Watu wawili๐ฌ walikuwa wanakunywa pombe๐บ๐ป baa. Wakati wanakunywa wakaanza kubishana๐ ๐พโโ na baadaye ule ubishi ukawa ugomvi.
Mmoja akamrukia mwenzake akaanza kumpiga. Baada ya kumpiga kwa muda mrefu akagundua kuwa mwenzake hapumui tena.
Kumbe amemwua mwenzie.๐ฐ
Ndipo alipoanza kukimbia๐๐พ huku shati laki likiwa limechafuka sana na damu. Wale waliyokuwa wanauangalia ule ugomvi wakaanza kumfukuza.
๐๐พ ๐๐ฟโโ๐๐พ๐๐ฟโโ๐๐พ๐๐ฟโโ๐๐พ
Huyu mwuaji akakimbilia kwenye ๐ก๐๐พnyumba ya mtu mmoja mcha Mungu na akamwomba yule mtu amfiche maana ameua mtu na watu walikuwa wanamfukuza.
Yule mcha Mungu akasema nitakuficha wapi wakati mimi nina chumba kimoja tu?๐จ
Yule mwuaji akamjibu akamwambia acha kuendelea kupoteza wakati fikiria tu mahali pa kunificha. Yule mcha Mungu akavua shati๐ lake safi akampa yule mwuaji alafu yeye akachukua lile shati la muaji lililojaa damu akalivaa.
Akampa sharti yule mwuaji na kumwambia tunza shati langu usilichafue. Yule mcha Mungu alipofungua mlango wa chumba chake wale watu wakamvamia๐๐ฟโโ๐๐พ๐๐ฟโโ๐๐พ๐๐ฟโโ๐๐พ๐๐พ๐๐ฟโโ๐๐พ๐๐ฟโโ๐๐พ na kumpiga sana wakijua yeye ndo mwuaji huku mwuaji akiondoka salama na kurudi kwake.
Baada ya kumpiga sana yule ndugu akapelekwa polisi๐ฎ๐พ๐ฎ๐ฝโโ na baadaye akapelekwa mahakamani na akahukumiwa kunyongwa๐ด๐ผ kwa kumwua mtu mwingine.
Yule mwuaji halisi akiwa kule nyumbani alijisikia vibaya sana๐ akaenda mahakamani akajisalimisha akasema yeye ndiye aliyeua, yule ndugu aachiwe huru.
Hakimuโ akamwambia umechelewa, yule ndugu kesha nyongwa.
Alilia๐ญ๐ฉ sana na kujiambia kuwa yule mtu amekufa kwa kosa ambalo sio lake.๐ฐ
Akakumbuka maneno ya mwisho ya yule ndugu _*"LITUNZE SHATI LANGU USILICHAFUE."*_
Wapendwa,
YESU alikufa kwa ajili ya dhambi zako na zangu. Alichukua vazi letu lililochafuliwa na uchafu wa dhambi zetu akatupa vazi Lake takatifu la haki. YESU aliuawa kwa kosa lako na langu. Akatupa haki Yake na kutuambia tusichafue tena maisha yetu.
Kuendelea kutenda dhambi baada ya yale ambayo Yesu ametufanyia ni kuidharau sana kazi ya msalaba na kuikanyagia chini Damu Yake ambayo tumesafishwa kwayo.
Ni kushindwa kuthamini kuwa kuna mtu alishakufa kwa ajili yetu. Ni kushindwa kutambua uthamani wa wokovu ambao tumeupokea.
Wapendwa,
*Tutapataje kupona tusipojali wokovu mkuu namna hii?*
T A F A K A R I