Sidebar with Floating Button
AckySHINE 🔁
AckyShine

Nia yako isishindwe

Featured Image
0 💬 ⬇️

Angalia utofauti wa mawazo ya maskini na tajiri

Featured Image

Maskini hudhani utajiri ni chanzo cha matatizo.
Tajiri hudhani umaskini ni chanzo cha matatizo.

Maskini hudhani ubinafsi ni kitu kibaya. Tajiri hudhani ubinafsi ni kitu kizuri.

Maskini ana mawazo ya kupata pesa bila kufanya kazi.
Tajiri ana mawazo ya kupata pesa kwa kufanya kazi.

0 💬 ⬇️

Ujumbe kwako wewe mwajiriwa au uliyejiari

Featured Image

Kama umeajiriwa au pia umejiajiri ni mojawapo ya njia zinazokuingizia kipato maana wengi wanaanzia hapo mpaka kuja kufikia kule wanakohitaji.
Ila kuna maswali machache ya kukupa changamoto ambayo nataka ujiulize:-

0 💬 ⬇️

Siri za mafanikio na Jinsi ya kufanikiwa

Featured Image

Tafuta fursa kila kona.
Tumia kipaji chako.
Kuwa na nidhamu katika fedha - matumizi mazuri ya pesa, nidhamu kwa watu wanaokuzunguka, usijikweze, usibague jamii, heshimu wote waliokaribu yako nk.

Kuwa na nidhamu katika afya yako: Afya ndio mtaji sahihi katika biashara yoyote - kuwa na mazoea ya kuangalia afya yako mara kwa mara nk.

0 💬 ⬇️

Njia nzuri ya kufanikiwa katika maisha

Featured Image

Kuna tofauti kubwa sana kati ya mtu anayejenga GHOROFA na yule anayejenga Nyumba ya KAWAIDA.

Anayejenga Ghorofa anatakiwa achimbe msingi Mrefu kwenda chini kabla hajaanza
kuinua Ghorofa yake juu. Hivyo wakati huyu mwingine anapokuwa anajenga Nyumba ya kawaida atakapokuwa tayari anakaribia hata kuezeka, unaweza kukuta yule anayejenga Ghorofa bado yuko kwenye Msingi.
Ila siku akianza kuinua Ghorofa lake, kila mtu atashangaa urefu wa juu atakaoenda nao.

0 💬 ⬇️

JITAMBUE: Kipi hauna kati ya pesa na muda?

Featured Image

Watu ambao hawana pesa ila wana muda wa bwerere. Hawajui thamani ya muda. Hawa ndo wale ambao hawajui cha kufanya. Anaamka mpaka analala usiku hana specific timetable. Unaweza kumkuta anaenda dukani ukamwambia nisindikize saluni na akakubali. Yupo yupo tu. Unaweza kuta ameingia Facebook hajui hata kwa mini. Basi tu kwa sababu ana bando. Akiperuzi akaona mahali wanaongelea mpira yumo

0 💬 ⬇️

Salamu za kuaga mwaka na kukaribisha mwaka mpya

Featured Image

Mwaka umefika mwisho, zimebaki siku tatu tu
kuingia mwaka mwingine lakini yapo mengi
niliyojifunza mwaka huu na pengine ningepesha
kushare:

0 💬 ⬇️

Jaribu kufikiria haya

Featured Image

1. Uelekeo ni muhimu kuliko kasi. Ni heri kwenda taratibu katika Uelekeo sahihi, kuliko kwenda kwa kasi katika Uelekeo usio sahihi.

2. Kulalamika mambo hayaendi wakati wewe mwenyewe hujui unakokwenda ni kuwa na matatizo ya akili.

3. Kasi yako inaamuliwa sana na umbali unaoweza kuona. Kama huoni chochote mbele ya maisha yako, basi huna chochote.

0 💬 ⬇️

Kanuni ya fedha ya matumizi na mipango ambayo itakusaidia ukiifuata

Featured Image

Jifunze kanuni za fedha
kama ilivyoainishwa hapo chini.
Fedha inatakiwa uwe na nidhamu nayo katika kutumia
Hii kanuni inatumika kwenye vyanzo vyako vyote vya fedha ili uwe na mafanikio yenye amani

0 💬 ⬇️

Ilinde ndoto yako

Featured Image

Ndoto ni nini?
Ndoto ambayo tunakwenda kuizungumzia sio ndoto unayoota ukiwa umelala ni ndoto ya mchana.
Ni kile kitu unachotamani kuja kukipata siku moja kabla hujaondoka duniani Ndoto inaweza kua katika makundi ya aina mbalimbali, unaweza kua na ndoto ya kuwa Rais, Mwimbaji bora, Mchezaji bora, Mwandishi Bora, Mfanyabiashara maarufu.
Vile vile unaweza kuwa na ndoto ya kumiliki vitu, nyumba nzuri ya kifahari sana labda ya milioni 300, Gari la kifahari sana, Unaweza kuwa na ndoto ya kumiliki utajiri au kuwa Bilionea,Kutembelea nchi fulani na kadhalika.

0 💬 ⬇️
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About