Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
KICHEKESHO: Ajira ngumu!! Cheki hawa walivyoamua kujiajiri
Updated at: 2023-04-29 22:52:42 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Jamaa mmoja alienda kuomba kazi Mbuga ya Wanyama, akaambiwa nafasi ya Kazi ipo ila hakuna Sokwe, "hivyo utajifanya Sokwe na tutakupa ngozi utavaa"
Jamaa siku ya kwanza akavaa, walipokuja watalii mambo yalienda vizuri, Siku iliyofuata Banda lake liliwekwa juu ya Banda la Simba, Jamaa ktk kuongeza mbwembwe akawa anarukaruka, kwa bahati mbaya si akaangukia ndani ya Banda la Simba, akawa anapiga kelele "Mama nakufaaa!"
Mara yule Simba akamwambia "Acha Ufala ww kelele za nini sasa, mimi mwenyewe Binadamu! rudi kwenye Banda lako kabla watalii hawajaja watatushtukia! chezea ajira ww"β¦β¦β¦!!
Updated at: 2024-05-25 17:45:32 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Et jana usiku mwiz kavunja mlango kwangu akaanza kutafuta kitu kila kona ikabid na mie niamke namuuliza unatafuta nini ananijibu hela ndipo nilipoanza na mie kutafuta nae maana hta hela ya kula Jana sikua nayo alichoka zaid nilipomuliza una uhakika uliweka humu?
Wanaume ni noma, Angalia wanachokifanyaga wakimwona mwanamke
Updated at: 2024-05-25 16:59:33 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Wanaume ni viumbe WASTAARABU sana..Mdada anapokua kavaa BIKINI na BRA tu, 98% ya mwili wake unakuwa waziβ¦Sisi kwa USTAARABU huwa tunaangalia pale PALIPOFUNIKWA..Hatutaki Dhambi za Kijinga kabisa Sisiβ¦
Updated at: 2024-05-25 17:54:11 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kama umesoma st Kayumba utakuwa una aidia na hayaβ¦
1.Unaenda shule umechelewa unakuta mwalim anakamata wachelewaj unaamua urudi nyumbani 2.unachukua kimbegu cha ubuyu unasugua sakafuni af unamuunguza mwenzio 3.mkiruhusiwa tu unakimbia unataka uwe wa kwanza kwenye njia yenu y kurudia nyumban 4.MTU akikukera unamfungia shule (mnapigana baada ya kufunga shule) 5.MTU akikunyima kitu chake unamwambia "Ahaa eeh utaona sa nne" 6.wadada wembamba ndo wanaongoza kwa kusuta wenzao 7.ukiibiwa daftar jipya unalia kuliko hata uliloandika 8.unajaza mapeni kwenye mkebe(compass) na mengine hayaandiki 9.vifaa vingine kwenye mkebe hujawahi hata kuvitumia mfano bikari labda utolee mwibaπ 10.hakuna habari nzur kama kuambiwa Leo hamna shule mwalim haupo 11.habari mbaya zaidi n kurud nyumban kutoka shule una njaa af unaambiwa chakula mgeni kaja tumempa 12.mtoto wa mwalim utamgundua tu kwanzia sweta begi na viatu vyake 13.usiombee umpige mtoto wa mwalim utataman uache shule 14.unatengeneza kifutio cha ndala af unatishia eti kinafuta hadi peniπ 15.ukaguzi na huna ufagio.. unaomba chelewa kwa watu af unaongeza kijiti katikati 16.siku ukienda na ufagio wanakagua maji, ukienda na naji wanakagua kuni au mboleaπ π Dah shule zetu hizi kiboko!!
Updated at: 2024-05-25 16:59:56 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
JE WAJUA!β¦..
Msuli mrefu kuliko yote kwenye mwili wa binadamu unaunganisha kope za macho na sehemu ya kutolea haja kubwa ndo mana kila ukijaribu kubana jicho moja sehemu ya haja kubwa hufunguka bila kutarajia?
Updated at: 2024-05-25 17:03:30 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Bosi wangu karudi safari yake kutoka serengeti..! Si akanitumia picha, lakini ilikuwa network yenyewe tabu.. kwahio picha haikufunguka na kwa vile niliona itachelewa kufunguka na ataona sikumjibu basi nami..
Nikampelekea msg nikamuandikia umependeza saana bosi mashaallahβ¦!! sasa baada tu ya kumfika msg.. na huku picha ikafunguka kumbe picha ya Sokwe..!! Basi Kaniambia kesho niende ofsini kwake kuna barua yangu.. Nahisi hyo barua ina pesa, hapa cjalala, nmekosa usingizi kabisa,nawaza ninunulie nn hyo pesa.Na kesho asubuhi sa 12 asubuhi atanikuta ofisini kwake naisubiri barua, sipendagi ujinga mimi.
Kilichotokea baada ya polisi wa kibongo kukutana na mwizi mzungu
POLISI KAKAMATA MZUNGU 'yestaday I saw u at ze maize shop..(jana nilikuona dukani kwa muhindi) when u saw me u started 2 six six.(uliponiona ulianza ku-sitasita) u ran n decided 2 plant a car.
Updated at: 2024-05-25 18:03:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
POLISI KAKAMATA MZUNGU 'yestaday I saw u at ze maize shop..(jana nilikuona dukani kwa muhindi) when u saw me u started 2 six six.(uliponiona ulianza ku-sitasita) u ran n decided 2 plant a car.(ulikimbia na ukaamua kupanda gari) zen u pot-cry me through ze window.(kisha ukanichungulia dirishani) now sleep down n snake well b4 I cut u a millet.(sasa lala chini kisha nyooka vizuri kabla sijakukata mtama) Chezea lugha wewe..!!!