VIPIMO VYA WALI
Mchele wa hudhurungi (brown rice)
na (wild rice kidogo ukipenda)Osha na Roweka - 2 Vikombe
Kitungu maji - 1 Kiasi
Kitunguu saumu - 1 Kijiko cha supu
Bizari ya manjano - 1/2 Kijiko cha chai
Mdalasini nzima - 1 kijiti
Iliki iliyosagwa - 1/4 Kijiko cha chai
Chumvi - Kiasi
Pilipili manga - 1/4 Kijiko cha cha
Mafuta - 2 Vijiko vya supu
Majani ya Bay(bay leaves) - 1
Mbegu ya giligilani iliyoponwa (coriander seeds) - 1 Kijiko cha chai
Supu ya kuku ya vidonge - 1
Maji ya wali - 4 vikombe
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
Kaanga kitungu, kabla ya kugeuka rangi tia thomu.
Kisha weka bizari zote na ukaange kidogo.
Tia mchele kisha maji na ufunike upike katika moto mdogo.
Na ikishawiva itakuwa tayari kwa kuliwa na kabeji na kuku wa tanduuri.
VIPIMO VYA KABEJI
Kabeji iliyokatwa katwa - 1/2
Karoti iliyokwaruzwa - 1-2
Pilipili mboga kubwa - 1
Figili mwitu (celery) iliyokatwa - 1 au 2 miche
Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 Kijiko cha supu
Pilipili mbichi - 1
Kisibiti (caraway seed) - 1/4 Kijiko cha chai
Bizari ya manjano ya unga = 1/2 Kijiko cha chai
Giligani ya unga - 1 Kijiko cha chai
Chumvi - Kiasi
Kitungu maji kilichokatwa -1
Kotmiri - upendavyo
Mafuta ya kukaangia - Kiasi
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
Kwenye sufuria kaanga kitungu, figili mwitu kisha tia thomu na pilipili zote.
Halafu tia bizari zote na ukaange kidogo.
Kisha weka kabeji na chumvi, ufunike moto mdogo ilainike kidogo na sio sana
Tia karoti na usiwache motoni sana, kisha zima moto na inyunyizie kotmiri juu.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!