Utaratibu wa Mkristo Mkatoliki Kanisani

✍️ DIN - Melkisedeck Leon ShineπŸ“… 2020-02-24 13:39:00πŸ’¬ 50 comments⏱️ ~2 min read
πŸ“„ PDF
Ninapoingia kanisani nachovya maji ya baraka na kusema;
"Unitakase Ee Bwana mimi na uovu wangu wote, ili nipate kustahili kushiriki ibada takatifu' Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu" Amina!
Ninapiga goti huku nikisema
"Mungu wangu na Bwana wangu"
πŸ™‹πŸ½Nikiinuka nasema
"Nitakusifu na kukuabudu katika Ekaristi takatifu"
πŸ™‹πŸ½Naenda mpaka kwenye bench, napiga magoti au nakaa nikiwa mimeinamisha kichwa (kama mabenchi yameisha nabaki nimejisimamia) huku nikitoa nia yangu ya kusali misa siku hiyo, mfano
"Ee Mungu, ninaungana nawe na jeshi lote la mbinguni, pamoja na Mama Bikira Maria, nikiwa na nia ya kumwombea mama yangu ambaye ni mgonjwa, jirani yangu ambaye mpaka sasa hatuelewani na pia familia yetu ambayo haina amani, Mungu kupitia misa hii rejesha hali ya mama yangu, rejesha uelewano na jirani yangu, na pia rejesha amani ya familia yetu pamoja na familia zote ambazo hazina amani"
πŸ™‹πŸ½Ninaendelea na misa na Kushiriki litrujia kikamilifu
πŸ™‹πŸ½Wakati wa komunyo nikikumbuka kuwa nina dhambi kubwa huwa nakominika kwa sala ya tamaa wala siendi mbele, huwa najikalia tu kwenye bench naangalia wenye moyo safi wanaenda mbele kumpokea Yesu (Kweli huwa najisikia wivu sana, itanibidi katikati ya wiki nifanye kitubio ili nisikae tena)"
πŸ™‹πŸ½Mwisho wakati wa kuondoka nachovya maji ya baraka nikisema
"Unilinde Ee Mwenyezi Mungu, nikapate kuwa mfano katika jamii yangu, na nikushuhudie katika matendo yangu"
(Hapo nachovya maji ya baraka na kufanya ishara ya msalaba) "Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, amina"
Usiku mwema wapendwa. Malaika awalinde
πŸ’¬

Discussion

Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.

50 comment(s)
πŸ” Login required to comment or reply

You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.

Log in to participate
T
Thomas Mtaki2016-09-29 07:24:31
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
B
Betty Kimaro2016-07-06 20:19:16
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
A
Alice Wanjiru2016-06-27 19:56:02
Rehema hushinda hukumu
H
Hellen Nduta2016-04-14 08:05:03
Endelea kuwa na imani!
T
Thomas Mwakalindile2016-04-08 02:44:37
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
N
Nancy Akumu2015-11-13 09:02:36
Katika imani, yote yanawezekana
A
Alice Wanjiru2015-10-25 08:52:14
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
G
George Wanjala2015-06-09 07:21:30
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
B
Benjamin Masanja2015-05-20 18:29:22
Mungu ni mwema, wakati wote!
V
Victor Sokoine2015-05-05 08:04:33
Tumaini ni nanga ya roho