Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 10:37:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Samaki (Tilapia 2) Nyanya ya kopo (Tomato tin 1) Kitunguu (Onion 1) Tangawizi (ginger kiasi) Kitunguu swaum (garlic clove ) Mafuta (Vegetable oil) Pilipili (scotch bonnet pepper 1) Tui la nazi zito (coconut milk 2 vikombe vya chai) Curry powder 1/2 cha kijiko cha chai Binzari nyembamba ya unga (ground cumin 1/2 kijiko cha chai Binzari manjano (turmaric 1/2 kijiko cha chai Chumvi (salt) Limao (lemon 1) Giligilani (fresh coriander)
Matayarisho
Marinate samaki na chumvi, limao, kitunguu swaum, tangawizi kwa muda wa masaa 6 au zaidi. Baada ya hapo wakaange au waoke katika oven mpaka waive ila usiwakaushe sana. Baada ya hapo saga pamoja nyanya ya kopo, kitunguu maji, kitunguu swaum na tangawizi. Kisha bandika huo mchanganyiko jikoni na upike mpaka ukauke maji kisha tia mafuta, binzari zote, curry powder, chumvi na pilipili na upike kwa muda wa dakika 5. Baada ya hapo tia maji kidogo (kama 1/2 kikombe) pamoja na tui la nazi. Acha uchemke mpaka tui liive na mchuzi ubakie kiasi. Baada ya hapo waweke samaki kwenye sufuria ya kuokea na kisha umwagie huo mchuzi juu ya hao samaki na owaoke (bake) kwa muda wa dakika 20. Ukisha toa kwenye oven katakata giligilani na utie kwenye hao samaki na hapo watakuwa tayari kwa kuliwa. unaweza kuwala na wali, ugali au chapati
Jinsi ya kupika Visheti Vya Kastadi Vya Shepu Ya Kombe
Updated at: 2024-05-25 10:34:51 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Unga wa ngano 1 Kilo
Siagi ¼ kilo
Mayai 2
Kastadi (custard) 3 vijiko vya supu
Baking powder 1 kijiko cha chai
Maziwa 1 ½ gilasi
Mafuta Ya kukaangia kiasi katika karai
Maandalizi na upikaji
Weka unga katika bakuli kubwa kisha changanya na unga wa kastadi na baking powder. Tia siagi uchanganye vizuri. Tia mayai, kisha maziwa ya baridi uchanganye vizuri usiukande sana. Fanya madonge kisha kata vipande vidogovidogo kisha ubonyeze kwa kidole uvikwaruze kwenye chujio lenye tundu itokee shepu (design) yake.
5- Tia mafuta katika karai yakipata moto, kaanga visheti hadi viive. Usiache hadi vikageuka rangi sana.
6- Eupua, weka katika sufuria au chombo kikubwa kusubiri shira.
Vipimo Vya Shira
Sukari ½ kilo
Hiliki ilosagwa 1 kijiko cha chai
‘arki (rose flavor) 5 matone
Maji 1 gilasi
Namna Ya Kutyarisha
Changanya sukari na maji uipike hadi iwe nzito. Ukiona mapovu yanatoka tia hilik na ‘arki . Mwagia katika visheti uchanganye vizuri hadi vishike na sukari.
Updated at: 2024-05-25 10:34:54 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Unga 2 Magi (kikombe kibuwa cha chai)
Sukari 1/3 Kikombe cha chai Mayai 5
Siagi 4 Vijiko vya chakula
Hamira 1 Kijiko cha chakula
Baking Powder 1 Kijiko cha chai
Vanilla 1 Kijiko cha chai
Hiliki zilizosagwa 1 Kijiko cha chai
Sukari ya laini ya unga
(icing sugar) 1 Magi
Jinsi ya kuandaa na kupika
Unavunja mayai, unatia sukari, hamira, baking powder, vanilla na hiliki ikisha unapiga kwa kutumia mchapo wa kupigia keki. Unapiga mchanganyiko kwa muda wa dakika tano.
Unatia siagi kwenye sufuria na unaiyayusha na kuipasha moto mpaka iwe moto ikisha unaimimina kwenye mchanganyiko na unapiga tena kwa dakika mbili tu.
Unatia unga kwenye sinia au bakuli kubwa ikisha unamimina ule mchanganyiko kwenye unga na unaukanda kutumia mkono, mpaka ulainike.
Ukiona unga mwingi basi ongeza maziwa kidogo mpaka uwe sawa, na ukiona unga mwepesi sana basi unaweza kuongeza unga kidogo pia mpaka ukae sawa mfano wa unga wa maandazi.
Sukuma na ukate madonge kama unavyoyaona hapo juu. Tumia kifuniko cha chupa kwa kukatia kiduara kidogo katikakti ya madonge. Ukimaliza kukata madonge yote, yaweke kidogo yavimbe halafu teleka mafuta na uyachome. Ukitoa kwenye mafuta yachuje moto na kabla ya kupoa yawe moto moto yarovye kwenye icing sugar na uhakikishe yote yameenea sukari juu. Ukimaliza tia kwenye sahani acha zipowe na zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Jinsi ya kutengeneza Muhogo Wa Nazi Na Samaki Wa Kukaanga
Updated at: 2024-05-25 10:34:39 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Muhogo - 3
Tui La Nazi - 2 vikombe
Chumvi - kiasi
Pilipili mbichi - 2
Mafuta - 1 kijiko moja
Kitunguu maji - 1 kidogo
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Chambua muhogo ukatekate au tumia iliyo tayari. Chemsha muhogo katika sufuria kwa maji kidogo na chumvi, funika uive muhogo. Karibu na kukauka maji tia tui, kitunguu maji ulichokatakata na pilipili mbichi. Unaupika moto mdogo mdogo hadi ukauke tayari kuliwa na samaki au kitoweo chochote kingine
Updated at: 2024-05-25 10:37:27 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kupata takriban gilasi 6
Mabungo - 3
Maji - 6 au 7 Gilasi
Sukari - kiasi upendacho
Chumvi - kidogo sana
Namna Ya Kutayarisha:
Kata mabungo na toa nyama yake tia katika mashine ya kusagia. Tia maji, sukari na chumvi usage kidogo tu. Chuja kisha mimina katika jagi uweke katika friji. Mimina katika gilasi.
