Log in to access your menu with tools for managing ๐ tasks, ๐ฅ clients, ๐ฐ finances, ๐ learning, ๐ personal growth, and ๐ spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Usiku wa leo uwe ni wenye faraja kwako, utawaliwe na usingizi wa mahaba kwenye kope zako, naomba ujenge taswira yangu katika mawazo yako, Usisahau kuniota sweet wangu. USIKU MWEMA
Updated at: 2024-05-25 15:37:46 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Usiku wa leo uwe ni wenye faraja kwako, utawaliwe na usingizi wa mahaba kwenye kope zako, naomba ujenge taswira yangu katika mawazo yako, Usisahau kuniota sweet wangu. USIKU MWEMA
Updated at: 2024-05-25 15:36:18 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Dah! Safari yetu ilikuwa ngumu kweli ila hatimaye tumefika japo ni usiku sana hebu tupige hodi tusije kabwa na vibaka hapa nje. Hodiiiiii, Hodiiiii, Tunaomba tufungulie Mlango,, sisi tunaitwa FURAHA, AMANI na UPENDO. Tumebeba HEKIMA, BUSARA na MAFANIKIO. Tulikuwa wengi HURUMA na UPOLE wanakuja nyuma. CHUKI na WIVU hawana nauli. TABU ni mahututi. SHIDA yuko jela. MATATIZO amepigwa shoti ya umeme. MIKOSI amefariki njiani. LAANA ameliwa na mamba. UVIVU ameungua na maji ya moto hajiwezi. Tutakuwa nawe daima maana tumefika kwa NEEMA . Mungu akulinde na mabaya yote katika dunia hii. ucku mwema.
Meseji ya kumwambia mpenzi wako kuwa umezama kwake
Updated at: 2024-05-25 15:23:20 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
tazama, nimezama ndani ya bahari la penzi lako siwezi kusonga mbele kurudi nyuma sijielewi haya mapenzi ya fujo hayafai kama wanipenda jaribu kunipa raha
Ujumbe wa kimahaba kumuomba mpenzi wako asichoke kuwasiliana na wewe kwa kutumia simu
Updated at: 2024-05-25 15:25:47 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Simu huboa wakati mwingine, kwani ni lazima ufungue meseji na kuzisoma, kuichaji simu kila mara, lakini usichoke kwani ndiyo inayotuwezesha tuwasiliane
SMS nzuri ya mapenzi ya kimahaba ya kutuma kwa mpenzi wako umpendaye
Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu.
Updated at: 2024-05-25 15:37:51 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu. Mawazoni ama ndotoni, Daima wewe hutawala, Kila asubuhi niamkapo, Nao usiku nilalapo, U chakula changu akilini, Nalo tulizo langu moyoni, Daima huuwaza upekee, Wewe uliojaaliwa, Na hivyo naihisi furaha, Daima wewe uwapo, Mawazoni mwangu.
Updated at: 2024-05-25 15:35:59 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mpenzi wangu T tambua kuwa ulimwengu tunaoishi una mambo muhimu matatu. Jambo la kwanza ni kumpata umpendaye, la pili ni kupata atakayekupenda la tatu ambalo ni kubwa kuliko yote ni kwa jambo la kwanza na la pili kuungana pamoja.
Nashukuru nimekupata wewe nikupendaye, naomba unipende na uungane name
Updated at: 2024-05-25 15:26:09 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Salamu yako ni nusu ya uhai wangu, kuikosa nisawa na kuidhulumu nafsi yangu, kuipata nisawa na ua ridi machoni mwangu, nakila ninapoipata huwa najisikia faraja moyoni mwangu, Nakupenda sana Muhibu wangu.
Updated at: 2024-05-25 15:25:30 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ni ngumu kwa watu wawili kupendana wanapoishi Dunia tofauti, lakini Dunia hizo zikutanapo na kuwa kitu kimoja, hiyo ndiyo maana ya kuitwa wewe na mimi.