Jinsi ya kupika Pilau Ya Nyama Ya Ng'ombe Na Nyanya

✍️ SW - Melkisedeck ShineπŸ“… 2022-04-10 07:51:57πŸ’¬ 0 comments⏱️ ~1 min read
πŸ“„ PDF

Viambaupishi

Mchele (Basmati) 3 vikombe Nyama ya ngo’mbe 1Β kg Pilipili boga 1 kubwa Nyanya 2 kubwa Vitunguu maji 2 vikubwa Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa 1 kijiko cha supu Tangawizi 1 kijiko cha chai Ndimu 1 Mafuta ya kupikia Β½ kikombe Mdalasini Β½ kijiko cha chai Binzari nyembamba 1 kijiko cha chai Pilipili manga Β½ Kijiko cha chai Hiliki Β½ Kijiko cha chai

Jinsi ya kuandaa na kupika

Loweka mchele wako katika chombo Chukuwa nyama na ioshe vizuri na itie thomu, tangawizi, ndimu, pilipili manga na chumvi kiasi Iweke jikoni hadi ikauke maji na kuwa imewiva huku ukiikaanga kaanga kwa hayo hayo mafuta yake hadi kuwa rangi ya hudhurungi katakata Vitunguu na nyanya weka pembeni Chukua pilipili boga, thomu, tangawizi na visage katika mashine ya kusagia Weka sufuria pembeni na utie mafuta, subiri yapate moto Kisha tia vitunguu na vikaange hadi kuwa hudhurungi na tia nyanya Kisha mimina mchanganyiko wako ulio usaga wa pilipili boga, thomu na tangawizi Koroga kwa dakika kadhaa Kisha mininia nyama uliyokuwa tayari, maji kiasi na chumvi wastani na subiri maji hayo yachemke Weka mchele humo na koroga kiasi na onja chumvi kama ipo sawa au kama ndogo unaweza kuongeza Funika na punguza moto na uache uive taratibu Baada ya kukauka maji kabisa basi ugeuze na subiri tena kwa dakika kama mbili na tayari kuliwa.
πŸ’¬

Discussion

Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.

0 comment(s)
πŸ” Login required to comment or reply

You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.

Log in to participate
No comments yet.