Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 17:10:24 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
01.π Wale wanafunzi walioongoza Mashuleni, wanaenda kwenye Engineering na Medical school.
02.π Wale waliokuwa wa pili, wanachukua MBA na LLB na kuja kuwa Mameneja wa wanafunzi walioshika nafasi ya kwanza.
03.π Wale waliokuwa wa tatu, wanageukia Siasa na kuwaongoza wote hapo juu. Yaani wa kwanza na wa pili.
04.π Wale waliofeli, wanaenda Jeshi, hawa wakigoma, basi hao wa juu wote hawana raha.
05.π Wale waliopata Zero na waliokataa shule wanakuwa waganga wa kienyeji, wote hapo juu watamtafuta huyu, pale mambo yao yanapokwenda kombo. Tuache kudharauliana, kila mtu ni boss akiwa kwenye nafasi yake. ππππππππππΏππΏπππππ
Updated at: 2024-05-25 17:09:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mtoto wa miaka sita alimuuliza babake: MTOTO: Baa, eti sisi wanadamu tulikuja vipi duniani? BABA: Mungu alimuumba Nabii Adam na Hawa. Kisha wao wakaanza kuzaa watoto na watoto wakazaa mpaka tukazaliwa sisi. (Mtoto hakuridhika akamfuta mamake) MTOTO: Mma, eti sisi wanadamu tulikuja vipi duniani? MAMA: Wanasayansi wamesema sisi tulitokana na manyani baadae tukawa binadamu. (Mtoto akarudi kwa baba) MTOTO: Baa mbona mama ansema sisi tulikuwa manyani mwanzo?Au wanidanganya? BABA: Mwanangu, mimi nimekuelezea kuhusu ukoo wetu. Mamako amekuelezea kuhusu ukoo waoπππΆπΌπΆπΌπΆπΌ
Updated at: 2023-04-29 22:53:38 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Karibuni tuangalie aina hizi 10 za ndoa.
1. NDOA YA MKEKA
Inatokana na kufumaniwa na Binti wa watu. Ndoa hii huwa Haina mahari. Hii huvunjika mwaka mmoja tu,baada ya wanandoa kugundua hawakuwa wakipendana!
2. NDOA YA MIHEMKO (NYEGE)
Hufungwa na vijana wenye umri wa miaka kati mume18 mke 16.Huvunjika baada ya miaka 3 au 4 ya ndoa.
4. NDOA YA MAONYESHO
Wenye ndoa Hii hupenda kujionyesha barabarani.Ila ndani hazina utii.Hupigana kila wanaporudi kutoka kwenye mizunguko. Cha kushangaza huwa hazivunjiki lakini ndiyo ndoa zinazoongoza kwa kuchepuka!
5. NDOA YA UHAMISHO.
Hufungwa na watumishi wa vijijini na mjini. Ili wa kijijini ahamie mjini.Mahari utoa anaetaka kuhamia mjini. Hata kama mahari atatoa mume lakini hii ndiyo ndoa yenye ukakasi zaidi.Huvunjika mara tu wanapoanza kuishi wote mjini. Salama ya hii ndoa ni kuhama kutoka mjini kwenda kijijini.
6. NDOA YA MIMBA.
Hufungwa kwa sababu wanaoowana hawataki kuonekana makwao kuwa wamezaa nje. Au muolewaji alikuwa hampendi muoaji kwa dhati.Muoaji hutumia mimba kama mtego wa kuingia ndoani. Hii huvunjika mtoto akizaliwa na kufikisha mwaka 1.
7. NDOA YA MALI (UTAJIRI)
Muolewaji miaka 18 au 28 Muoaji 65 au 70.Ndoa hii pia huitwa ndoa ya babu na mjuukuu. Ndoa ya aina hii hudumu, kwasababu mwenye kauli ni mwenye mali. Asilimia kubwa ya waume wa ndoa hizi hulea watoto wasio wao.
8. NDOA YA KWASABABU.
Hufungwa ili mradi muoaji au muolewaji aonekane tu kwa jamii kuwa naye kaoa au kaolewa.Huwa hazina utii wala upendo dhati. Ndoa ya aina hii ikifikisha miaka 4 huwa hazivunjiki wahusika huishi kwa mazoea.
9. NDOA YA UPENDO.
Ndoa hizi ziliishia mwaka 1978 kabla ya vita vya kagera.Muoaji na muolewaji hawakuangalia vitu ila utu tu ambao uliwaunganisha na kutengeneza upendo wa kudumu. Hii ilidumu miaka yote.
10. NDOA KUCHUMA
Ndoa hii ufungwa ili mradi muoaji au muolewaji akapate kitu au vitu fulani kutoka kwa upande mmoja wapo. Hii hudumu miaka kadhaa kutegemea na malengo ya mhusika. Wengine husubiri mpaka mhusika afe,lkn hujikuta wanakufa wao kwanza. Kuwa mwangalifu!