Ξ±, Maria.
Katika Kurani jina hilo kwa Kiarabu ni Ω
Ψ±ΩΩ
, Maryam.
Jina hili limeenea sana duniani kote, hasa kwa heshima ya mama wa Yesu.
Anatajwa kwa kawaida kwa kutanguliza sifa yake mojawapo, hasa Bikira.
Mapokeo ya karne ya 2 (Injili ya Yakobo) kuhusu Bikira Maria yanasema alikuwa binti pekee wa Yohakimu na Ana. Lakini habari muhimu zaidi ni zile zinazopatikana katika Biblia ya Kikristo.