ACKYSHINE ARTICLE Β· PRINTABLE READER

MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI

✍️ SW - Melkisedeck ShineπŸ“… June 11, 2016πŸ’¬ 0 comments
πŸ—‚οΈ Biashara - Mbinu za Ujasiriamali na Biashara Kufanya tofauti#Karibu AckySHINE#SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF#Ujasiriamali: Kujitambua na Kuwa na Mafanikio Katika Maisha🌐 Kiswahili
MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI

✍🏽Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa.

πŸ‘‰πŸΎKatika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa

πŸ™‡πŸ½πŸ“š Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi 🏑 na πŸš— πŸš™magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!)

πŸ‘‰πŸΎWapo πŸ™‡πŸ½πŸ“šwasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana

πŸ‘‰πŸΎLakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga

Hii inachangiwa na mambo mawili:-
πŸ‘‡πŸ½
I. Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli

πŸ‘‰πŸΎHata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio

πŸ‘‰πŸΎKadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa!

πŸ™‡πŸ½πŸ“šWasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika
πŸ‘‡πŸΎ
II. Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani!

πŸ‘‰πŸΎKatika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha.

βœ‹πŸΎHuwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!

πŸ€”Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninakwambia: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani

πŸ›£Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti

😎Ukitaka kufanikiwa ungana na waliofanikiwa wakuelekeze

πŸ˜€πŸ™πŸ½ Hii habari haitaki hasira, vumilia tu na jiongeze

βœ…
Direct PDF download

The download button now generates the PDF on the server. It no longer depends on an off-screen browser canvas, so the former blank-PDF capture path is bypassed.