Afya ya uzazi inahusiana na mfumo wa uzazi wa mtu, na via vya uzazi kwa watu. Kwa hali hiyo basi inahusiana na mambo yote yanayojumuisha uzazi na ujinsia. Ina maana kuwa watu wana uwezo wa kukidhi mapenzi na usalama katika maisha yao, kwamba watu wana uwezo wa kuwa na watoto na pia wana uhuru wa kuamua, kama lini na kwa muda gani wapate watoto. Yaliyomo humu yanampa haki mwanamume na mwanamke kupewa habari au kuelekezwa na kufikiwa na njia za uzazi wa mpango ambazo ni salama, zinazofanya kazi, anazomudu kulipia na njia zinazokubalika za uzazi wa mpango alizochagua na haki ya kuwa na huduma za afya zinazofaa ambazo zitawawezesha wanawake kuwa salama wakati wa ujazito na kujifungua.