Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/mobile/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Jinsi ya kumfanya mwanamke afurahi na akupende kwa kumfanyia mambo anayoyataka

Featured Image

Kuna mambo ya msingi ambayo mwanamke anahitaji kutoka kwa mwanamme ili kufurahi na kutulia katika mahusiano japokuwa sio rahisi kukwambia mojakwa moja.

Mambo hayo ni kama ifuatavyo;

Kupewa nafasi na kipaumbele.

Wanawake wanapenda kuwa namba moja au kupendwa kuliko yeyote. Kumpenda mwanamke haikuishii kwenye kumpata na kumliki, kisha kujisahau kwa kisingizio kuwa umemuoa au umemvisha pete ya uchumba, ni zaidi ya hapo. Wanawake wanapenda watangulizwe katika mapenzi na kusiwepo na mwingine wa kuchukua nafasi yao katika mazungumzo na mapenzi kwa ujumla na katika maisha yao.

ย 

Kuheshimiwa

Wanawake wanapenda kueshimiwa kwa maneno na matendo. Wanawake hawapendi kuitwa majina mabaya kwa mfano mjinga, Malaya au kulinganishwa na wanawake wenzao wabaya. Wanawake hawapendi kukosewa heshima hasa mbele za watu, hata kama ni kwa mambo madogo madogo.

Kuridhishwa Kwenye tendo la ndoa

Mwanamke anapenda aridhishwe Kwenye tendo la ndoa. Hata kama utakuwa na kiwango kikubwa cha mapenzi juu ya mpenzi wako kwa kiwango gani, ukiwa dhaifu katika tendo la ndoa utayumbisha penzi lako. Utundu na ufundi unahitajika ili kumkata kiu mpenzi wako. Mwanamme anatakiwa kuhakikisha kuwa anamtosheleza mpenzi wake katika tendo hilo.

ย 

Nafasi ya kuongea na kujieleza

Wanawake wanapenda wapewe nafasi ya kuongea na kujieleza vile watakavyo. Mpe uhuru mpenzi wako kuzungumza na kumsikiliza bila kumkatiza kwa ukali pale anapoongea sana. Kwa kawaida wanawake wanatajwa kuzungumza maneno 25,000 kwa siku, wakati wanaume wakibaki na kiwango cha maneno 5,000 kwa siku, wanawake hupenda zaidi kujieleza walivyo mbele ya wengine. Kwa hiyo wakizuiwa wasiongee hujiona kama wanakosa nafasi muhimu ya kueleza mawazo yao.

ย 

Kusaidiwa katika shida na matatizo yao

Wanawake wengi hutegemea kuwa wanapokuwa na wapenzi watasaidiwa katika matatizo ya kimaisha na migogoro ya kimawazo. Kwa mfano ushauri juu ya maisha yao, kulindwa na hatari za kimaisha, kusaidiwa katika shida na kuongozwa pale wanapohisi kushindwa kufanya jambo. Kama mwanaume hatamfanyia mpenzi wake hili atakuwa amekosa sifa za kuteka penzi la mwanamke.

Kubembelezwa

Wanawake hupenda kubembelezwa hasa pale wanapokuwa na huzuni. Wanawake wengi hupenda kuelimishwa zaidi kuliko kufokewa. Wanawake hawapendi kukaripiwa, mara nyingi hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na misuguano na wengine. Ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa.

Mfahamu zaidi Mwanamke kwa Kupitia Kitabu hiki kizuri cha SIRI ZA MWANAMKE
[products columns="2" ids="30827"]
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Njia za Kujenga Ushirikiano na Msichana katika Malengo ya Pamoja

Njia za Kujenga Ushirikiano na Msichana katika Malengo ya Pamoja

Kuwashirikisha wasichana katika malengo ya pamoja ni jambo muhimu sana katika jamii yetu. Wasicha... Read More

Siri za kumpata mpenzi bora

Siri za kumpata mpenzi bora

Jinsi ya kupata mpenzi bora
1_ lazima na wewe uwe bora kwanza
Read More

Kuweka Kipaumbele cha Amani na Furaha katika Maisha ya Familia Yako

Kuweka Kipaumbele cha Amani na Furaha katika Maisha ya Familia Yako

Kuweka kipaumbele cha amani na furaha katika maisha ya familia yako ni muhimu sana. Familia ni ki... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na mabadiliko ya kibinafsi na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na mabadiliko ya kibinafsi na mpenzi wako

Kuelewa na kukabiliana na mabadiliko ya kibinafsi ni sehemu muhimu ya uhusiano wenye afya na mpenzi ... Read More
Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mazingira ya upendo na kuunga mkono ndoto za kila mmoja

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mazingira ya upendo na kuunga mkono ndoto za kila mmoja

Kuwa na mpenzi ambaye mnashirikiana ndoto na kujenga maisha pamoja ni mojawapo ya vitu vizuri zai... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Uvumilivu na Mshikamano katika Familia

Kuweka Kipaumbele cha Uvumilivu na Mshikamano katika Familia

Kuweka Kipaumbele cha Uvumilivu na Mshikamano katika Familia

Familia ni muhimu sana katika... Read More

Kuweka Nafasi ya Kujifunza na Kukuza katika Mahusiano yako

Kuweka Nafasi ya Kujifunza na Kukuza katika Mahusiano yako

Kuweka nafasi ya kujifunza na kukuza katika mahusiano yako ni muhimu sana. Mahusiano ni kitu kizu... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mipango ya Baadaye katika Familia: Kuweka Maono ya Pamoja

Jinsi ya Kuwa na Mipango ya Baadaye katika Familia: Kuweka Maono ya Pamoja

  1. Kuanzisha mawasiliano ya wazi: Ili kuweza kufikia malengo ya pamoja kama familia, ni mu... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kimawazo na maadili na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kimawazo na maadili na mpenzi wako

Katika uhusiano, tofauti za kimawazo na maadili ni jambo ambalo linaweza kusababisha migogoro kat... Read More

Mwanamme: Namna ya Kutunza Familia, Kukaa na Mke na Kulea watoto wa kike na wa kiume inavyotakiwa

Mwanamme: Namna ya Kutunza Familia, Kukaa na Mke na Kulea watoto wa kike na wa kiume inavyotakiwa

Read More
Je, watu wanapendelea kujaribu mbinu za kuleta msisimko wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kujaribu mbinu za kuleta msisimko wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Karibu kwenye blogi hii ambapo tutazungumzia kuhusu mbinu za kuleta msisimko wakati wa ngono/kufa... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za tabia na mienendo ya watoto wenu na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za tabia na mienendo ya watoto wenu na mpenzi wako

Kama wazazi na wenzi, tunajua kuwa kuna tofauti katika tabia na mienendo yetu. Lakini pia, inawez... Read More

๐Ÿ“– Explore More Articles