
Mafundisho ya Msingi kuhusu Roho Mtakatifu

Roho Mtakatifu ndiye Mlezi wa ndani wa sala ya Kikristo
Kusadiki kwa Roho Mtakatifu maana yake ni kusadiki kwa nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu
Roho Mtakatifu huitwa pia Mfariji wa kweli, Roho wa Bwana, Roho wa Kristu
Alama zinazowakilisha Roho Mtakatifu ni hizi; Maji, Mpako wa mafuta, Moto, wingu, tendo la kuweka mikono, njiwa
Neno Manabii maana yake ni waliovuviwa na Roho Mtakatifu waseme kwa jina la Mungu
Roho Mtakatifu aliwashukia Mitume siku ya Pentekoste, yaani siku ya hamsini toka Pasaka. (Mdo 2:1-4)
Roho Mtakatifu aliwatia Mitume Mwanga wa nguvu ili waweze kuhubiri Injili na kueneza Kanisa kote duniani
Roho Mtakatifu anatufanyia haya;
1. Anatuangaza tufahamu mafundisho ya dini
2. Anatuimarisha tutende mema na kuacha mabaya
3. Anatutakasa na kutututia uzima rohoni mwetu
4. Analiongoza Kanisa. (Yoh 16:13-15)
Roho Mtakatifu anatutakasa kwa;
1. Neema ya utakaso
2. Fadhila za Kimungu na vipaji vyake
Maandiko Matakatifu ndiyo vitabu vyote 73 ambavyo viliandikwa na watu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu vikakusanywa na Kanisa kwa jina la âBibliaâ, yaani âVitabuâ.
Hao âwanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifuâ (2Pet 1:21).
Roho Mtakatifu ni upendo wa Mungu, nafsi ya tatu ya Utatu Mtakatifu, mwenye Umungu mmoja na Baba na Mwana.
âPendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisiâ (Rom 5:5).
Ametumwa kwetu atufanyie kazi pasipo kuonekana.
âUpepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Rohoâ (Yoh 3:8).
âWote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Munguâ (Rom 8:14).
Ndiyo, kazi zote za Roho Mtakatifu zinahusiana na Yesu na kulenga hasa kuandaa watu wampokee, wamfuate na kumshuhudia katika umoja wa kundi lake, Kanisa.
âAjapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia. Nanyi pia mnashuhudiaâ (Yoh 15:26-27).
Kumpokea Roho Mtakatifu maana yake ni kuja kuongozwa naye badala ya kutawaliwa na shetani.
âKwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanae mioyoni mwetu, aliaye, âAba!â yaani, âBaba!â Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu. Lakini wakati ule, kwa kuwa hamkumjua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si miungu⌠Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Rohoâ (Gal 4:6-8; 5:25).
âIkiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wakeâ (Rom 8:9).
Tukimpokea Roho Mtakatifu papo hapo tunapokea pia adili kuu la upendo:
âPendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisiâ (Rom 5:5).
Tena tunapokea vipaji vyake ambavyo Yesu alikuwa navyo kikamilifu.
âRoho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana. Na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwanaâ (Isa 11:2-3).
Mambo hayo, tofauti na karama, ni ya lazima kwa yeyote apate wokovu wa milele.
Hapana, hatuwezi kuhakikisha neema ya utakaso kwa kuwa ni tukio ambalo linapita maumbile na kufanyika rohoni, hivyo halifikiwi na hisi zetu. Pengine Mungu anatokeza dalili fulani za badiliko hilo kama vile furaha ya ndani au karama ya nje, lakini hizo hazihitajiki wala hazitoshi kuthibitishia mtu amepata neema hiyo.
âWengi wataniambia siku ile: Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri: Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovuâ (Math 7:22-23).
âNijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kituâ (1Kor 13:1-3).
Hapana, karama si zile za kushangaza tu, tena zile muhimu zaidi si hizo, bali zile zinazojenga zaidi Kanisa, kama zile za uongozi:
âMungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lughaâ (1Kor 12:28).
