Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/mobile/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Jinsi ya kulima vitunguu (vitunguu maji) kwa mbinu za kilimo bora na kwa faida

Featured Image

Vitunguu ni zao la mbogamboga na hulimwa kwa ajili ya balbu zake ambazo hutumika kama kiungo cha chakula. Vitunguu vina matumizi mengi sana na vina madini joto, chuma, vitamin A, vitamin B, vitamin C na vitamin E.
Vitunguu hulimwa na hukubali zaidi nyanda za baridi. Nyanda zenye joto vitunguu hulimwa pia. Vitunguu vinaweza kulimwa mwaka mzima endapo maji yanapatikana.

Aina za vitunguu vinavyolimwa Tanzania

  • Red Creole
  • Bombay Red
  • Hybrid F1

Hali ya hewa

Joto linatakiwa sana kwa ajili ya ukuaji wa balbu ila joto likizidi vitunguu hukomaa mapema kabla balbu hazijafikia ukubwa unaostahili, hivyo mkulima anaweza kupata mazao kidogo.

Udongo

Vitunguu huweza kupandwa kwenye udongo wowote wenye rutuba, usiotuamisha maji na usionata sana. Hufanya vizuri kwenye udongo wenye asidi kidogo japo udongo wenye alkali kidogo sio mbaya sana. Kwenye udongo wenye mchanga mchanga umwagiliaji ni lazima. Udongo mzuri sana kwa ustawi wa vitunguu ni tifutifu-kichanga.

Mbolea

Epuka matumizi ya mbolea mbichi isioiva vizuri kwani husababisha vitunguu kuwa na shingo pana sana majani hukua sana badala ya balbu.

Umwagiliaji

Umwagiliaji ni muhimu sana hasa wakati wa kuanza kutengeneza balbu. Unyevu uliozidi ni hatari sana kipindi cha ukuaji.

Kitalu cha vitunguu

Ni muhimu kumwagilia maji ya kutosha siku kumi za mwanzo tangu kusia mbegu kitaluni. Vitunguu hukaa kitaluni kwa wiki 6-8 na miche ifikiapo upana wa penseli na urefu wa sm 15 ni tayari kwa kuhamishia shambani/bustanini.

Upandaji

Kabla ya kupanda udongo ni lazima utifuliwe vizuri na reki kuondoa mabaki ya mimea na mawe ama Vipande vikubwa vya udongo. Matuta yawe na upana wa mita moja. Vitunguu hupandwa kwa mstari mojakwamoja ama kutokea kitaluni. Pia huweza kupandwa kwa mstari pacha. Vitunguu hupandwa sm 10-15 kutoka mmea hadi mmea na sm 10-15 kutoka mstari hadi mstari, kama inavyoonekana kwenye mchoro hapa chini. Pia epuka kupanda vitunguu mahali palipopandwa mboga jamii ya vitunguu siku za nyuma. Mfano Vitunguu saumu na vitunguu majani.

Utunzaji wa shamba

Kutandazia shamba na majani yaliyooza vizuri ama mabua inashauriwa ili kuongeza ruba ya ardhi, zuia magonjwa yatokanayo na udongo na magugu. Kupanda vitunguu kwenye matuta yaliyoinuka ni muhimu sana kuzuiya utuamishaji wa maji na mlipuko wa magojwa ya miche. Kungoa magugu na uvunaji ufanywe kwa mkono.
Vitunguu hufanya vizuri kama shamba litawekewa mbolea ya samadi ama mboji ilioiva vizuri. Kiasi cha tani 25-40 kwa heka kinashauriwa. Hii ni sawa na kilo 7.5 -12 kwa tuta lenye urefu wa mita 3 na upana wa mita 1.

