Haki za binadamu ni haki zinazohusiana na mambo ya msingi na asili ya uhuru na heshima ya ubinadamu ambapo watu wote wamepewa haki ya kupata heshima kama binadamu. Mara mtu azaliwapo mume au mke hupata haki hizi. Haki hizi zinatambuliwa kimataifa na zina usawa kwa watu wote. Nchi mbalimbali zimetia saini na kuidhinisha haki hizi za kimataifa na kufanya ni sehemu ya sheria zao pamoja na kuweka sera zinazolinda haki hizi. Haki za uzazi zina misingi yake katika haki za binadamu na pia zinahusiana na haki za mtu mmojammoja. Kupata habari juu ya ujinsia na mada zinazohusu afya ya uzazi. Mwanamke au mwanaume kuamua kwa uhuru na kuwajibika, kama unataka kujamiaana lini na nani. Uhuru wa maamuzi. Kuamua kwa hiari na kuwajibika juu ya idadi na muda wa kupishana katika kupata watoto. Kupata huduma za afya ya uzazi kwa urahisi. Haki za kufanya maamuzi kuhusu afya ya uzazi, kwa uhuru, bila kunyanyaswa, kulazimishwa, bila kutumia nguvu pamoja na maamuzi nani wa kufunga naye ndoa. Kujilinda kutokana na mila zenye madhara kama vile ukeketaji wa wanawake. Haki hizi zimerekebishwa tangu mkutano uliofanyika Cairo mwaka 19941.