Maswali na Majibu kuhusu dhamira

✍️ DIN - Melkisedeck Leon ShineπŸ“… 2020-02-16 09:01:00πŸ’¬ 50 comments⏱️ ~2 min read
πŸ“„ PDF
Dhamiri adilifu ni nini?

Dhamiri adilifu, iliyo ndani kabisa mwa mtu, ni uamuzi wa akili ambao kwa wakati wake unamuagiza mtu atende mema na kukwepa maovu


Katika hukumu zake dhamira ifuate nini?

Katika hukumu zake dhamira ifuate daima Injili, Amri za Mungu na za Kanisa na wajibu zetu.


Twajenga na kutunza dhamira zetu namna gani?

Twajenga na kutunza dhamira zetu kwa;-

1. Kufuata sauti ya Roho Mtakatifu 2. Kuzingatia mafundisho ya dini 3. Kuzingatia mila na desturi njema tulizopata katika malezi. 4 Kufuata mifano na tabia njema ya wenzetu na ya Watakatifu


Hadhi ya nafsi ya mtu inadai nini kuhusu dhamiri adilifu?

Hadhi ya nafsi ya mtu inadai unyofu wa dhamiri adilifu, yaani upande wa akili na sheria ya Mungu


Dhamiri adilifu inaundwa namna gani iwe nyofu na ya kweli?

Dhamiri nyofu inayosema kweli inaundwa kwa;

1. Malezi 2. Upokeaji wa neno la Mungu 3. Upokeaji wa Mafundisho ya Kanisa 4. Sala 5. Utafiti wa dhamiri


Dhamiri adilifu inatengenezwa na kusaidiwa na nini?

Dhamiri adilifu inatengenezwa na vipaji vya Roho Mtakatifu na kusaidiwa na mashauri ya watu wenye busara.


Dhamiri inatakiwa kufuata daima masharti gani?

Dhamira inatakiwa kufuata daima masharti yafuatayo

1. Hairuhusiwi kutenda maovu kusudi yapatikane mema 2. Yoyote muyatakayo mtendewe na watu, ninyi watendeeni vivyo hivyo. (Mt 7:12) 3. Upendo hufuata daima nia na heshima kwa jirani na kwa dhamira yake

πŸ’¬

Discussion

Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.

50 comment(s)
πŸ” Login required to comment or reply

You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.

Log in to participate
G
Grace Wairimu2020-10-28 16:23:39
Mungu akubariki!
D
Diana Mallya2020-05-22 07:59:18
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
G
Grace Njuguna2020-03-26 09:14:06
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
J
John Malisa2019-10-17 03:49:58
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
K
Kenneth Murithi2019-08-13 14:15:55
Endelea kuwa na imani!
F
Francis Mrope2019-06-16 10:58:11
Rehema zake hudumu milele
M
Mercy Atieno2019-05-15 02:20:43
Mwamini Bwana; anajua njia
R
Rose Waithera2019-04-20 23:18:33
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
L
Lucy Wangui2019-02-20 13:35:44
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
D
David Musyoka2018-12-27 15:45:34
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
G
Grace Mligo2018-07-08 04:45:02
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
R
Ruth Mtangi2018-06-08 15:00:08
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
J
John Lissu2017-12-08 07:45:11
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
T
Thomas Mwakalindile2017-12-04 19:05:37
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
A
Agnes Lowassa2017-08-30 08:18:13
Kwa Mungu, yote yanawezekana
A
Ann Awino2017-08-17 16:14:14
Rehema hushinda hukumu
S
Samuel Were2017-05-03 21:32:58
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
J
Joseph Kiwanga2017-01-22 13:12:49
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
S
Stephen Mushi2016-12-10 11:23:27
Neema na amani iwe nawe.
F
Francis Njeru2016-12-09 12:24:14
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita