Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Kilichotokea kati ya mkaka na mdada walipokutana hotelini
Mkaka aliingia kwenye hoteli moja akaketi meza moja na mdada mrembo maarufu sana; MKAKA: Samahani dada sijui saa ngapi? MDADA: Nani kakwambia saa yangu ndio ya kuangalia kila mtu?
Updated at: 2024-05-25 18:08:53 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mkaka aliingia kwenye hoteli moja akaketi meza moja na mdada mrembo maarufu sana; MKAKA: Samahani dada sijui saa ngapi? MDADA: Nani kakwambia saa yangu ndio ya kuangalia kila mtu?
MKAKA: Samahani sanaβ¦.jamaa akachukua Galaxy yake akapiga simuβ¦.aise saa ngapi saa hizi? mi ndio nimeingia toka USA nataka kurekibisha saa yangu ifwate muda wa huku. Na wewe uwahi kuchukua iPad nimekuja nazo tatu tu za zawadi. Halafu ntafutie mtoto mzuri nimumwagie midola niliyokuja nayo, ok ciao tuonane badae. MDADA: Kaka samahani saa hizi ni saaβ¦.. MKAKA: Achana na mimi wewe
Zuzu kaniuliza, "Anko, unajua vitu vinavyoanzia na K ni vitamu sana."
Nikashtuka, "Astaghafilulah we mtoto! Niondolee wehu wako hapa!"
Updated at: 2024-05-25 18:05:22 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Zuzu kaniuliza, "Anko, unajua vitu vinavyoanzia na K ni vitamu sana."
Nikashtuka, "Astaghafilulah we mtoto! Niondolee wehu wako hapa!"
Zuzu akatabasamu. Akaendelea kuongea kabla sijafanikiwa kumzuia. "Kweli kabisa anko. Vitu vinavyoanza na K ni vitamu sana kwa mfano kuku, kalimati, keki, kabab, katleti, kashata, kisheti na karoti."
Nikashusha pumzi. "Ahaa! Kumbe ndo hivyo, ni kweli!"
Zuzu akanitupia swali. "Kwani we anko ulidhani nini?"
MLEVI; "Nakunywa bia tano! MCHUNGAJI; "Bia moja bei gani!? MLEVU; "2500/ MCHUNGAJI; "Ulianza lini kunywa bia!? MLEVI; "Miaka 18 iliyopita!
MCHUNGAJI; "Kwa hiyo kwa siku unatumia zaidi ya 10,000?? MLEVI; "Ndio! MCHUNGAJI; "Kama u gekuwa unatunza hiyo pesa 10,000 kwa siku leo hii si ungekuwa na Range Rover!? MLEVI; "Samahani, naweza kukuuliza swali!? MCHUNGAJI; "Uliza! MLEVI; "Unakunywa bia!? MCHUNGAJI; "Hapana! MLEVI; "Nionyeshe Range Rover yako! MCHUNGAJI; "akasepa"
Updated at: 2024-05-25 17:15:27 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Et jana usiku mwiz kavunja mlango kwangu akaanza kutafuta kitu kila kona ikabid na mie niamke namuuliza unatafuta nini ananijibu hela ndipo nilipoanza na mie kutafuta nae maana hta hela ya kula Jana sikua nayo alichoka zaid nilipomuliza una uhakika uliweka humu? sipendagi ujingaπΆπ» na kitu hela mm!
Soma alichokisema mlevi baada ya kukuta watu wakimpiga mwizi
Updated at: 2024-05-25 18:01:04 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mlevi mmoja aliona wananchi wakipiga mwizi akawaambia "mwacheni msimpige, hii tabia yenu ya kupiga wezi mtakuja shtukia mnampiga Yesu, maana imeandikwa atakuja kama mwizi!"
Updated at: 2024-05-25 17:11:57 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MZARAMO V/S MCHAGA. Mzaramo alitangaza anatibu magonjwa yooooooote kwa tsh. 100,000/= Na kama akishindwa kukutibu anakurudishia laki yako nakukuongeza laki nyingine. MCHAGA akaona hii fursa yakujipatia hela aiwezi mpita akaenda kutibiwa. MZARAMO: "unaumwa nini?" MCHAGA: "Sisikii ladha ya aina yoyote mdomoni kabisaaaa.." MZARAMO: "sawa, toa laki kabisa.." Mchaga akatoa. MZARAMO akamuagiza msaidizi wake; "Naomba kikopo no.27 mpe anywe huyu.." MCHAGA akanywa akatema faster; "Puh puu puu, Aisee huu si mkojo huu..?" MZARAMO: "Umepona karibu tena.." Mchaga aka-mind sana Kesho yake akarudi tena hakuamini ameliwa pesa yake. MCHAGA: aisee nina tatizo la kumbukumbu nasahau sanaaaaa.." MZARAMO akamwambia "hakuna tabu, toa laki tukupe tiba..' MCHAGA akatoa pesa akijua leo lazima afanikiwe..' MZARAMO: "nesi naomba kikopo no.27.." MCHAGA: "ASA CHALII ANGU HICHO SI CHA JANA CHA MKOJO HICHO AISEE..?" MZARAMO: "UMEPONA KUMBUKUMBU UNAYO.