âBasi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema tuliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia, kwa bidii; mwenye kurehemu, kwa furahaâ (Rom 12:6-8).
Karama nyingine muhimu zinatuwezesha kuishi kwa useja kama Yesu na Paulo, au kwa ndoa:
âNipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo; walakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi. Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane; ni heri wakae kama mimi nilivyoâ (1Kor 7:7-8).
âSi wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwaâ (Math 19:11).
Tunavyoona katika historia ya watawa, mara nyingi karama ya useja inaendana na nyingine katika maisha ya sala, ya kijumuia na ya kitume. Hivyo Filipo âalikuwa na binti wanne, mabikira, waliokuwa wakitabiriâ (Mdo 21:9).
Karama zinagawiwa na Roho Mtakatifu jinsi anavyotaka, si kwa sifa au faida ya binafsi, bali kwa ustawi wa taifa la Mungu.
âKazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye⌠Je, wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza? Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri?⌠Kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa⌠Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amaniâ (1Kor 12:11,29-30; 14:12,33). Kwa ajili hiyo mitume walipambanua na kuratibu karama katika ibada na katika maisha ya jumuia zisije zikavuruga Kanisa.
Karama za kushangaza zina hatari mbalimbali, hasa zikitiwa maanani mno. Hapo ni rahisi zilete majivuno, kijicho na mafarakano.
âIkiwa kwenu kuna husuda na fitina, je, si watu wa tabia ya mwili ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?⌠Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata utajiri, mmemiliki pasipo sisi. Naam, laiti mngemiliki⌠Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asiangukeâ (1Kor 3:3; 4:8; 10:12).
Katika mambo yasiyothibitika ni rahisi kudanganyika kuwa yametoka kwa Mungu, kumbe sivyo. Kisha kudanganyika ni vigumu kuachana nayo hata yakiwa na madhara kwa mhusika au kwa Kanisa.
âWapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea dunianiâ (1Yoh 4:1).
Tunda la kuongozwa na Roho Mtakatifu ni umoja wa Kanisa unaotokana na ustawi wa upendo na vipaji ndani ya waamini.
âWote walijaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri. Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho mojaâ (Mdo 4:31-32).
âTunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheriaâ (Gal 5:22-23).
âLakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli. Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani. Maana hapo palipo wivu na ugomvi, ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya. Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi; tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafikiâ (Yak 3:14-17).
Madhehebu yanapozidi kufarakana ni lazima tujiulize kama kweli ni kazi ya Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu anatusaidia tusali kama Yesu, akiwa mlezi wa ndani na kutumia vipaji vyake saba.
âMungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, âAba!â yaani, âBaba!ââ (Gal 4:6).
âRoho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo; lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa⌠huwaombea watakatifu kama apendavyo Munguâ (Rom 8:26-27).
Ndiyo sababu Kanisa linatuhimiza tumtamani na kumualika kila mara, âNjoo, Roho Mtakatifu!â yaani kumuomba Baba kwa njia ya Mwana amtume zaidi na zaidi ndani mwetu.
Roho Mtakatifu anaweza kutufikisha hadi muungano wa dhati na Mungu.
âYeye awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake, katika utu wa ndani. Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Munguâ (Ef 3:16-19).
âHuyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yoteâ (Yoh 16:13).
Safari hiyo inategemea sana sala isiyoishia katika maneno bali inalenga kupenya mafumbo kwa imani na upendo.
Ni Sakramenti yenye kumpa Mkristu Roho Mtakatifu na ukamilifu wa mapaji yake saba, kumfanya mkristu mkamilifu na kumwandika Askari hodari wa Yesu Kristo Mpaka Kufa
Roho Mtakatifu ni nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu, ni Mungu Halisi sawa na Mungu Baba na Mwana. (Yoh 14:16-17,26)
Maana yake ni kupata nguvu ya Kuhubiri Injili, Neno la Mungu linalopenya kwenye Moyo Kama Moto.
