Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰

Nini kinachokufanya udhani utashindwa sasa?

β€’
Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image

Kwa mujibu wa Biologia, baada ya tendo la kukutana kimwili takribani mbegu milioni 200 hadi 300 hutolewa na mwanaume…halafu zote huanza kupiga mbizi kuogelea kwenye njia safarini kukutana na yai la kike.

Ajabu ya kwanza ni kwamba sio zote 200 - 300 ambazo hufanikiwa kulifikia yai( nyingi huchoka na kufia njiani maana si mashindano ya mchezo mchezo).
Ajabu ya pili ni kwamba kati ya hizi 300 zinazofanikiwa kufikia yai, ni moja tu..moja tu itakayoshinda nakufanikiwa kupenya na kurutubisha yai, na kwa mantiki hii ILIYOSHINDA NI WEWE HAPO.

Umewahi kuwaza kuhusu hili vizuri?
Yaani ulishindana mbio hizo ukiwa huna macho na ulishinda, ulishindana bila elimu na ukashinda,ulishindana bila hata cheti chochote wala msaada wa yeyote ….na UKASHINDA.

Nini kinachokufanya udhani utashindwa sasa?
Tena sasa uko na macho yote, miguu, sasa Unamjua Mungu, sasa ukiwa na mipango,ndoto na maono.
Kumbuka ULISHASHINDA toka tumboni huna sababu ya kuwa na hofu yeyote, PAMBANA

AckySHINE Solutions
✨ Join AckySHINE for more features! ✨

Comments 0

Please log in or register to comment or reply.
No comments yet. Be the first to share your thoughts! πŸ“

πŸ”— Related Posts

🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About