Daima Tunakumbushwa kuungama dhambi zetu hata kama ni ndogo kiasi gani

✍️ DIN - Melkisedeck Leon ShineπŸ“… 2016-12-20 06:29:00πŸ’¬ 50 comments⏱️ ~2 min read
πŸ“„ PDF

Kulikuwa na vijana wawili walioamua kwenda kwa padri kumwelezea shida zao.
Basi walipofika kwa yule padre, wakamwambia padre, " samahani padre tuko hapa mbele yako kwa kuwa tumejisikia kuwa ni wadhambi ha hivyo tunahitaji kuungama.

Basi wakwanza akamwambia padre, " Mimi dhambi zangu ni kubwa sana hata ninaona aibu kuziungama", wa pili akamwambia padre, " sahamani padre mimi nimetenda dhambi ila siyo kubwa sana kama za mwenzangu, bali ni dhambi ndogondogo." Baada ya kusikia hayo padre aliwaambia basi kila mmoja aende akaokote mawe kadiri ya dhambi alizozitenda na akamletee. Hao vijana walienda kuokota mawe kadiri ya dhambi za kila mmoja wao. Mmoja wao alileta jiwe moja kubwa ambalo alikuja akilivilingisha hadi pale alipokuwepo padre, na mwingine alileta mawe madogomadogo mengi kwenye mfuko. Baada ya padre kuone kuwa walifanya alivyowaagiza, basi aliwaambia kuwa kila mmoja arudishe mawe yake sehemu ile ile alipoyaokota. Yule aliyebeba jiwe kubwa ilikuwa rahisi kujua alipolitoa hivyo alilivilingisha mara moja na kulirudisha mahali pake, wakati yule aliyekuwa na mawe madogomadogo alishindwa kukumbuka mahali alipoyatoa, hivyo akaishia kuhangaika na kumwambia padre kuwa hawezi kumbuka mahali alipotoa kila jiwe, na kwake ni vigumu.

Baada ya hayo padre aliwaambia wote kuwa yule mwenye dhambi kubwa daima ni rahisi kuiungama maana huwa inashika nafasi kubwa katika nafsi yake na inamfanya asiwe na amani daima, kwa hivyo ni rahisi kukumbuka kuiungama dhambi yake, vilevile padre akamgeukia yule mwingine aliyebeba mfuko wa mawe madogomadogo na akamwambia kuwa, jinsi ulivyoshindwa kurudisha hayo mawe katika nafasi yake kila moja, ndivyo ilivyo kwa dhambi ndogondogo ulizotenda. Dhambi zionekanazo kuwa ni ndogo zaweza sahulika na kukufanya utende dhambi nyingine ya kutokukumbuka wajibu wako wa kuungama ukidhani kuwa hujatenda dhambi.

Daima tunakumbushwa kuungama dhambi zetu hata kama ni ndogo au hata kama tumesahau, kwa maana kuna zile dhambi ambazo ni nyepesi na rahisi kusahulika na hivyo kutufanya daima tujihisi kuwa sisi hatuna haja ya kuungama.

πŸ’¬

Discussion

Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.

50 comment(s)
πŸ” Login required to comment or reply

You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.

Log in to participate
R
Rose Waithera2020-10-02 18:33:12
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
M
Margaret Mahiga2020-07-31 01:37:30
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
E
Edward Lowassa2020-04-02 04:02:24
Mungu akubariki!
J
Janet Sumari2020-03-12 11:10:14
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
L
Lucy Mahiga2020-01-31 08:19:09
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
T
Tabitha Okumu2019-12-14 03:06:46
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
M
Mary Kendi2019-12-13 19:40:02
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
C
Charles Mrope2019-09-22 17:19:10
Sifa kwa Bwana!
V
Victor Sokoine2019-06-11 02:37:55
Rehema zake hudumu milele
E
Edith Cherotich2019-04-03 12:29:37
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
N
Nancy Komba2018-06-24 16:26:47
Tembea kwa imani, si kwa kuona
C
Charles Wafula2018-06-20 17:29:50
Tumaini ni nanga ya roho
D
David Sokoine2018-06-01 19:47:55
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
N
Nancy Komba2018-02-23 03:51:21
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
I
Isaac Kiptoo2017-10-10 04:56:43
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
D
Dorothy Mwakalindile2017-09-18 12:23:24
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
E
Esther Nyambura2017-09-13 08:24:28
Baraka kwako na familia yako.
M
Monica Lissu2017-04-12 13:36:53
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
M
Mariam Kawawa2017-02-26 12:02:30
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
J
Joseph Kiwanga2017-02-01 08:44:21
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine