Mungu ndiye Muumba wa vitu vyote, katika mbingu na nchi, Mkubwa wa Ulimwengu mwenye kuwtunza watu wema na kuwaadhibu watu wabaya. (Mt: 6:8-9, Yoh 20: 17)
Sifa za Mungu
Mungu ni Muumba wa vitu vyote
Mungu ni Muumba wa vyote maana yake amefanya vitu vyote kwa kutaka tuu pasipokutumia kitu chochote (Yoh. 1:3)
Mungu ni Roho
Mungu ni Roho kamili na ukamilifu wake hauna mpaka na haonekani wala hashikiki. (Yoh. 4:24, Kut 3:13-15, Zb 144:3, Lk: 24:39)
Mungu ni muweza wa yote
Mungu anaweza kufanya kila anachokitaka. (Zab. 135:6)
Mungu ni wa Milele
Hii ina maana Mungu hana mwanzo wala mwisho, amekuwepo kabla ya nyakati, yupo na atakuwepo baada ya nyakati. Yeye ndiye anazifanya nyakati, Yupo daima. (1 Tim, 1:17)
Mungu ni mwema
Maana yake anavipenda na kuvitunza viumbe vyake hasa wanadamu na anavitakia mema tuu (Zab: 25:8-10)
Mungu ni mwenye haki
Kila mtu hupata kwa Mungu Haki yake kadiri na anavyostahili.
Mungu aenea pote
Hii ina maana yupo kila mahali Mbinguni na Duniani, Hakuna mahalia asipokuwepo. (Zab: 139:7-12).
Mungu anajua kila kitu
Mungu anajua yote, ya sasa, ya zamani na ya wakati ujao hata mawazo yetu
Mungu ni mwenye huruma
Anawasamehe watu dhambi zao wakitubu
Mungu ni mwenye subira
Mungu anakawia kuwaadhibu wakosefu maana anataka kuwapa nafasi ya kuongoka. (Eze; 33:11, Zb: 102: 1-5)
Aidha Mungu yupo Mmoja tuu ambayae kwake kuna nafsi Tatu ambazo ni sawa, Baba ni Mungu, Mwana ni Mungu na Roho Mtakatifu ni Mungu. Hli ndilo linaitwa Fumbo la Utatu Mtakatifu. (Lk. 3:21-22)
Mungu ndiye Muumba wa vitu vyote, katika mbingu na nchi, Mkubwa wa Ulimwengu mwenye kuwtunza watu wema na kuwaadhibu watu wabaya. (Mt: 6:8-9, Yoh 20: 17)Sifa za MunguMungu ni Muumba wa vitu vyoteMungu ni Muumba wa vyote maana yake amefanya vitu vyote kwa kutaka tuu pasipokutumia kitu chochote (Yoh. 1:3)Mungu ni RohoMungu ni Roho kamili na ukamilifu wake hauna mpaka na haonekani wala hashikiki. (Yoh. 4:24, Kut 3:13-15, Zb 144:3, Lk: 24:39)Mungu ni muweza wa yoteMungu anaweza kufanya kila anachokitaka. (Zab. 135:6)Mungu ni wa MileleHii ina maana Mungu hana mwanzo wala mwisho, amekuwepo kabla ya nyakati, yupo na atakuwepo baada ya nyakati. Yeye ndiye anazifanya nyakati, Yupo daima. (1 Tim, 1:17)Mungu ni mwemaMaana yake anavipenda na kuvitunza viumbe vyake hasa wanadamu na anavitakia mema tuu (Zab: 25:8-10)Mungu ni mwenye hakiKila mtu hupata kwa Mungu Haki yake kadiri na anavyostahili.Mungu aenea poteHii ina maana yupo kila mahali Mbinguni na Duniani, Hakuna mahalia asipokuwepo. (Zab: 139:7-12).Mungu anajua kila kituMungu anajua yote, ya sasa, ya zamani na ya wakati ujao hata mawazo yetuMungu ni mwenye hurumaAnawasamehe watu dhambi zao wakitubuMungu ni mwenye subiraMungu anakawia kuwaadhibu wakosefu maana anataka kuwapa nafasi ya kuongoka. (Eze; 33:11, Zb: 102: 1-5)Aidha Mungu yupo Mmoja tuu ambayae kwake kuna nafsi Tatu ambazo ni sawa, Baba ni Mungu, Mwana ni Mungu na Roho Mtakatifu ni Mungu. Hli ndilo linaitwa Fumbo la Utatu Mtakatifu. (Lk. 3:21-22)
Discussion
Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.
You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.
Log in to participate