Uvunaji

Vitunguu huvunwa kuanzia siku 90-150 tangu kusia mbegu. Dalili za kukomaa ni kuanguka kwa majani. Vitunguu huvunwa kwa kuvuta kwa mkono na kuhifadhiwa siku kadhaa shambani vikiwa vimefunikwa na majani. Baada ya hapo majani hukatwa na balbu hupakiwa kwa ajili ya kuhifadhi kusubiria bei nzuri. Vitunguu huweza kuhifadhiwa hadi miezi 9 tangu vivunwe bila kuharibika. Vitunguu vihifadhiwe kwenye nyuzijoto chini ya 4.4ย ยฐC ama juu ya nyuzijoto 25ยฐC ili visiharibike.

Yafahamu Mambo Mbalimbali ya muhimu kuhusu kilimo cha Mazao ya Mboga Mboga kwa Ku-Download Kitabu cha MBINU ZA KILIMO BORA CHA MBOGA

Ni kitabu kinachotoa elimu ya Kilimo Cha Mboga. Kipo katika Mfumo wa PDF (Soft copy).

Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10, ambayo ni nyanya, kabichi, bamia, vitunguu maji, vitunguu twaumu, hoho, matikiti, karoti, uyoga na matango. Bila kusahau kilimo cha mboga kama chainizi na mchicha.

Pia utaweza kufahamu mbinu mbalimbali za kilimo cha mboga kama vile kuandaa shamba na kitalu, udhibiti wa wadudu na magonjwa katika mboga, kuvuna na kuhifadhi mboga, vilevile utajifunza kuhusu kilimo cha matone.

Kitabu hiki niย Soft copy [pdf]ย kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

[products columns="2" ids="30832"]
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Mbinu za kulima parachichi ili kupata faida

Mbinu za kulima parachichi ili kupata faida

Kilimo cha Parachichi nacho kinalipa ukilima.

Na, Patrick Tungu

Utangulizi

M... Read More

Kilimo bora cha matikiti maji

Kilimo bora cha matikiti maji

Ili kulima tikiti maji, inakubidi uwe na sehemu ya kutosha, yenye jua la kutosha, maji mengi na a... Read More

Mambo 8 ya kuzingatia kabla ya kuleta mifugo (kuku, ng'ombe,mbuzi n.k) wapya bandani

Mambo 8 ya kuzingatia kabla ya kuleta mifugo (kuku, ng'ombe,mbuzi n.k) wapya bandani

Mambo hayo ni haya yafuatayo; 1. Hakikisha unaondoa matandazo yote ndani ya nyumba, 2. Ondoa vyombo ... Read More
Jinsi vitunguu swaumu vinavyosaidia kuzuia wadudu shambani

Jinsi vitunguu swaumu vinavyosaidia kuzuia wadudu shambani

Vitungu saumu vina manufaa sana katika kukabiliana na aina mbalimbali za wadudu waharibifu na baadhi... Read More
Mbinu za kuzuia magonjwa kwa kuku

Mbinu za kuzuia magonjwa kwa kuku

Mbinu hizo ni hizi zifuatazo;

Read More

Matumizi ya mihogo kama dawa ya kuzuia wadudu kwenye mimea

Matumizi ya mihogo kama dawa ya kuzuia wadudu kwenye mimea

Muhogo Inazuia Minyoo na vidukari.

Hatua za Kutayarisha dawa

KILIMO BORA CHA ZAO LA MBAAZI

KILIMO BORA CHA ZAO LA MBAAZI

Utangulizi

Mbaazi ni zao la chakula ambalo pia linaweza kulimwa kama zao la bi... Read More

Mambo makubwa yanayosababisha kulazimika kulima au kutifua udongo

Mambo makubwa yanayosababisha kulazimika kulima au kutifua udongo

Kutifua udongo ni jambo la muhimu sana ili kuufanya udongo kuwa bora.

<... Read More
Aina kuu ya mizinga bora ya nyuki kwa ajili ya kupata asali nyingi

Aina kuu ya mizinga bora ya nyuki kwa ajili ya kupata asali nyingi

Mizinga ya Kifuniko juu (Top bar)

Hii ni aina ya mizinga inayotumika sana na weng... Read More
๐Ÿ“– Explore More Articles