Uhusiano mzuri na wazazi ni muhimu sana siyo katika masuala ya uchaguzi wa mchumba tu, bali katika masuala yote ya msingi maishani. Kwa hiyo, hatua ya kwanza ni kujaribu kuelewana nao.
Mara nyingi vijana hufikiri wazazi hawaelewi maisha ya vijana wa kisasa. Mara nyingine hufikiri kwamba mila na desturi zinamzuia kijana kufanya uamuzi ambao unafaa. Pia wengine hufikiri kwamba tofauti ya malengo kati ya vijana na wazazi huleta mgongano.
Hali kama hii ikijitokeza, ni vizuri kuwasiliana na wazazi kwa nia ya kuelewana. Usisahau kwamba wazazi wakati wote wanajaribu kujena maisha bora ya baadaye ya watoto wao. Unapowasiliana na wazazi jaribu kuwaeleza kwa heshima na upole kwa nini hukubaliani na mawazo yao na kwa nini unaona uamuzi wako unafaa. Inawezekana kwa kufanya hivi unaweza kupata ridhaa ya wazazi wako.
Kama hujawahi kuzungumza na wazazi wako kwa karibu, mara nyingi i i inakuwa vigumu kuanzisha mazungumzo. Jaribu kuanza kwa mazungumzo rahisi. Tafuta muda mzuri wa kuanzisha mazungumzo. Usianzishe mazungumzo na wazazi wakati wamechoka au wakati wametingwa na kazi nyingi; hawatakusikiliza. Jaribu kuwa wazi na mkweli, na waonyeshe wazazi wako kwamba unayajali mawazo yao. Kwa kufanya hivyo wazazi wako wanaweza kukuamini na kuafikiana na wewe katika maswali mazito zaidi. Vilevile onyesha kwamba unawaheshimu. Inachukua muda mrefu kufanikisha mawasiliano mazuri na wazazi, lakini ni vema kuyaanzisha mapema kwa ajili ya kufanikisha lengo la mawasiliano mazuri na wazazi.
Uhusiano mzuri na wazazi ni muhimu sana siyo katika masuala ya uchaguzi wa mchumba tu, bali katika masuala yote ya msingi maishani. Kwa hiyo, hatua ya kwanza ni kujaribu kuelewana nao. Mara nyingi vijana hufikiri wazazi hawaelewi maisha ya vijana wa kisasa. Mara nyingine hufikiri kwamba mila na desturi zinamzuia kijana kufanya uamuzi ambao unafaa. Pia wengine hufikiri kwamba tofauti ya malengo kati ya vijana na wazazi huleta mgongano. Hali kama hii ikijitokeza, ni vizuri kuwasiliana na wazazi kwa nia ya kuelewana. Usisahau kwamba wazazi wakati wote wanajaribu kujena maisha bora ya baadaye ya watoto wao. Unapowasiliana na wazazi jaribu kuwaeleza kwa heshima na upole kwa nini hukubaliani na mawazo yao na kwa nini unaona uamuzi wako unafaa. Inawezekana kwa kufanya hivi unaweza kupata ridhaa ya wazazi wako. Kama hujawahi kuzungumza na wazazi wako kwa karibu, mara nyingi i i inakuwa vigumu kuanzisha mazungumzo. Jaribu kuanza kwa mazungumzo rahisi. Tafuta muda mzuri wa kuanzisha mazungumzo. Usianzishe mazungumzo na wazazi wakati wamechoka au wakati wametingwa na kazi nyingi; hawatakusikiliza. Jaribu kuwa wazi na mkweli, na waonyeshe wazazi wako kwamba unayajali mawazo yao. Kwa kufanya hivyo wazazi wako wanaweza kukuamini na kuafikiana na wewe katika maswali mazito zaidi. Vilevile onyesha kwamba unawaheshimu. Inachukua muda mrefu kufanikisha mawasiliano mazuri na wazazi, lakini ni vema kuyaanzisha mapema kwa ajili ya kufanikisha lengo la mawasiliano mazuri na wazazi.
π¬
Discussion
Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.
0 comment(s)
π Login required to comment or reply
You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.
Hata kama utafanya kila kitu usibakwe bado inaweza ikatokea. Ubakaji na unyanyasaji wa ujinsia unaweza kutokea kwa kila mtu. Hata hivyo kuna baadhi yaβ¦
Kujenga uhusiano na msichana ni jambo muhimu katika maisha ya kimapenzi. Uhusiano unapokuwa imara, huwa ni rahisi kwa pande zote mbili kuwa na furaha β¦
Inawezekana kwa msichana au mwanamke aliyebakwa kupatamimba. Uwezekano wa kupata mimba ni sawa kama vile amekubalimwenyewe au kulazimishwa. Iwapo mwatβ¦
Tunaposema dawa za kulevya ina maana ni matumizi mabaya ya dawa na hasa pale yatumikapo kinyume cha maelekezo ya tabibu na hivyo kuleta madhara kwa mtβ¦
Je, muda wa kufanya ngono/kufanya mapenzi ni muhimu? Hili ni swali ambalo huwa linawasumbua wapenzi wengi. Wengine husema ni muhimu kufanya mapenzi maβ¦
Jinsi ya Kuonyesha Utambulisho Wako kwa Msichana Kuonyesha utambulisho wako kwa msichana ni hatua muhimu katika kujenga uhusiano wa karibu na mwenzakoβ¦
Discussion
Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.
You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.
Log in to participate