Roho Mtakatifu anawafanyia Waamini haya.
1. Anawatakasa
2. Anawaangaza na kuwavuta ili waende kwenye uzima wa milele
Roho Mtakatifu anatutakasa kwa njia ya Sakramenti, Visakramenti, Fadhila za Kimungu na vipaji vyake. (Yoh 16:8)
Roho Mtakatifu anatenda kazi zake kwa njia hizi;
1. Anatuangaza kwa Mwanga wake tupate kuelewa mafundisho ya dini
2. Anatupatia neema za msaada za kutusaidia kutunza utakatifu wetu
3. Anatuvuta kwa mapendo yake tuzitumie Neema na kufika kwenye uzima wa milele.
4. Anatufariji katika shida zote. Ndio maana Roho Mtakatifu huitwa pia Mfariji
Inaitwa Sakramenti ya Kipaimara kwa sababu inaimarisha na kukamilisha neema ya Ubatizo
Anakuja kufanya yafuatayo;
1. Anakuja kutuongezea Neema ya Utakaso
2. Anatuletea pia ukamilifu wa mapaji yake saba na msaada wa kuungama imani yetu mbele za watu
Mapaji saba ya Roho Mtakatifu ni msaada wake wa kuimarisha na kuzoesha akili na moyo wetu kwa mambo ya utumishi wa Mungu
Mapaji Hayo ni;
1. Hekima
2. Akili
3. Shauuri
4. Nguvu
5. Elimu
6. Ibada
7. Uchaji wa Mungu (Isaya 11:2)
Ni upendaji wa Mambo ya Mungu na Machukio ya Mambo ya Dunia
Ni mwangaza wa Roho Mtakatifu wa Kutusaidia tumjue zaidi Mungu na Ukamilifu wake na kuwa na Hakika kwamba Mungu peke yake aweza kutuliza roho zetu
Ni utaratibu wa Kuchagua Siku zote mambo yenye kufaa kwa sifs ya Mungu na kwa Wokovu wetu
Ni moyo wa kushika sana Amri za Mungu na mambo ya utumishi wake tusiogope watu, matukano, mateso wala kufa. (Rum 8:38-39)
Ni maarifa ya kutambua werevu na udanganyifu wa shetani; anaposhawishi mwenyewe au kwa kutumia vitu au watu. (1Pet 5:8-9)
Ni roho ya kupenda utumishi wa Mungu na yote yale yenye kumpa Mungu sifa na Heshima
Ni hofu ya kumchukiza Mungu kwa Dhambi kama vile mtoto mwema aogopavyo kumchukiza mzazi au mlezi wake.
Roho Mtakatifu hutajwa katika fungu la tatu la Matendo ya Utukufu tusemapo; Aliyepeleka Roho Mtakatatifu. (Mdo 2:1-4)
Kabla ya kupaa mbinguni Yesu aliwaahidia Mitume kuwapelekea Roho Mtakatifu; ndiye nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu. (Yoh 16:7)
Ndiyo, kwani twataka kwake maonyo na msaada. Tusipokuwa na neema yake hatuwezi kutenda jambo jema la kufaa kutuokoa. (Yoh 16:13)
Matunda ya Roho Mtakatifu ni;
1. Upendo
2. Furaha
3. Amani
4. Uaminifu
5. Uvumilivu
6. Utu wema
7. Fadhila
8. Upole
9. Kiasi
(Wagalatia 5:22, 23)
Biblia ni mkusanyiko wa vitabu mbalimbali vinavyohusu kazi ya Mungu ya kuwakomboa mwanadamu kuanzia enzi za Mababu na manabii Wa Waisraeli, Enzi za Yesu na za Mitume wa Yesu.
Biblia iliundwa kwa kukusanya vitabu vya dini vya wakristo hapo awali na kuunda kitabu kimoja. Kwa maana hii, Biblia ni vitabu teule vya dini vilivyoonekana vinafaa kutumika kwa waumini Wakristo ili kusaidia Imani yao. Hivyo basi, kama Biblia ni vitabu teule tuu vipo vitabu vingine vya dini ambavyo havikuwekwa Kwenye Biblia.
