Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/mobile/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Featured Image

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda.

Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?

Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote.

Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo.

Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ofanisi.
Kama umeipenda.

Share kwa wengine ili nao wazinduke.

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE
[products columns="2" ids="30827"]
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kudumisha Heshima na Utu katika Familia: Kuheshimu Tofauti na Upekee

Jinsi ya Kudumisha Heshima na Utu katika Familia: Kuheshimu Tofauti na Upekee

Familia ni sehemu muhimu sana katika maisha yetu. Ni mahali ambapo tunakua na kujifunza maadili y... Read More

Kuweka Mazingira ya Shukrani na Kuwa na Amani na Furaha katika Familia

Kuweka Mazingira ya Shukrani na Kuwa na Amani na Furaha katika Familia

Kuweka Mazingira ya Shukrani na Kuwa na Amani na Furaha katika Familia

Familia ni muhimu s... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Kujenga Ushirikiano wa Kujenga na Kuunga Mkono Ndoto za Familia

Kuweka Kipaumbele cha Kujenga Ushirikiano wa Kujenga na Kuunga Mkono Ndoto za Familia

Kujenga ushirikiano wa familia ni jambo muhimu sana katika maisha. Kuweka kipaumbele cha kujenga ... Read More

Jinsi ya Kuimarisha Upendo na Kuunda Maisha ya Ndoa yenye Maana na mke wako

Jinsi ya Kuimarisha Upendo na Kuunda Maisha ya Ndoa yenye Maana na mke wako

Kuimarisha upendo na kuunda maisha ya ndoa yenye maana na mke wako ni muhimu katika kudumisha uhusia... Read More
Kujenga Uhusiano wa Kudumu: Je, Kufanya Mapenzi ya Mara Moja Inafaa?

Kujenga Uhusiano wa Kudumu: Je, Kufanya Mapenzi ya Mara Moja Inafaa?

Kujenga uhusiano wa kudumu ni jambo muhimu sana katika maisha ya kimapenzi. Kuna mambo mengi amba... Read More

Jinsi ya Kuendelea Kujifunza na Kukua katika Ndoa

Jinsi ya Kuendelea Kujifunza na Kukua katika Ndoa

Kuendelea kujifunza na kukua katika ndoa ni muhimu sana kwa ustawi wa uhusiano wenu na kujenga ndoa ... Read More
Jinsi ya Kusaidia Watoto kukabiliana na Teknolojia na Matumizi ya Mtandao

Jinsi ya Kusaidia Watoto kukabiliana na Teknolojia na Matumizi ya Mtandao

Habari za leo wapendwa wasomaji! Hii ni makala ya kujadili jinsi ya kusaidia watoto kukabiliana n... Read More

Jinsi ya Kuimarisha Uimara na Uthabiti wa Ndoa na mke wako

Jinsi ya Kuimarisha Uimara na Uthabiti wa Ndoa na mke wako

Kuimarisha uimara na uthabiti wa ndoa na mke wako ni muhimu katika kudumisha uhusiano wa ndoa wenye ... Read More
Vidokezo vya Kuwa na Tarehe ya Kimapenzi na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Tarehe ya Kimapenzi na Msichana

Kama wewe ni miongoni mwa wanaume wanaotaka kuwa na tarehe ya kimapenzi na msichana, kuna vidokez... Read More

Mambo 5 ambayo wanawake wanatamani mwanaume ajue wakati wa kufanya mapenzi

Mambo 5 ambayo wanawake wanatamani mwanaume ajue wakati wa kufanya mapenzi

Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo wanawake hutamani sana wanaume zao wawe wanajua katika mapenzi, il... Read More

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kukosa Mawasiliano na Kuwa na Mipasuko katika Familia Yako

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kukosa Mawasiliano na Kuwa na Mipasuko katika Familia Yako

Karibu katika makala yetu inayojadili njia za kupunguza mazoea ya kukosa mawasiliano na kuwa na m... Read More

Je, watu wanapendelea kujaribu kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kujaribu kufanya mapenzi?

Habari za leo wapendwa wasomaji! Leo, tunajadili kuhusu je, watu wanapendelea kujaribu kufanya ma... Read More

πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About