MAANA YA SALA KWA MKRISTO

โœ๏ธ DIN - Melkisedeck Leon Shine๐Ÿ“… 2015-02-02 02:14:00๐Ÿ’ฌ 50 commentsโฑ๏ธ ~2 min read
๐Ÿ“„ PDF
Sala ni kuinua mioyo yetu kwa Mungu na kuongea nae. Watu wote wanapaswa kusali, wema na wabaya. Inatupasa kusali kila siku bila kukata tama kwa ibada, kwa matumaini na kwa saburi. Kama mfano Yesu Alitufundisha sala ya Baba yetu.
Yatupasa kuwaombea wengine, watu wote wenye shida wakosefu na hata maadui zetu, vilevile tumtolee Mungu shukrani kila wakati na hasa kwa kuadhimisha Ekaristi Takatifu.
Masifu ni sala au wimbo unaomsifu na kumtambua Mungu kuwa Mungu.
Sababu za kusali
1. Kumuabudu Mungu
2. Kumshukuru Mungu
3. Kuomba Neema na Baraka kwa ajili yetu na wenzetu
4. Kuomba msamaha
Namna za sala
1. Sala ya sauti :ย Sala asaliyo mtu au kikundi kwa kutumia maneno
2. Sala ya fikra :ย Sala asaliyo mtu akiwa peke yake au na wengine kimya kimya akimuwaza Mungu.
3. Sala ya Taamuli:ย Kumtazama tuu Mungu kwa upendo Mkubwa Moyoni.
Nyakati zote zinafaa kwa sala hasa
1. Asubuhi na jioni
2. Kabla na baada ya kula
3. Kila dominika
4. Sikukuu za amri
5. Kabla na baada ya kazi
6. Katika kishawishi
Vyanzo vya sala za Kikristo
1. Neno la Mungu
2. Liturujia ya Kanisa
3. Fadhila za Kimungu
4. Matukio ya kila siku
Aidha Roho Mtakatifu ndiye mlezi wa ndani wa sala ya Kikristo akitufundisha kusali na kusali ndani mwetu.
Sala Muhimu kwa Mkristo
Sala kubwa ya kanisa ni Misa Takatifu na sala Bora kwa Bikira Maria ni Rozari Takatifu.
Sala nyingine Muhimu kwa Mkristu ni:
1. Baraka ya Sakramenti kuu
2. Andamo la Ekaristi
3. Litania Takatifu
4. Njia ya Msalaba
5. Rozari takatifu
6. Novena
Mtu anaweza kusali popote lakini kanisani ndio mahali rasmi pa sala, Aidha familia ni shule ya kwanza ya sala ambapo mtu hujifunza na kujizoesha kusali anapokua katika familia.
Changamoto na majaribu wakati wa kusali
1. Mtawanyiko wa mawazo
2. Ukavu wa Moyo
3. Uvivu na uregevu
Faida ya Sala
1. Zinaleta neema nyingi
2. Zinatuimarisha ili tushinde vishawishi na dhambi
3. Zinatuunganisha na Mungu
4. Zinatudumisha katika kutenda mema
Nenoย Aminaย katika sala linamaanaย โ€˜Na iwe hivyoโ€™.ย Na nenoย Aeluyaย maana yake niย Msifuni Mungu.
๐Ÿ’ฌ

Discussion

Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.

50 comment(s)
๐Ÿ” Login required to comment or reply

You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.

Log in to participate
S
Samuel Omondi2024-05-13 12:08:09
Imani inaweza kusogeza milima
B
Betty Kimaro2023-11-11 02:40:05
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
C
Christopher Oloo2023-11-08 04:52:08
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
M
Moses Mwita2023-08-27 03:08:36
Kwa Mungu, yote yanawezekana
P
Peter Mbise2023-08-02 05:32:30
Mwamini Bwana; anajua njia
J
Janet Mwikali2023-07-11 23:43:57
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
G
Grace Njuguna2023-03-12 12:29:19
Nguvu hutoka kwa Bwana
P
Paul Ndomba2023-02-05 10:50:26
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
T
Tabitha Okumu2022-05-24 00:29:16
Neema ya Mungu inatosha kwako
H
Hellen Nduta2022-05-19 23:35:25
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
A
Anna Mahiga2022-04-07 00:47:21
Dumu katika Bwana.
J
Josephine Nduta2021-09-29 20:47:40
Baraka kwako na familia yako.
F
Frank Macha2021-08-02 20:20:11
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
D
Diana Mumbua2021-07-30 01:24:41
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
J
Jane Malecela2021-07-15 06:23:59
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
J
James Mduma2021-06-08 16:50:54
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
E
Esther Nyambura2021-05-28 04:31:42
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
I
Isaac Kiptoo2021-04-11 23:17:37
Endelea kuwa na imani!
D
Dorothy Mwakalindile2020-12-27 00:19:55
Sifa kwa Bwana!
C
Chris Okello2020-12-10 20:10:20
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika