Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/mobile/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Jinsi ya Kulima Mgagani: Kilimo bora cha Mgagani

Featured Image

Utangulizi

Migagani, migange, mikabili au miangani ni mimea ya jenasi Cleome katika familia na oda Brassicales (kabichi). Mgagani (Cleome gynandra) au Spider plant kwa kingereza, ni mmea wa asili ya Afrika unaostawi vizuri kwa kumwagiliwa hapa afrika ya mashariki wakati wa joto. Pia huchumwa mashambani ikiwa imeota yenyewe zao hili hushambiliwa na magonjwa na wadudu mara chache. Majani na Matawi machanga yana virutubisho kuliko Sukuma wiki na kabichi. Mahitaji yake yanaongezeka kwenye miji midogo na mikubwa kila siku.

Mgagani wa kawaida, huliwa takriban kila mahali pa Afrika na katika mabara mengine pia. Wanawake wengi wenye mimba au waliozaa hula mmea huu, kwa sababu una chuma nyingi kiasi na husaidia kuongeza damu. Mboga ya mgagani huitwa magagani.

Aina Za Mgagani

Kwa Afrika kuna aina 50 za mgagani , lakini ni aina nne tu zinazoliwa. Aina bora zinazalishwa na kituo cha AVRDC-THE WORLD VEGETABLE CENTER zina majani mapana, uchungu kidogo na ina majani mengi Zaidi na huvunwa kwa muda mrefu. Aina hizi ni pamoja na PS ambayo ina shina na matawi ya zambarau na GS I yenye shina na matawi ya kijani, mbegu za aina bora zina weza kupatikana toka kwenye kituo cha the world Vegetable Center, Arusha Tanzania. Ikumbukwe kuwa wakilima wengi wa nchi za Tanzania na kenya wanalima na kuuza mbegu za aina hizi na pia baadhi ya makampuni ya mbegu yameanza kuuza.

Mazingira Mgagani Unapoota

Kwa asili mgagani unastawi vizuri sehemu zenye joto na udongo wa aina mbalimbali kama tifutifu. Zao hili halikui vizuri katika udongo unaotuamisha maji, au katika maeneo ya baridi au kivuli. Katika eneo la mita za mraba 1-2, familia inaweza kupata mgagani wa kula kwa muda wa miezi minne.

ย 


Kutayarisha Shamba La Kuotesha Mgagani

Anza kwa kutifua ardhi vizuri na changanya na mbolea ya samadi kwa kiwango cha kilo moja hadi mbili kwa mita mraba. Mgagani waweza kuoteshwa peke yake au kwa kuchanganywa na mazao mengine kama mnavu au mchicha.

Uoteshaji Wa Mgagani

Baada ya kuandaa shamba lako sia mbegu kwa kutawanya au katika mstari ya umbali wa sm 30-50, majira ya mvua au kwa kumwagilia, kina cha mstari kisizidi sm1, funika kwa udongo kidogo na mwagilia kama hakuna mvua. Punguza miche iliyosongamana inapokuwa na majani manne hadi matano na iwe katika nafasi ya sm 15-20 toka mche hadi mche kwa upandaji wa kutawanya.

Palizi Ya Mgagani

Hakikisha shamba ni Safi hasa mwezi wa kwanza baadae magugu yanaweza kuzuliwa Na kivuli cha mgagani umeota vizuri.

Umwagiliaji Wa Mgagani

Unyevu wa kutosha ni muhimu kwa zao hili na inashauriwa kumwagilia ni majira ya kiangazi angalau mara mbili kwa wiki. Mgagani hustahimili ukame kuliko nyanya au mchicha lakini mimea isiachwe ikanyauka.

Uvunaji Wa Mgagani

Kwa uvunaji wa moja kwa moja mimea inaweza kungโ€™olewa baada ya wiki nne hadi sita, kwa kuvuna majani, uchumaji unaweza kufanyika kila mara hadi miezi minne, Mimea iliyo na umri wa Zaidi ya miezi minne, inaweza kukatwa shina na kuchipua na kuendelea kuvunwa baada ya wiki nne hadi miezi minne kulingana na hali ya hewa na matunzo.

ย 

Uzalishaji Wa Mbegu Za Mgagani

Kwa kawaida mgagani hutoa mbegu kwenye shina au matawi vifuko vya mbegu vikikauka huwa mbegu imekomaa. Mimea ikatwe usawa wa ardhi na kutungiwa kwenye sakafu. Safi na ngumu, kuondoa mbegu toka kwenye maganda. Ondoa maganda, mashina na majani yaliyochanganyika na mbegu. Uchafu mwingine mbegu zihifadhiwe katika mifuko ya plastiki au ya karatasi au makopo na kuweka sehemu iliyo kavu. Kwa kuwa mbegu zina mafuta ya asili ya dawa za kuua wadudu ni vigumu sana kushambuliwa na wadudu waharibifu.

Mauzo Ya Mbegu Za Mgagani

Makundi ya wakulima yaliyopata mafunzo ya uzalishaji wa mbegu sasa yanazalisha kwa ajili ya wakulima wengine. Katika nchi ya kenya ambapo mgagani unaliwa sana, uzalishaji wa mbegu hupatia wakulima mapato Zaidi kuliko kuzalisha mboga mbegu za mgagani zinaptikana madukani.

Mauzo Ya Mgagani

Matawi malaini na machanga yenye majani yanaweza kuvunwa na kuwekwa kwenye mafungu ya uzito wa gramu 100-200. Majani yaliyo kaushwa kwa jua na kuwekwa kwenye vyombo mbalimbali huuzwa.

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Faida ya kupanda maharagwe katikati ya kabichi

Faida ya kupanda maharagwe katikati ya kabichi

Maharagwe yanapandwa kwenye kabichi yanafanya kazi zifuatazo;

Kudhibiti wadudu (... Read More

Jinsi ya kutengeneza mbolea ya mboji kitaalamu na kwa urahisi

Jinsi ya kutengeneza mbolea ya mboji kitaalamu na kwa urahisi

Mbolea ya mboji hutokana na mabaki ya majani na miti. Majani na miti yanapooza hugeuka na kutenge... Read More

Jinsi ya Kufuga vizuri kware Kwa Faida

Jinsi ya Kufuga vizuri kware Kwa Faida

Kware au Read More

Jinsi ya kutunza nyumba ya kuku ili kuzuia magonjwa

Jinsi ya kutunza nyumba ya kuku ili kuzuia magonjwa

1. Nyumba ya kuku iwe safi na kavu muda wote kuzuia ueneaji na kuzaliana kwa vijidudu vya magonjwa ... Read More
Jinsi vitunguu swaumu vinavyosaidia kuzuia wadudu shambani

Jinsi vitunguu swaumu vinavyosaidia kuzuia wadudu shambani

Vitungu saumu vina manufaa sana katika kukabiliana na aina mbalimbali za wadudu waharibifu na baadhi... Read More
Namna ya kukabiliana na Magonjwa ya kuku

Namna ya kukabiliana na Magonjwa ya kuku

Hakikisha unamuona mtaalamu wa mifugo mara uonapo dalili zozote za kuumwa kwa mifugo wako. Tenga na... Read More
Aina kuu ya mizinga bora ya nyuki kwa ajili ya kupata asali nyingi

Aina kuu ya mizinga bora ya nyuki kwa ajili ya kupata asali nyingi

Mizinga ya Kifuniko juu (Top bar)

Hii ni aina ya mizinga inayotumika sana na weng... Read More
Kilimo kizuri cha pilipili hoho

Kilimo kizuri cha pilipili hoho

Pilipili hoho ni zao la jamii ya pilipili isiyo kali, tunda lake ni nene ki... Read More

Ufugaji wa nguruwe na faida zake

Ufugaji wa nguruwe na faida zake

Na, Patrick Tungu