Wakristo wa kwanza walichagua vitabu kadhaa na kuviweka pamoja na kisha kuvita Biblia. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu muhimu tuu vya dini mpaka kufikia Enzi za Mitume.
Hapana, Biblia sio kitabu pekee cha neno la Mungu isipokua Biblia ni kitabu kilichoidhinishwa rasmi kutumika Kama kitabu kikuu cha Wakristo. Hii ni kwa sababu Biblia imeundwa na vitabu muhimu tuu vilivyochaguliwa na wakristo wa kwanza vilivyoonekana vinafaa kwa kufundishia, Ibada na kukuza Imani. Kwa hiyo basi vipo vitabu vingine ambavyo haikuwekwa Kwenye Biblia ambavyo ni Maneno ya Mungu.
Hii ndiyo sababu kwa nini Wakatoliki wana vitabu vingi kuliko madhehebu Mengine. Yaani sababu ni kwamba madhehebu Mengine walivitoa vitabu vingine vilivyounda Biblia. Na Wakatoliki waliweka vitabu vingine vya dini Kwenye Biblia walivyoona vinafaa pia kutumika.
Nje ya Biblia kuna Neno la Mungu na Maandiko Matakatifu. Hii Inamaanisha kuwa Biblia sio kitabu pekee cha neno la Mungu. Zipo nyaraka na Vipo vitabu vingine vingi ambavyo viliandikwa na Manabii na Mitume ambavyo havikuwekwa kwenye Biblia lakini ni mafundisho ya Mungu. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vikuu vya Mungu.
Kumbuka kuwa sio nyaraka zote za Mitume ziliandikwa Kwenye Biblia. Vile vile manabii walikuwa ni wengi kuliko waliowekwa Kwenye Biblia.
Hapana, Biblia sio mafundisho pekee ya Mungu. Hii ni kwa sababu sio mambo yote aliyofanya na kusema Mungu yaliandikwa na vilevile Mitume hawakua watu wa Mwisho kupokea Roho mtakatifu na kupokea neno la Mungu.
Biblia inatuthibitishia kuwa haijakamilika tunaposoma (Yohane 21:25)
Biblia inatuambia hiviâŚâKuna mambo Mengine mengi aliyofanya Yesu, ambayo Kama yangeandikwa yote, moja baada ya jingine, nadhani hata ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa.ââŚKwa mstari huu Biblia inatuthibitishia kuwa haikuandikwa vitu vyote.
Biblia sio mwisho wa Maandiko ya Kimungu.
Biblia ni sehemu ya maneno ya Mungu mpaka miaka ya Mitume
Hata sasa Mungu anafanya kazi na watu wake kupitia Roho Mtakatifu na kwa kwa sababu hii Biblia sio mwisho wa kazi ya Mungu ya kusema na watu wake.
Mungu yu hai na anafanya kazi na watu wake mpaka sasa kwa kutumia vinywa vya watu Kama aliyofanya hapo awali.
Hata maneno unayohubiriwa sasa yanaweza kuwa ni kutoka kwa Mungu kwa maana hata waandishi wa Biblia walitumiwa na Mungu Kama wahubiri wa sasa. Mungu ni yule yule, Roho Mtakatifu ni yuleyule na Neno ni lile lile.
Kwa hiyo Biblia ni maneno yaliyochaguliwa mpaka enzi za Mitume. Vitabu vilivyofwata Baada ya Mitume japokuwa viliandikwa kwa Roho Mtakatifu havikuwekwa Kwenye Biblia.
Kanisa katoliki linatumia mapokeo na Makala za watakatifu kwa Imani kuwa Mungu yule yule aliyefanya kazi tangu zamani anafanya kazi na watu wake mpaka sasa na hivyo Maandiko ya watu wa Mungu yanafaa kutumika kama yalivyotumika ya watu wa kale.