Updated at: 2024-05-25 10:23:06 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga wa ngano - magi 2 (vikombe vikubwa)
Hamira kijiko 1 cha chai
Sukari Vijiko 2 vya supu
Maziwa ¾ Magi
Siagi Vijiko 2 vya supu
Mafuta ya kukaangia kiasi
VIAMBAUPISHI:SHIRA
Sukari ¾ Kikombe
Maji ¾ Kikombe
Illiki ya unga kiasi
Zafarani kiasi
JINSI YA KUPIKA
Katika bakuli, changanya vipimo vyote pamoja na ukande unga usiwe mgumu wala laini sana uwe kiasi. Kisha fanya donge moja na iache pahali penye joto mpaka iimuke. Halafu weka mafuta ya kukaangia kwenye moto. Sukuma donge hadi liwe duara sio nyembamba sana, kisha katakata kama maandazi. Mafuta ya kisha pata moto choma mittai hukuunazigeuza hadi ziwive na kugeuka rangi. Katika sufuria tia vipimo vya shira na iache ichemke isiwe nzito sana. Mimina mitai kwenye shira na uzipepete, kisha weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Mapishi mazuri ya Wali Wa Kukaanga Kwa Kidari Cha Kuku
Updated at: 2024-05-25 10:23:11 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo vya Wali:
Mchele - 3 vikombe
*Maji ya kupikia - 5 vikombe
*Kidonge cha supu - 1
Samli - 2 vijiko vya supu
Chumvi kiasi
Hiliki - 3 chembe
Bay leaf - 1
Vipimo Vya Kuku
Kidari (chicken breast) - 1Kilo
Kitunguu - 1
Tangawizi mbichi - ½ kipande
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 7 chembe
Pilipili mbichi - 3
Ndimu - 2
Pilipilimanga - 1 kijiko cha chai
Mdalasini - ½ kijiko cha chai
Jira/Cummin ya unga - 1 kijiko cha chai
Maji - ¼ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Wali:
Osha na roweka mchele kisha weka sufuria katika moto tia samli ipashe moto. Tia hiliki, bay leaf, kaanga, kisha tia mchele ukaange kidogo. Tia maji, chumvi na kidonge cha supu, upike wali kama unavyopika pilau. *Maji kisia kwa kutegemea mchele ulivyo. *Unaweza kutumia supu yoyote badala ya kidonge.
Kuku:
Katakata kidari cha kuku vipande vya kiasi, weka katika sufuria, tia ndimu, bizari zote, chumvi. Katakata kitunguu vipande vidogodogo, pilipili, na kitunguu thomu (chopped), tia katika kuku. Chuna tangawizi mbichi tia katika kuku. Changanya vitu vyote vizuri. Tia maji kiasi ¼ kikombe tu kiasi cha kumkaushia kuku. Weka katika moto mpike huku unageuzageuza. Anapokaribia kukauka epua akiwa tayari kuliwa na wali (na saladi upendayo)
Jinsi ya kutengeneza Slesi Za Chokoleti Na Karameli
Updated at: 2024-05-25 10:34:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga - 1 Magi (vikombe vya chai)
Sukari ya browni - ½ Magi
Siagi iliyoyayushwa - 125 g
Nazi iliyokunwa - ½ Magi
MJAZO WA KARMEL (Caramel filling)
Syrup - 1/3 kikombe cha chai
Siagi iliyoyayushwa - 125 g
Maziwa matamu ya mgando - 2 vikopo (condensed milk)
MJAZO WA CHOKOLETI (Chocolate filling)
Chokoleti - 185 g (dark chocolate)
Mafuta - 3 Vijiko vya chai
MAANDALIZI
Changanya unga, sukari, siagi na nazi iliyokunwa kwenye bakuli mpaka unga ushikamane. Paka mafuta treya ya kuchomea kisha utandaze kwenye treya ya 20cm kwa 30 cm au (8 in kwa 12 in) unaweza kuweka karatasi ya kuchomea chini ukipenda. Choma kwenye moto 325˚C kwa muda wa dakika 15 mpaka 18 au mpaka ibadilike kuwa rangi ya browni. Kwenye sufuria ndogo tia syrup siagi na maziwa matamu ya mgando na changanya kwa moto mdogo mpaka uwe mzito kasha mimina juu ya keki uliyochoma na choma tena kwa muda wa dakika 20 mpaka karameli iwe rangi ya dhahabu. Kwenye sufuria ndogo nyingine tia vipande vya chokoleti na mafuta na ukoroge kwa moto mdogo mpaka iyayuke kisha wacha ipoe kidogo mimina juu ya mjazo wa karameli kisha weka kwenye friji mpaka ishikamane. Kata vipande weka kwenye sahani tiyari kwa kuliwa