Naamini umeshawahi kusikia kuhusu changamoto ya uvimbe kwenye kizazi kwa Wanawake yaani Fibroids. Uchunguzi unaonesha kuwa kati ya asilimia 30 mpaka 70 ya wanawake wapo kwenye hatari ya kupata tatizohili au wengine Tayari wameshalipata. Mpaka hivi sasa hakuna Sababu ya moja kwa moja ambayo inaelezwa kama chanzo cha tatizo hili.
JE NI NANI YUPO HATARINI ZAIDI KULIPATA UVIMBE KWENYE KIZAZI?
Ni Wanawake ambao wanakaribia kukoma hedhi (Menopause) hasa wa kati ya miaka ya 38-45.
Pia Wanawake wanene au wenye Matumbo makubwa (Obesity)
Pia wanawake wasiokuwa na watoto wapo kwenye hatari zaidi ukifananisha na wale wenye Watoto.
DALILI ZA UVIMBE KWENYE KIZAZI NI ZIPI
Tatizo hili linaweza kuwa na Dalili au Kutokuwa na Dalili kabisa. Lakini kwa mara nyingi Dalili zake ni hiziโฆ
๐๐ฟKutoka kwa Hedhi nzito pia kwa muda zaidi ya kawaida.
๐๐ฟDamu kutoka kipindi ambacho sio cha siku zake.
๐๐ฟMaumivu ya Sehemu za Kiuno.
๐๐ฟMaumivu ya Chini ya Mgongo.
๐๐ฟKwenda haja ndogo mara nyingikwa hali isiyo ya kawaida.
๐๐ฟMaumivu wakati wa tendo la ndoa.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!