Yesu alituambia hivi katika (Yohane 16:12-15)..âNinayo mengi ya kuwaambieni Ila kwa sasa hamuwezi kuyastahimili. Lakini atakapokuja huyo Roho wa Ukweli atawaongoza kwenye ukweli wote. Maana hatasema kwa Mamlaka yake mwenyewe bali atasema atakayoyasikia na kuwajulisheni yatakayokuja. Yeye atanitukuza Mimi kwa kuwa atawajulisheni Yale atakayoyapata kutoka kwangu ââŚ
Sasa basi,kama Roho Mtakatifu ni yuleyule na kazi zake ni Zile Zile za tangu Mitume, kwa nini hatukubali kuwa Anafanya kazi mpaka sasa kupitia watu wa Mungu? Kwa nini tunakataa mafundisho yao? Kwa nini tunashindwa kuelewa kuwa Biblia haikuwa mwisho wa Neno la Mungu? Kwa nini tunakana Mapokeo ya Watakatifu? Kwa nini hatuwaamini watumishi wake wa sasa?
Comments
Please log in or register to leave a comment or reply.
Patrick Kidata (Guest) on May 23, 2019
Sifa kwa Bwana!
Raphael Okoth (Guest) on April 13, 2019
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
Mary Mrope (Guest) on March 8, 2019
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
David Musyoka (Guest) on January 16, 2019
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
Stephen Mushi (Guest) on November 30, 2018
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
Edith Cherotich (Guest) on October 28, 2018
Imani inaweza kusogeza milima
Stephen Kikwete (Guest) on August 18, 2018
Mungu ni mwema, wakati wote!
Frank Sokoine (Guest) on August 9, 2018
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
James Mduma (Guest) on August 4, 2018
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
Nora Kidata (Guest) on July 13, 2018
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
Joseph Njoroge (Guest) on May 17, 2018
Rehema hushinda hukumu
Alex Nyamweya (Guest) on May 8, 2018
Dumu katika Bwana.
Nancy Akumu (Guest) on May 3, 2018
Tumaini ni nanga ya roho
Tabitha Okumu (Guest) on April 7, 2018
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
Emily Chepngeno (Guest) on April 5, 2018
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
Mary Kendi (Guest) on March 14, 2018
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
Nancy Akumu (Guest) on March 9, 2018
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
Susan Wangari (Guest) on March 6, 2018
Neema na amani iwe nawe.
Violet Mumo (Guest) on February 8, 2018
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
Ann Awino (Guest) on December 7, 2017
Rehema zake hudumu milele
Joseph Kitine (Guest) on November 8, 2017
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
Vincent Mwangangi (Guest) on October 24, 2017
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
George Wanjala (Guest) on October 11, 2017
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
Martin Otieno (Guest) on July 27, 2017
Rehema zake hudumu milele
Paul Ndomba (Guest) on March 14, 2017
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Edwin Ndambuki (Guest) on February 23, 2017
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
Lucy Wangui (Guest) on November 23, 2016
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
Diana Mumbua (Guest) on September 3, 2016
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
Victor Malima (Guest) on April 7, 2016
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
Francis Mrope (Guest) on March 21, 2016
Tumaini ni nanga ya roho
Thomas Mwakalindile (Guest) on March 2, 2016
Imani inaweza kusogeza milima
Alice Wanjiru (Guest) on February 19, 2016
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
Jackson Makori (Guest) on January 2, 2016
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
Nancy Komba (Guest) on December 25, 2015
Nguvu hutoka kwa Bwana
Robert Ndunguru (Guest) on November 20, 2015
Wakati wa Mungu ni kamilifu
Edward Chepkoech (Guest) on October 6, 2015
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
Anna Sumari (Guest) on October 1, 2015
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
Dorothy Mwakalindile (Guest) on September 19, 2015
Endelea kuwa na imani!
Anna Sumari (Guest) on August 20, 2015
Dumu katika Bwana.
Kevin Maina (Guest) on June 27, 2015
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi