
Dalili za kwanza za msichana au mwanamke kuwa na mimba ni zipi?

Dalili moja i iliyo wazi zaidi ni kukosa hedhi. Mwanamke akijamii ana na mwanaume bila kutumia kinga yoyote na asipopata hedhi katika muda unaotakiwa, mara nyingi i i ina maana kwamba amepata mimba.
The ListPages module does not work recursively.
Dalili nyingine ni kuvimba matiti na chuchu kuchomachoma. Baadhi ya wanawake wanaota mavuzi mengi na wengine wengi rangi ya chuchu i inabadilika kuwa nyeusi. Pia, karibu nusu ya wanawake wajawazito huumwa tumbo na wengine hutapika. Wanawake wengi husikia mkojo mara kwa mara na wengine hujisikia wachovu na kuona kizunguzungu, hasa katika miezi mitatu ya mwanzo. Wakati mwingine wanawake hupenda au huchukia baadhi ya vyakula.
Ili mwanamke awe na uhakika kama ni mjamzito au hapana, akapimwe mkojo kwenye kliniki au hospitalini, mara anapokuwa na wasiwasi Comments
Please log in or register to leave a comment or reply.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!