ACKYSHINE ARTICLE ยท PRINTABLE READER

Jifunze kitu Kwenye mfano huu kuhusu Maombi na kuomba

โœ๏ธ DIN - Melkisedeck Leon Shine๐Ÿ“… January 17, 2017๐Ÿ’ฌ 50 comments
๐Ÿ—‚๏ธ Mafundisho ya Msingi ya Kanisa Katoliki: Makala za Katoliki#Karibu AckySHINE#Katoliki: Mifano ya Kufundisha#Katoliki: Sala na Kusali๐ŸŒ Kiswahili
Jifunze kitu Kwenye mfano huu kuhusu Maombi na kuomba

Nabii mmoja aliumwa
na Jino, lilimtesa sanaโ€ฆ
Akapiga magoti kumlilia
Mungu ili amponye..
Mungu akamuonesha mti
flani ili majani yake
Yapate kumtibu..
Akaenda kwenye mti ule,
Akachukua majani yake
akatumia na kweli
akaponaโ€ฆ
Baada ya Muda Mrefu
Kupita, nabii yule aliumwa
na Jino tenaโ€ฆ
Safari Hii alienda
moja kwa moja kwenye mti
Na kuchuma majani yake
na kuyatumia,Lakini
hakupona..
Akaja tena Kwa Mungu
na kumwambiaโ€ฆ
"Mbona ule mti niliutumia
Haukuniponyesha kama
Wakati ule? "
Mungu akamjibuโ€ฆ
"Mara ya Mwanzo ulipona
Kwa kuwa
ulinitegemea mimi, mara ya
Pili hakupona kwa kuwa
Uliutegemea Mti"..

KILA WAKATI TUNAPASWA
KUMUOMBA NA
KUMTEGEMEA MUNGU,
HATA KAMA KWA JAMBO
AMBALO ALISHATUJIBU..
KWA KUTOKUFANYA HIVYO
NDIYO MAANA MARA
KADHAA
TUNAKOSA MAFANIKIOโ€ฆ

โœ”Tulipooomba mchumba
Tulipompata
Hatukuombea Ulinzi wa
ndoa zetu, matokeo yake
Ni vilio kwenye ndoa
Karibu zote..

โœ” Tuliomba watoto,
Tulipowapata
muda mwingi tukatumia
Akili zetu kuwalea
Na kusahau kumshirikisha
Mungu katika malezi yao,
mwisho wa yote
Tunaishia kusema
Watoto wa siku hiziโ€ฆ

โœ” Tuliomba kazi kwa Mungu ,
Tulipopata tukaanza
Kutumia akili zetu katika
Kazi hizo na kuanza
Kudharau wenzetu na
Kuzisaliti ndoa
na familia zetu..
โ–ช Familia zinaliaโ€ฆ
โ–ช Watoto wanalia
Baraka zitatoka wapi?

โ–ช Kabla ya Kupata kazi
Tulikuwa Hatukosi
Kanisani,
Hakukosi kwenye
Maombiโ€ฆ
TUMEPATA KAZI
TUMEKUWA BIZE
HAKUNA MAOMBI
WALA KANISANI..
Baraka zitokee wapi?
Mafanikio yatoke wapi?
Mshahara mkubwa
Lakini madeni kila siku,
Tena tunakopeshwa na
Tuliowazidi mshaharaโ€ฆ

Wapendwa tustuke..
Tumrudie Munguโ€ฆ
Tusisingizie uchawi..
Tumejiroga wenyewe..

Tumuweke Mungu mbele..

Tafakari chukua hatua

โœ…
Direct PDF download

The download button now generates the PDF on the server. It no longer depends on an off-screen browser canvas, so the former blank-PDF capture path is bypassed.