Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 10:23:02 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (plain flour) 1/4 Kitunguu kikubwa (chopped/slice onion) 1 Yai (egg) 1 Chumvi (salt) Mafuta (cooking oil)
Matayarisho
Tia unga, chumvi na maji kiasi katika bakuli kisha koroga mpaka madonge yote yaondoke. Baada ya hapo tia yai na vitunguu kisha koroga tena mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri. baada ya hapo choma chapati zako kama kawaida (jinsi ya kuchoma unaweza kuangalia kwenye recipe yangu ya chapati za maji katika older posts) na baada ya hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kabichi 1/2 kilo Nyanya ya kopo 1/2 Kitunguu 1 Curry powder 1/2 kijiko cha chai Chumvi Olive oil
Matayarisho
Kwanza kabisa bandua magada ya juu ya kabichi, kisha ioshe na uikaushe maji baaba ya hapo katakata kabichi (inapendeza zaidi kama ikikatwa nyembamba) kisha saga pamoja nyanya na kitunguu. Baada yahapo tia katika sufuria ya kupikia, ipike mpaka maji yote yatakapokauka kisha tia chumvi, curry powder na mafuta pika kwa muda kiasi kisha tia kabichi na upunguze moto. Pika mpaka kabishi itakapoiva kisha ipua na itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila kwa wali au ugali.
Updated at: 2024-05-25 10:34:47 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Wali wa hoho ni chakula maalum kinachotumika katika hafla au sherehe. Ni chakula chenye ladha nzuri na kina muonekano wa kuvutia kinapokuwa mezani tayari kwa kuliwa.
Mara nyingi huandaliwa kama zawadi katika harusi hususan kwa watu wa pwani. Kwa kuwa zawadi hiyo au maarufu kama kombe huwa kuna vyakula vingi, ikiwamo chakula hiki ambacho hufanya kombe kuwa na muonekano wa kupendeza.
Mbali na kuliwa kama kombe chakula hiki kinaweza kuandaliwa kama mlo wa usiku.
Mahitaji:
• Mchele ½ kg • Nyanya 3 • Mafuta ya kupika ¼ kikombe cha chai • Chumvi kiasi • Kitunguu swaumu kilichosagwa kijiko 1 cha mezani • Kitunguu maji kilichosagwa kijiko 1 cha mezani • Hoho 4 • Nyama ya kusaga ¼ • Tangawizi kijiko 1 cha chakula • Limao au ndimu kipande
Maadalizi:
• Chukua mchele uoshe vizuri kasha chuja maji • Chukua nyama ya kusaga na kamulia ndimu, weka chumvi na tangawizi, changanya vizuri na weka jikoni.iache ichemke hadi ikauke maji yote. • Chukua maji na kiasi cha robo tatu lita chemsha na weka pembeni • Chukua sufuria kavu yenye uwezo wa kupika kiasi cha kilo moja • Weka mafuta ya kupika kiasi cha vijiko vitatu na acha yapate moto • Weka vitunguu maji, menya nyanya na katakata halafu weeka katika sufuria hiyo. • Weka chumvi na kanga hadi vilainike kabisa • Baada ya kuiva weka vitunguu swaumu na baadaye mchele • Koroga hadi uchanganyike na weka nyama. Endelea kukoroga, baada ya hapo weka maji kiasi cha kuivisha mchele huo. Acha vichemke hadi vikaukie. • Palia mkaa juu yake au kama unatumia jiko la gesi au umeme weka kwenye oven hadi maji yakauke kabisa. • Baada ya hapo chukua hoho na kasha kata upande wa juu kama vifuniko. Kasha ondoa matunda ya ndani yake. Funika na kasha zipange kwenye sufuria yenye maji na chumvi na mafuta kidogo kiasi cha kijiko kimoja. Chemsha jikoni hadi ziive. • Baada ya kuiva, chukua hoho zako na kasha chota wali kw akutumia kijiko kasha jaza katika kila hoho na weka kwenye sahani tayari kwa kuliwa. • Unaweza kupamba na salad ukipenda.
Updated at: 2024-05-25 10:23:09 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga wa mchele - 500g
Samli - 250g
Sukari - 250g
Hiliki iliyosagwa - 1/2 kijiko cha chai
Arki (rose flavour) - 1/2 kijiko cha chai
Baking powder - 1 kijiko cha chai
Mayai - 4
Maji ya baridi - 1/2 kikombe cha chai
MAANDALIZI
Saga sukari iwe laini kiasi, changanya unga wa mchele, baking powder, hiliki na sukari. Pasha moto samli mpaka iwe nyepesi kama maji mimina kwenye ule mchanganyiko wa unga wa mchele, kisha uchanganye pamoja na arki. Ongeza mayai yaliopigwa endelea kuchanganya mpaka unga umeanza kuchanganyika vizuri. Ongeza maji ya baridi sana kama nusu kikombe tu ili uchanganyike vizuri. Kata kwa design unayotaka viwe vinene visiwe kama cookies za kawaida kama ilivyo kwenye picha na ukipenda utaweka kidoto kwa kutumia zaafarani katikati ya kileja kama inavyoonesha hapo juu. Choma kwa moto wa baina ya 300F na 350F kwa dakika 15 mpaka 20 visiwe vyekundu toa na tayari kwa kuliwa.